MBINU WALIZOTUMIA MAKAFIRI WA KIQUREISH KATIKA KUUPINGA UISLAMU MAKKAH


image


Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)


mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah.

 

-    Maqureish wa Makkah walitumia kila mbinu kuhakikisha kuwa ujumbe wa Uislamu haufiki na kukubalika katika jamii yao, miongoni ni hizi zifuatazo;

 

  1. Kumkatisha tamaa Mtume (s.a.w) na wafuasi wake.

-  Makafiri walimdhihaki Mtume (s.a.w) na waumini wachache kwa 

    kumuita majina mabaya kama; mwendawazimu, mtunga mashiri, 

    aliyepagawa na mashetani, mchawi, n.k.

 

-  Pamoja na kusimangwa huko Mtume (s.a.w) na waislamu hawakukata 

    tamaa, waliendelea kuutangaza Uislamu katika jamii yote.

 

  1. Mbinu ya Vitisho na Kumkataza Mtume (s.a.w) kuulingania Uislamu kwa kumtumia Ami yake, Abu Talib.

 

-  Wakuu wa Maquraish walimuagiza Abu Talib amkataze Muhammad 

    (mwanae) kuendelea kuutangaza Uislamu kwa kumbadilishia mtoto 

    mwingine la sivyo watamshambulia yeye na Muhammad (s.a.w).

 

-  Mbinu hii haikufanikiwa badala yake Abu Talib alimuunga mkono 

    Mtume (s.a.w) kwa kazi yake baada ya kujua msimamo wake.

 

  1. Mbinu ya Kumhonga na kumrubuni Mtume (s.a.w).

-  Maquraish walitumia diplomasia kwa kumtaka Mtume (s.a.w) aache 

    kazi ya kuutangaza Uislamu kwa kumpa kati ya vitu vifuatavyo; 

    utajiri, mwanamke mzuri, madaraka au yote kama akitaka.

 

-  Mtume (s.a.w) aliwakatalia vyote hivyo kwa kumsomea aya za Qur’an 

    (41:1-37) mjumbe aliyetumwa kazi hiyo, Utbah bin Rabi’ah.

 

  1. Mbinu ya kutaka kumlaghai Mtume (s.a.w).

-  Maqureish walimletea Mtume (s.a.w) pendekezo kuwa washirikiane 

    katika ibada kwa awamu, mwaka mmoja wamuabudu Mungu mmoja 

    kwa pamoja na mwaka unaofuatia waabudu miungu yao pamoja pia.

 

-  Hapo ndipo iliposhuka suratul-Kafiruun kuvunja pendekezo lao hilo la 

    kushiki katika ibada na Mtume akawasomea aya za Qur’an kukataa.

    Rejea Qur’an (109:1-6) na (10:15).

 

  1. Mbinu ya Kuwatesa na kuwaua Waislamu.

-  Baada ya Maqureish kuona mbinu zote zimefeli, walianza kutumia 

   nguvu na mabavu kuwatesa, kuwanyonga na kuwaua Waislamu 

   waliong’ang’ani imani yao kama akina; Bilal bin Rabbah, Sumaiyya,      

   Ammar bin Yasir na baba yake, n.k.

 

- Pamoja na mateso na mauaji, waislamu walibakia na msimamo wao  

   bila kutetereka na kukata tamaa. 

 

  1. Mbinu ya fitina, kuipinga Qur’an na kuzuia watu kukutana na Mtume (s.a.w).

-  Maquraish kwa kuhofia ujumbe wa Qur’an kuenea kwa watu, 

    walianza kuzuia watu kwenda kuonana na Mtume (s.a.w) kwa 

    kuwashawishi kuwa wasisikilize aya za Qur’an kwani ni uchawi, 

    mashairi ya Muhammad.

 

-  Walizidi kufitinisha kwa kumzuia Mtume (s.a.w) kuswali na 

    kuwaambia watu kuwa Muhammad anapinga ibada na miungu wenu, 

    lakini mbinu na ushawishi wao ulifeli pia.

   Rejea Qur’an (31:6), (41:26), (10:38), (11:13) na (96:9-19). 

 

  1. Mbinu ya kuwatenga na kila huduma ya kijamii.

-  Maquraish walizidi kuongeza mateso kwa waislamu kwa kutenga na 

    kuwafukuza Makka na kwenda kuishi katika jangwa la Shi’ab miaka 

    mitatu bila chakula wala mahusiano mengine ya kijamii.

 

-  Mbinu pia ilifeli baada ya baadhi ya Maquiesh kuona huruma kwa 

    ndugu zao waliotengwa bila sababu za msingi, hivyo wakavunja  

    mkataba wa kuwatenga.

 

  1. Mbinu ya kutaka kumuua Mtume (s.a.w).

-  Maquish waliazimia kumuua Mtume (s.a.w) na rafiki yake Abubakar 

   (r.a) walipogundua kuwa waislamu wamehamia mji wa Madinah.

 

-  Mbinu hii pia ilifeli baada ya Allah (s.w) kuwanusu katika pango yeye 

    na sahibu yake Abubakar (r.a).

    Rejea Qur’an (9:40).



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    2 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    6 Maktaba ya vitabu    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Maana ya kusimamisha uislamu katika dini
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Madhumuni ya dola ya uislamu
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Wanaostahiki kupewa sadaqat
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Sababu za makafiri wa kiqureish kuupinga ujumbe wa uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Maswali juu ya Sunnah na hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kumkafini (kumvisha sanda maiti)
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Elimu ya mwingozo na elimu ya mazingira katika uislamu
Mahusiano kati ya elimu ya mwongizo na elimu ya mazingira katika uislamu. Soma Zaidi...

image Maana ya sadaqat
Nguzo za imani, maana ya sadaqat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)
Zifuatazo ni njia nyingi za kumjua Mwenyezi Mungu (EDK form 2:dhana ya elimu katika uislamu) Soma Zaidi...

image Zoezi la nne mada ya fiqh.
Maswali mbalimbali kuhusu fiqh. Soma Zaidi...