Faida za kula Faida za kula Boga
Makala hii inakwenda kukueleza faida za kula maboga, na mbegu zake kwa afya yako
19. Boga (pumpkin)
Boga ni katika vyakula vya asili walivyotumia mababu zetu toka enzi za zamani sana. Boga ni katika chakula chenye vitamin A. pia boga husaidia katika kushusha presha kwani mna kwenye mbegu za maboga aina ya mafuta pytoestrogens ambayo ndio hupunguza shinikizo la damu (hypertension).
Maboga husaidia katika ku[ata usingizi mnono kwani mna kwenye mbegu za maboga typtophan aina ya amino asid ambayo husaidia katika kurelax. Pia mna beta-carotene na aina zingine za antioxidant ambazo husaidia katika kuzuia kupata cancer.
Maboga ni muhimu katika kuboresha na kuimarisha afya ya nguvu za kiume. Pia chakula hiki ni muhimu kwa afya ya moyo. Kwani kutokana na kambakamba zilizomo kwenye maboga mlaji anakuwa na nafasi ndogo sana ya kuweza kupata mabonjwa ya moyo (coronary heart diseases).
Chakula cha maboga pia husaidia katika kuzuia na mlaji kupata ugonjwa wa kisukari. Pia huimarisha vyema afya ya mwenye kisukari. Chakula hiki husaidia katika ufyonzwaji wa glucose kwenda kwenye tishu za mwili. Pia husaidia katika kubalans kiwango cha sukari ndani ya mwili.
Maboga husaidia katika kuboresha na kuimarisha mfumo wa kinga mwilini (immune system). kwani vitamin C pamoja na beta-carotene husaidia mara dufu katika kuimarisha mfumo wa kinga ili kuweza kupambana na maradhi mbalimbali mwilini. Isitoshe beta-carotene kuweza kubadilishwa kuwa vitamin A, na hali hii huweza kusaidia katika kuzalishwa kwa seli hai nyeupe mwilini ambazo ndio hupambana na maradhi na vijidudu vishambulizi kama bakteria, fangas na virusi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Simulizi za Hadithi Audio π2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π3 web hosting π4 kitabu cha Simulizi π5 Dua za Mitume na Manabii π6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Fahamu kuhusu maji, kazizake mwilini na athari za upungufu wake mwilini
Hpa utafahamu faida za maji mwilini pamoja na athari za upungufu wa maji mwilini na dalili zake
Soma Zaidi...Faida za kiafya za kula pera
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula pera
Soma Zaidi...Vyakula bora kwa ajili ya afya ya macho.
βMacho ni moja ya viungo muhimu zaidi vinavyokuunganisha na ulimwengu, lakini mara nyingi tunayasahau hadi pale tunapoanza kupata changamoto za kuona. Kama ilivyo viungo vingine, macho yanahitaji virutubisho maalum ili yasibadilike ubora kadiri umri unavyosonga mbele. Makala haya yanakupa orodha ya vyakula bora unayoweza kuingiza kwenye sahani yako leo ili kuimarisha uwezo wako wa kuona
Soma Zaidi...Vyakula hatari na salama kwa vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula hatari na salama kwa vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Faida za kula Papai
Okoa afya yako kwa kula tunda papai, kwa hakika hutajuta, papai lina virutubisho vingi
Soma Zaidi...