image

Maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa

MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA TENDO LA NDOA

 

Maumivu wakati wa tendo la ndoa hutokea sana na pengine ni kawaida hasa kwa wanawake. Ijapokuwa kwa wanaume sio sana. Maumivu haya yanaweza kuwa ya tumbo, ya kiuno, ama viungo vya siri yaani uume na uke. Pia maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa tendo la ndoa ama baada.

 

Je na wewe ni katika wanaopatwa na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa. Na je umepata kujuwa chanzo cha tatizo lako?. makala hii ni kwa ajili yako. Katika makala hii tutakwenda kuona maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa.

 

Sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa.1.Mkao uliotumika. Ipo baadhi ya mikao inaongeza uwezekano wa kupatwa na maumivu ya tumbo wakati wa tendo. Mikao hii ni ile ambayo inaruhusu uume kuingia ndani zaidi. Kama unasumbuliwa na tatizo hili jaribu kutumia mikao ambayo utaweza kudhibiti uingiaji wa uume.

 

2.Kama tumbo la uzazi (uterus) limeinama kidogo. Hii hutokea pale tumbo la uzazi linapolalia nyuma kidogo kuelekea kwenye shingo ya uzazi. Hali hii huwewa kupelekea maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa.

 

3.Maka una tatizo la kuota tishu zinazopaswa kuota kwenye tumbo la uzazi zikaota sehemu nyingine. Hali hii hutambulika kama endometruisis. Haki hii huweza kupelekea maumivu ya mgongo, nyonga na tumbo wakati wa tendo la ndoa. Dalili za hali hii ni pamoja na:-

 

A.Maumivu makali zaidi wakati wa tendo la ndoaB.Kupata hedhi yenye damu nyingiC.Kutokwa na damu kabla na baada ya kumaiza hedhiD.Maumivu ya tumbo

 

4.Kama ovari ina matatizo yaani inajaa maji, hali hii hutambulika kama ovarian cysts. Hii hutokea endapo juu y aovari ama ndani kunkuwa na kama vijifuko vijidogo vinajaa maji. Sasa vikiwa vidogo havinaga maumivu ila vikiwa ni vikubwa vinaweza kupelekea maumivu ya chini ya tumbo. Maumivu haya yanaweza kuwa makali zaidi wakati wa tendola ndoa. Pia mtu anaweza kupata dalili zifuatazo:-

 

A.Maumivu ya mgongo wa chini ama kwenye mapajaB.Unahisi tumbo limejaa ama kushiba, ama tumbo linakuwa zitoC.Tumbo kujaa gezi na kucheua gesi kwa mdomoni.

 

5.Kama kuna mashambulizi kwenye kibofu kitaalamu hali hii huitwa interstial cystitis. Misuli ya kwenye kibofu inashambuliwa na kuvimba na baadaye kutoa dalili kama:-A.Maumivu ya tumbo na nyongaB.Kukojoa mara kwa maraC.Kujihisi kukojoa tena punde baada ya kukojoaD.Kuvuja kwa mkojo yaani kutoka mkojo bila ya wewe kujuwa.E.Maumivu kwenye uke na mashavu ya uke (papa)

 

6.Kuwa na uvimbe kwenye tumbo la mimba kitaalamu huitwa fibroid. Huu ni uvimbe usiosabababishwa na saratani. Uvimbe huuu huweza kuleta dalili kama:-A.maumivu ya tumbo na mgongo sehemu ya chiniB.Kupata damu nyingi ya hedhi pamoja na maumivu makaliC.Maumivu wakati wa tendo la ndoaD.Kukosa choo.

