image

Mbinu za kupunguza Magonjwa ya kuambukiza.

Posti hii inahusu zaidi mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza kiwango cha kuwepo kwa magonjwa ya kuambukiza, kwa hiyo zifuatazo ni mbinu ambazo zinapaswa kutumika ili kupunguza kiwango cha magonjwa ya kuambukiza.

Mbinu za kupunguza Magonjwa ya kuambukiza.

1.kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa kuna magonjwa mengi ya kuambukiza ingawa tunajaribu kuyatibu ila si yote yanaweza kuisha ila kuna njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza kiwango cha kuwepo kwa magonjwa ya kuambukiza.njia zenyewe ni kama ifuatavyo.

 

2.Kuangalia mazingira.

Kwanza kabisa mazingira ya watu yanapaswa kuangaliwa, yaani maisha ya watu kwa ujumla kwa mfano usafi pakiwepo choo, maji yaliyochenshwa na kuchujwa na mambo mengine ambayo yanaweza kuwa chanzo cha uchafu.

 

2. Pia kuangalia chakula kinachotumiwa na watu wa kwenye mazingira kama kinaweza kuwasaidia watu kuweza kuwa na kinga ya kupambana dhidi ya magonjwa na jinsi ya kutumia chakula kama ni sahihi.

 

3. Vile vile tunapaswa kuangalia kama kuna mtu yeyote kwenye jamii ana Dalili za ugonjwa tunapaswa kukusanya sampuli na kuzipeleka maabara ili kutambua tatizo lililopo na kuweza kutatua tatizo kwenye mazingira.

 

4. Pia kama kuna Ugonjwa ambao umekidhiri kwenye jamii husika ambao unaleta shida na matatizo makubwa kwa jamii hiyo chanjo ni lazima ili kuweza kutokomeza Tatizo lililopo.

 

5. Tibu magonjwa yaliyomo kwenye mazingira kwa kutumia dawa mbalimbali ambazo zimeagizwa na wahudumu wa afya baada ya kugundua ugonjwa uliopo kwenye mazingira.

 

6 . Pia elimu inapaswa kutolewa kwa jamii baada ya kuangalia mazingira, chakula kinachotumiwa na watu waliopo kwenye mazingira husika ili kuhakikisha kuwa wanatumia chakula kwa kuzingatia mlo kamili na kuepuka utapia mlo kwa watoto na watu wazima.

 

7. Kuhakikisha kubwa mazingira yanakuwa masafi kwa kukata nyasi ndefu, kufukia mashimo,kuchoma takataka mbalimbali zilizoizunguka nyumba na kuhakikisha kuwa watu wamefundishwa namna ya kutunza mazingira na pia kuhakikisha kubwa wanachemsha maji na kuchuja kabla ya kunywa.

 

8. Kuhakikisha mazingira hayana wadudu wanaosababisha magonjwa, wadudu kama vile chawa, mbu, viroboto, kunguni na wengine wengi ambao ukaa kwenye mazingira ya watu, kama kuna dawa wanaweza kuuawa ili kupunguza Magonjwa.

 

9. Pia kuhakikisha watu wanapata mahitaji ya msingi ya maisha kama vile makazi, mavazi na chakula pia wapewe na dawa kama kuna Magonjwa vile vile na wale ambao hawajiwezi kabisa wanapaswa kutafutiwa huduma za kijamii kwa kupitia viongozi wa serikali.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 933


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Ugonjwa wa mfumo wa kinga ya mwili inavyoshambulia ini.
Ugonjwa huu hupelekea kuvimba kwenye ini yako ambayo hutokea wakati mfumo wa kinga ya mwili wako unaposhambulia ini lako. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa surua kwa watoto.
Surua ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na homa na upele mwekundu, unaotokea utotoni. Wakati mtu aliye na virusi akikohoa au kupiga chafya, matone yaliyoambukizwa huenea angani na kutua kwenye sehemu zilizo karibu. Mtoto anaweza kupata virusi kwa ku Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa wa uchovu sugu.
Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa uchovu sugu ni ugonjwa tata unaoonyeshwa na uchovu mwingi ambao hauwezi kuelezewa na hali yoyote ya matibabu. Uchovu unaweza kuwa mbaya zaidi kwa shughuli za kimwili au kiakili, lakini haiboresha kwa kupumzika Soma Zaidi...

Dalili za vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Sababu za mngurumo wa moyo
Mngurumo wa moyo ni sauti wakati wa mzunguko wa mapigo ya moyo wako kama vile kutetemeka inayotolewa na damu yenye msukosuko ndani au karibu na moyo wako. Sauti hizi zinaweza kusikika na kifaa kinachojulikana kama stethoscope. Mapigo ya moyo ya kawaida Soma Zaidi...

IJUE HOMA YA CHIKUNGUNYA (CHIKV) DALILI ZAKE, TIBA YAKE, CHANJO YAKE, NA MBU ANAYESAMBAZA HOMA HII
Haya ni maradhi ambayo husambazwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu kwa kupitia mbu. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa kisukari
Ugonjwa wa kisukari hurejelea kundi la magonjwa yanayoathiri jinsi mwili wako unavyotumia sukari kwenye damu (glucose). Glucose ni muhimu kwa afya yako kwa sababu ni chanzo muhimu cha nishati kwa seli zinazounda misuli na tishu zako. Pia ndio chanzo ki Soma Zaidi...

Aina za kisukari
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za kisukari Soma Zaidi...

MJUE MBU, NA YAJUWE MARADHI MAKUU MATANO (5) HATARI YANAYOAMBUKIZWA NA MBU, malaria kukamata namba moja kwenye maradhi hayo)
Mbu ni katika wadudu ambao husababisja vifo vya maelfu kila mwaka, na mamilioni ya watu wanaathirika na maradhi yaletwayo na mbu. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa Saratani ya ini.
Saratani ya ini ni Saratani inayoanzia kwenye seli za ini lako. Soma Zaidi...

Zijuwe kazi za ini mwilini
Katika somo hili na yanayofuata utajifunz akuhusu ini. Post hii ina muendelezo wa post zinazofuat. Katika mfululizo huuutajifunz akuhusu ini na maradhi yake na kujiking nayo. Soma Zaidi...

Sababu za mdomo kuwa mchungu
Hapa utajifunza sababu zinzopelekea mdomo kubadilika ladha na kuwa mchungu, ama mchachu. Soma Zaidi...