Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa walio na majeraha ya macho kutokana na aina mbalimbali ya jeraha
Ishara na Dalili za jeraha la jicho.
1. Kuwa na Maumivu kwenye jicho.
2. Uwekundu na uvimbe kwenye jicho.
3. Kutokuwa na uwezo wa kufungua jicho.
4.Kuwashwa kwa jicho
5. Kupungua kwa uwezo wa kuona
6.jicho kutoa machozi.
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa walio na majeraha ya macho yaliyoingiliwa na uchafu Kama vile wadudu,kijiti,n.k
1. Mwambie mgonjwa aketi chini kwenye kiti anyanyue kichwa juu aangalie mwanga.
2. Simama nyuma ya mgonjwa ili iwe rahisi kumtoa uchafu Tumia Kidole gumba , kwa upole, tenganisha kope na uchunguze kilichopo ndani ya jicho.
3. Mwambie mgonjwa aangalie kushoto, kulia, juu na chini.
4.mwagia macho maji Safi na salama.
5. Ondoa kwa kutumia pamba au kitambaa Safi ili kuondoa uchafu.
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa wenye majeraha ya macho yanayohusiana na kemikali iliyomwagika kwenye jicho.
1. Ondoa mgonjwa kutoka eneo hilo, funga chombo cha kemikali
2. Mwagilia jicho la mgonjwa kwa maji baridi ya bomba kwa angalau dakika 10.
3. Usiruhusu maji yaliyochafuliwa kumwagika kwenye jicho ambalo halijaathirika
4. Mwambie mgonjwa atunze jicho lisilojeruhiwa kwa sababu Kuna uwezekano wa kuambikiza jicho lingine.
5 inapaswa utambue Ni aina ganu ya kemikali imeingia jichoni.
6. Mpeleke mgonjwa hospitali kwa usimamizi zaidi.
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa wenye majeraha ya macho yanaliyoingiliwa na vitu vyenye ncha Kali Kama vile Pini,sindano,n.k
1. Weka kitambaa Safi juu ya jicho lililopata jeraha.
2. Mwombe mgonjwa atunze jicho lisilojeruhiwa kwa sababu harakati hii itasababisha msogeo wa jicho lililojeruhiwa ambalo linaweza kuongezea kupata Maumivu.
4. Mpeleke mgonjwa hospitali kwa usimamizi zaidi.
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa wenye majeraha ya macho yanayohusiana na gesi
1. Hakikisha ulinzi wako mwenyewe kutoka kwa gesi
2. Mtoe mgonjwa kwenye Hilo eneo na kumweka sehemu yenye hewa nzuri.
3.mwambie mgonjwa kuwa atapona
4. Mkataze mgonjwa kusugua jicho
5. Mpeleke mgonjwa hospitali kwa usimamizi zaidi
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kuyatunza macho
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya kazi ya protin na vyakula vya protini mwilini
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na shambulio la moyo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya fati na mafuta
Soma Zaidi...Hii posti inahusu zaidi sifa za mkojo usio wa kawaida,ukiona mkojo wa namna hii unapaswa kwenda hospitalini kwa matibabu au vipimo vya zaidi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali za chakula kushindwa kumengenywa kwenye tumbo,ni sababu mbalimbali hasa za kiafya kama tutakavyoona hapo mbeleni
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza jinsi ya kumfanyia huduma ya Kwanza kwa mtu aloanguka kifafa
Soma Zaidi...Unyanyasaji wa kimwili. Unyanyasaji wa watoto kimwili hutokea wakati mtoto amejeruhiwa kimwili kimakusudi. Unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa watoto kingono ni shughuli yoyote ya kingono na mtoto, kama vile kumpapasa, kushikana mdomo na sehemu
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa tatizo na kuishiwa damu, kuishiwa damu ni tatizo linolowakumba watu wengi na kusababisha matatizo mengi
Soma Zaidi...