 

7.Kama mtu ana maradhi ya ngono kama gonoria na chlamydia. Hapa mtu anaweza kuona dalili kama:-A.Kutokwa na uchafu ukeniB.Kutoka na harufu mbaya ukeniC.Maumivu wakati wa kukojoa na kuhisi kama unaunguwaD.Maumivu ya tumbo kwa chini pamoja na nyongaE.Maumivu na kutokwa na damu wakati wa hedhi na baada ya hedi

 

8.UTI na PID; kwa pamoja haya ni mashambuizi ya bakteria ama fangasi ama virusi. Mashambulizi haya huathiri mfumo wa uzazi hapa itakuwa na PID na endapo yatashambulia mfumo wa mkojo itakuwa ni UTI. ugonjwa wa UTI na PID huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

 

Dalili za PIDA.Maumivu makali ya nyonga wakatii wa tendo la ndoaB.Maumivu wakati wa kukojoaC.Kutokwa na damu wakati wa hedhi na baada

 

Dalili za UTIA.Maumivu ya tumbo ambayo huongezeka wakati wa tendo la ndoaB.Maumivu wakati wa kukojoaC.Kukojoa mra kwa maraD.Mkojo mchafu na wenye harufu kali.

 

9.kama kuna uvimbe katika tezi dume.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/11/11/Thursday - 12:25:20 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1359


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Maelekezo muhimu kwa Mama au mlezi wa mtoto mgonjwa
Posti hii inahusu zaidi maelekezo muhimu kwa mama au mlezi wa mtoto mgonjwa. Ni maelekezo muhimu hasa wakati wa kutoa dawa kwa mtoto. Soma Zaidi...

je mwana mke ana weza kubeba mimba kama hayupo kwenye siku zake za hatali ama
Mimba haipatikani kila siku, na pia mimba huingia kwa siku moja na katika muda mmoja. Baada ya mimba kutungwa hakuna tena nafasi ya kutungwa mimba nyingine. Soma Zaidi...

Dalili za PID
Posti hii inahusu zaidi dalili za PID maana yake ni maambukizi kwenye pelvic kwa kitaalamu huitwa pelvic infection disease, ni ugonjwa unaoshambulia sana wanawake na wasichana Soma Zaidi...

Aina za uvimbe kwenye kizazi.
Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali za uvimbe kwenye kizazi, uvimbe unatokea kwenye kizazi ila utofautiana kulingana na sehemu ambazo uvimbe huo umepata. Soma Zaidi...

Dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14 Soma Zaidi...

Dalili za mimba changa
Zijuwe dalili 17 za mimba na mimba changa, kuanzia siku ya kwanza mpaka mwezi mmoja Soma Zaidi...

Kazi na mdalasini katika kutibu matatizo ya homoni.
Posti hii inahusu zaidi kazi ya mdalasini katika matibabu ya homoni kwa wanawake. Soma Zaidi...

Njia za kuzuia mimba zisiharibike.
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuzuia mimba zisiharibike, kwa sababu kila mama anayebeba mimba anategemea kupata mtoto kwa hiyo na sisi hamu yetu ni kuhakikisha kwamba mtoto anazaliwa kwa kuzuia mimba kuharibik Soma Zaidi...

Hatari ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito
Posti hii inahusu zaidi hatari za kutokwa na damu wakati wa ujauzito, hali hii utokea wakati wa ujauzito ambapo Kuna baadhi ya wajawazito utokwa na damu jambo ambalo hatupaswi kutarajia kwa sababu tunafahamu kabisa mama akishapata ujauzito na damu zinakom Soma Zaidi...

Sababu za Ugonjwa wa kifafa cha mimba.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kifafa cha mimba, kwa kawaida mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu sababu za kuwepo kwa kifafa cha mimba ila kuna visababishi vinavyofikiliwa kama ni Dalili za kifafa cha mimba kama ifuatavyo Soma Zaidi...

Ni ipi hasa siku ambayo nitafute ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kutafuta ujauzito Soma Zaidi...

Uchungu usio wa kawaida kwa akina Mama.
Posti hii inahusu zaidi uchungu usio wa kawaida kwa akina Mama, kwa kawaida uchungu unapaswa kuwa ndani ya masaa Kumi na mawili ila Kuna wakati mwingine uchungu unaweza kuwa zaidi ya masaa Kumi na mawili na kusababisha madhara yasiyo ya kawaida kwa Mama n Soma Zaidi...