Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo chini upande wa kushoto

MAUMIVU YA TUMBO KWA CHINI UPANDE WA KUSHOTO

 

Sehemu ya kushoto ya tumbo lako kwa chini hupatikana mwishilizo wa utumbo mkubwa. Pia kwa upande wa wanawake sehemu hii hupatikana ovari ya kushoto. Katika hali za kawaida maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto sio jambo la kuogopesha sana. Kwani maumivu haya yanaweza kuondoka yenyewe bila ya kuhitaji uangalizi wa kidaktari.

 

Je na wewe ni mmoja kati ya wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo kwa shini upande wa kushoto? Je una muda gani na tatizo hili?. makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakwenda kukujuza sababu za maumivu ya tumbo sehemu ya chini upand wa kushoto.

 

Kama nilivyotangulia kukuijuza kuwa maumivu haya si jambo la kuogopesha. Basi ni vyema kwa haraka ukamuona daktari endapo utaona dalili zifuatazo:-A.HomaB.Sehemu husika kuwa na ugumu na maumivuC.Kuvimba kwa tumboD.Kuona damu kwenye kinyesiE.Kuendelea kuwa na kichefuchefu na kutapika kwa masik kadhaaF.Kupungua uzitoG.Ngozi kuwa na njano.

 

Sababu za maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto1.Kuwa na shida kwenye utumbo mkubwa.Hii hutikea pale kwenye utumbo mkubwa kunapoota kama vijifuko vijidogo. Hivi sio jambo la kuogopa sana kiafya maana mara nyingi havina madhara na hupotea vyenyewe. Hali hii huwapata sana wenye umri zaidi ya miaka 40. sasa ikitokea vijifuko hivi vimeshambuliwa na vijidudu huvimba na kuleta maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto. Dalili zake ni kama:-

 

A.HomaB.KichefuchefuC.KutapikaD.Tumbo kujaa na kuiwa gumuE.KuharishaF.Kukosa choo

 

2.Gesi tumboni.Sababu nyingine ni kujaa gesi tumboni. Gesi tumboni inaweza kusababishwa na:-A.Kumeza hewa sanaB.Kula kupitilizaC.Kuvuta sigaraD.Kutafuna bigjiiE.Chakula kutokumeng’enywa vyemaF.Kula vyakula vyenye gesiG.Kuwa na bakteria kwenye utumbo mkubwa.

 

3.Kuvimbiwa ama chakula kutokumeng’enywa vyema tumboni. Hali hii huplekea maumivu ya tumbo kwa juu. Maumivu haya wakati mwingine husambaa na kuathiri chini ya tumbo upande wa kushoto. Mtu pia ataona dalili kama:-A.KiunguliaB.Kuhisi kishiba na tumbo kujaaC.Kucheua gesiD.kichefuchefu

 

4.Ngiri henia; henia ina dalili kama:-A.Kuongezeka uvimbe maeneo ya tumboni (si kila henia)B.Maumivu kuongezekaC.Maumivu wakati unaponyanyua kituD.Kujihisi umeshiba5. kuwa na vijiwe kwenye figoVijiwe vya kwenye vigo vinatokana na mkusanyiko wa madini ya chumvi. Vijiwe hivi vinaweza kutokea kwenye figo, kibofu ama maeneo mengine kwenye mfumo wa mkojo. Vijijiwe hvi vinaweza kusababisha maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto. Pia vinaweza kusababisha maumivu ya mgongo upande mmoja na nyuma pia na kwenye mbavu. Tofauti na dalili hizi pia mgonjwa anaweza kupata dalili zifuatazo:-

 

A.Mkojo wenye rangi ya kahawiya, nyekundu ama mawingu mawingu na haruu kaliB.Mkojo wenye maumivu makali unaotokea mra kwa maraC.KichefuchefuD.VomitingE.Homa

 

Maumivu ya tumbo kwa chini uapande wa kulia kwa wanawake, husababishwa na yafuatayo:-A.Tumbo la changoB.Kuota tishu za tumbo la uzazi maeneo mengineC.Kuwa na shida kwenye ovariD.Kuwa na ujauzito uliotungia njeE.Kuwa na ugonjwa wa PID

 

?



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/11/11/Thursday - 12:27:24 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 3749


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Athari za kutokutibu minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya athari zinazoweza kutokea endapo minyoo haitotibiwa Soma Zaidi...

Matibabu ya fangasi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu matibabu ya fangasi Soma Zaidi...

Dalili za saratani ya koo
Saratani ya Koo inarejelea Vivimbe vya Saratani vinavyotokea kwenye koo lako (koromeo), sanduku la sauti (larynx) au tonsils. Soma Zaidi...

Dalili za madonda ya koo
Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya koo, ni ugonjwa unaoshambulia sana sehemu ya koo la hewa, na na huwa na dalili zake kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Koo langu limekauka yaweza kuwa ni muadhirika?
kuwashwa na koo ni katika dalili za kuwa na maambukizi mwilini. Kuwa na maambukizi haimaanishi ni HIV ama UKIMWI laa hili ni neno pana. Hapa nitakujuza kwa ufupi kuhusu swali hilo la muulizaji kuwa anawashwa na koo. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa pepopunda kwa watoto
Pepopunda ni ugonjwa hatari wa kutishia maisha unaosababishwa na sumu inayojulikana Kama tetanospasmin inayotolewa kwenye majeraha yaliyoambukizwa. Bakteria ya pepopunda huingia kwenye mwili wa mtoto mchanga kupitia kisiki cha kitovu ambacho kimekatwa na Soma Zaidi...

Presha ya kushuka/hypotension
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu presha ya kushuka/ hypotension Soma Zaidi...

Ni Nini husababisha kinjwaa kutoa harufu mbaya?
Posti hii inaelezea kuhusiana na sababu zinazosababisha kinjwa au mdomo kutoa harufu mbaya? Soma Zaidi...

Ugonjwa wa upungufu wa maji mwilini.
Upungufu wa maji mwilini hutokea unapotumia au kupoteza Majimaji mengi zaidi ya unayonywa, na mwili wako hauna maji ya kutosha na Majimaji mengine ya kufanya kazi zake za kawaida. Usipochukua nafasi ya Vimiminika vilivyopotea, utapungukiwa na maji. Soma Zaidi...

Dalili za maumivu ya uti wa Mgongo
Posti hii inahusu zaidi dalili za uti wa mgongo ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uti wa Mgongo. Soma Zaidi...

Dalili za minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za minyoo Soma Zaidi...

Zifahmu Dalili za homa ya ini Kali ya pombe.
Posti hii inaonyesha dalili na Mambo Hatari yanayosababisha homa ya ini Kali ya pombe. Soma Zaidi...