Faida za kula Tango
Matunda ya zamani na ya asili, zijuwe faida za kiafya za tango
17.Tango (coccumber).
Tango ni katika mimea jamii ya matikiti na maboga. Tango ni katika matunda ambayo unatakiwa uyale sana kwenye maisha yako. Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 95 ya tango ni maji. Tango lina vitamin K, B vitamins, copper, potassium, vitamin C, na madini ya manganese.
Tango lina anti-inflammatory flavonol ambayo huitwa fisetin. Hii husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo. Hii husaidia katika kutunza kumbukumbu na kuimarisha afya ya mfumo wa fahamu pamoja na neva.
Tafiti zinaonesha kuwa tango lina polyphenols ambazo huitwa lignans (pinoresinol, lariciresinol, and secoisolariciresinol), husaidia katika kuzuia kupata aina mbalimbali za saratani (cancer) kama saratani ya kizazi kwa wanaume na wanawake.
Tango pia lina antioxidant flavonoids, kamavile quercetin, apigenin, luteolin, na kaempferol, ambazo husaidia katika kupambana na maradhi kama saratani na maradhi mengineyo.
Tango hupunguza joto tumboni, pia huondoa bajteria wanaoleta harufu mbaya mdomoni. Tafiti zinathibitisha kuwa tango husaidia katika kuondoa misongo ya mawazo na hii ni kutokana na uwepo wa vitamin B1, vitamin B5, and vitamin B7 (biotin) kwenye tango.
Tango huimarisha afya ya moyo na kupumguza shinikuizo la damu. Tanago husaidia mfumo wa kumengβenya chakula ufanye kazi kwa ufanisi. Tango husaidia katika kuthibiti uzito wa mwili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Madrasa kiganjani π2 Simulizi za Hadithi Audio π3 Dua za Mitume na Manabii π4 Bongolite - Game zone - Play free game π5 Kitau cha Fiqh π6 ai web app
Post zinazofanana:
Faida za kiafya za kula topetope/ accustard apple
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula topetope/ accustard apple
Soma Zaidi...Faida za kiafya za nyanya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyanya
Soma Zaidi...Faida za kula Ndizi
Kuna faida kubwa za kiafya kwa kula ndizi, soma makala hii mpaka mwisho
Soma Zaidi...Vyakula vya kuoambana na mafua
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua
Soma Zaidi...UPUNGUFU WA VITAMIN NA MAJI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...