Maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada

MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA NA BAADA

 

 

Hii ni hali inayowapata wanawake kwa kiasi kikubwa wakati wanaposhiriki tendo la ndoa. Maumivu haya pia yanaweza kumpata mwanaume ila kwa uchache sana. Hali hii kitaalamu inafahamika kama dyspareunia.

 

Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa uume unapoingia kwa mara ya kwanza, ama wakati wote wa kuingia na kutoka ama baada ya kumaliza tendo la ndoa. Maumivu ya wakati wa tendo la ndoa yanaweza kutokea kwenye uke, ama uume ama kwenye tumbo kwa kwa wanawake. Makala hii itakwenda kukuorodheshea sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa.

 

Sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa

1.Uke kuwa mkavu kutokana na maandalizi mabovu kabla ya kuingiza uume. Pia inaweza kuwa ni kutokana na kukosa hamu ya kushiriki tendo.

 

2.Kuwepo kwa majeraha kwenye uume ama uke. Majeraha haya yanaweza kuwa ni kukeketwa ana ya namna nyingine.

 

3.Kuwepo kwa uvimbe ama ukawa na matatizo ya ngozi katika sehemu za siri. Haya yote yanaweza kusababisha maumivu wakati wa kuingia kwa uume.

 

4.Maumbile ya uke. Wakati mwingine jinsi uke ulivyo inaweza kuwa ni tatizo. Kuwa uke mwingine unatabia ya kubana misui yake. Hali hii inaweza kupelekea maumivu wakai wa kupenya kwa uume.

 

5.Matatizo ya kimaumbile, kwa mfano kuwa na ukilema kwenye uke, ama kuwa na nyama ama ngozi ambayo inaweza kuzuia kupenya kwa uume.

 

6.Kuwepo kwa maradhi katka mfumo wa uzazi wa kike. Matatizo haya ya kiafya yanaweza kuwa kwenye ovari, ama kukawa na uvimbe ndani ya kizazi ama kukawa na shida katika mirija ya uretas.

 

7.Kufanyiwa baadhi ya matibabu katika maeneo ya siri. Kwa mfano baadhi ya matibabu ya saratani katika sehemu za siri, matibabu haya yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa

 

8.Matatizo ya kisaikolojia na misongo ya mawaso. Wakati mwingine uoga, kuwa na msongo wa mawazo ama kukumbuka maumivu uliyoyappata siku zanyuma, hali hizi zinaweza kupelekea maumivu wakati mwingine.

 

9.Staili iliyotumika wakati wa kufanya sex. Wakati mwingine mikao ya kufanya tendo la ndoa inaweza kuwa ni sababu ya maumivu. Ni vyema kutumia mikao iliyo rahisi



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-03     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1155


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Njia za kupunguza tatizo la kutanuka kwa tezi dume.
Posti hii inahusu zaidi njia ambazo tunaweza kutumia ili kuweza kupunguza tatizo hili la kutanuka kwa tezi dume, kwa hiyo tunaweza kutumia njia zifuatazo ili kuweza kupunguza tatizo hili kwenye jamii kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Siku za kupata ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata ujauzito Soma Zaidi...

Fahamu siku za kubeba mimba na zisizo za kubeba mimba.
Posti hii inahusu zaidi siku za kubeba mimba na zisizo za kubeba mimba , tunapaswa kujua hivi Ili kuweza kupanga uzazi na kuepuka njia ambazo ni hatarishi kwa afya zetu. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu fangasi za ukeni
Posti hii inahusu zaidi fangasi za ukeni, hili ni tatizo kubwa ambalo linawakumba watoto, akina dada na wanawake kwa hiyo na vizuri kujua Dalili zake na kuweza kuchukua hatua mapema. Soma Zaidi...

Sababu za mwanamke kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa
Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazosababisha kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Soma Zaidi...

Uume ukiwa unaingia na ukiwa ndani nahic maumivu Kama uke unawaka Moto tafadhali nishauri
Je unasumbuliwa namaumivi wakati wa nlishiriki tendo la ndoa ama baada. Huwenda post hii ikakusaidia. Soma Zaidi...

Fahamu dalili za hatari kwa wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa mama mjamzito, kwa sababu kuna baadhi ya Dalili zikitokea kwa mama mjamzito ni vizuri kabisa kuwahi hospitali mara moja. Soma Zaidi...

Madhara ya tumbaku na sigara
Post hii itakwenda kuangalia madhara ya tumbaku na sigara anayoweza kuyapata mvutaji Soma Zaidi...

Je tumbo huanza kukua baada ya mda gan?
Ni Swali kila mjamzito anataka kujiuliza hasa akiwa katika mimba ya kwanza. Wengine wanataka kujuwa ni muda gani anujuwe mavazi makubwa. Kama na wewe unataka kujuwa muda ambao tumbo huwa kubwa, endelea kusoma. Soma Zaidi...

Napenda kuuliza mke wangu anamuda wa wiki moja . tumbo na maziwa vinauma je dalili hizo zinawekuwa ni ujauzito...?
Maumivu ya tumbo kwa mjamzito huweza kuanaa kuonekana mwanzoni kabisa mwaujauzito, ndani ya mwezi mmoja. Ikabidi si dalili pekee ya kuwa ni mjamzito. Soma Zaidi...

Kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.
Post hii inahusu zaidi kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, hali hii utokea kwa watoto wadogo wakati wa kuzaliwa kwa sababu maalum kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

Changamoto za kwenye ndoa kwa waliotoa mimba mara Kwa mara
Posti hii inahusu zaidi changamoto za kwenye ndoa kwa wale waliotoa mimba mara Kwa mara,hizi ni changamoto za wakati wa kufanya tendo na mme wake au mtu mwingine kwa ajili ya kupata mtoto. Soma Zaidi...