MBINU ZA KUWAKINGA WATOTO NA SARATANI.


image


Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo tunaweza kuzitumia ili kuwakinga watoto dhidi ya saratani, kama tulivyotangulia kusema kwamba saratani ya watoto mara nyingi Usababishwa na akina Mama hasa kwa sababu ya mtindo wa maisha wakati wa ujauzito kwa hiyo tunaweza kutumia njia zifuatazo ili kuweza kuepuka na tatizo hili la saratani kwa watoto.


Mbinu za kupunguza tatizo la saratani kwa watoto.

1.Kwanza kabisa akina Mama wakati wa ujauzito wanapaswa kuhudhuria maudhurio yote ya kliniki ili kuweza kupata mafundisho mbalimbali yanayohusu namna ya kuishi wakati wa ujauzito ili kuweza kupata mtoto ambaye hana matatizo yoyote.

 

2 . Lakini cha kushangaza Mama anaanza mahudhurio ya kliniki mimba ikiwa na miezi sita au saba kusema ukweli hata kama mama anapata mafundisho aameshaharibu kama ni maisha yasiyo ya kawaida kwa mimba ameshafanya na mimba sasa ni kubwa, kwa hiyo akina Mama  mnapaswa kujali  hali  zenu na kutunza watoto wenu vizuri kwa hiyo tuwatunze watoto wetu ili waweze kuwa na afya njema na tushirikiane kuitokomeza janga la saratani kwa watoto wetu.

 

3. Akina Mama wanapaswa kuepuka kabisa matumizi ya sigara wakati wa ujauzito kwasababu moshi wa sigara unaweza kuingia kwenye plasenta na kusababisha maambukizi kwenye sehemu ya plasenta hali ambayo Usababisha kiwango cha kupelekea chakula kutoka kwenye plasenta kwenda kwa mtoto kubwa na hitilafu kubwa hatimaye mtoto uzaliwa akiwa na Dalili za saratani.

 

 4. pia moshi wa sigara usababisha kupunguza kwa vichiocheo vya progesterone na oestrogen na pia katika kufanyika kwa mtoto moshi wa sigara unaweza kusababisha sehemu nyingine kutokamilika vizuri na kusababisha mapungufu kwa mtoto ambayo Usababisha saratani kwa watoto.kwa hiyo akina Mama ni vizuri kuachana na matumizi ya sigara wakati wa ujauzito ili kuweza kumpatia mtoto nafasi ya kukua vizuri akiwa tumboni na akizaliwa awe na afya njema kama watoto wengine.

 

5. Akina mama wanapaswa kukamilisha kwa chanjo za watoto wao, tunajua kubwa chanjo kwa watoto na kwa mama akiwa na mimba ni lazima kuchomwa sindano ya Tetunus kwa ajili ya Mama na mtoto na pia mtoto akizaliwa anapaswa kutumia chanjo zote na kuzimaliza kwa wakati chanjo hizi ni kama vile, chanjo ya kifua kikuu ambayo utolewa kwenye bega la kulia , hii chanjo utolewa tu mtoto anapozaliwa, chanjo ya pili ni chanjo ya polio ambayo uzuia kupooza na utolewa baada ya kuzaliwa, wiki ya sita, wiki ya Kumi mpaka mwisho wiki ya Kumi na nne.

 

6.Chanjo nyingine ni chanjo ya kuzuia kuharisha ambayo kwa kitaalamu huitwa Rotarix ambayo utolewa kwa matone, chanjo hiyo utolewa wiki ya sita na wiki ya Kumi, pia chanjo nyingine ni chanjo inayoitwa pentavalent ambayo inatibu Magonjwa matano Nayo utolewa kwenye wiki ya sita, kumi na kumi na nne, pia chanjo nyingine ni chanjo inayotibu upumuaji na magonjwa ya Nimonia nayo utolewa kwenye wiki ya sita, wiki ya Kumi na wiki ya Kumi na nne na nyingine ni chanjo ya Surua ambayo utolewa kwenye wiki ya nane na kumi na tano, kwa hiyo mtoto akipokea chanjo zote ni mara chache kupata magonjwa ya saratani.

 

7. Kupunguza uharibifu wa hewa kwenye nyumba.

Kwa wakati mwingine mtoto anaweza kupata ugonjwa huu wa saratani kwa sababu ya kuwepo kwa uharibifu wa hewa kwenye nyumba kwa sababu nyumba nyingine unakuta kuna mionzi mikali  na mambo kama hayo ambayo yanaweza kusababisha kuwepo kwa uharibifu kwenye afya wa mtoto , kwa kawaida weka nyumba katika hali ya usafi pamoja na hewa safi.

 

8. Watoto wadogo wasikae Juani kwa mda mrefu.

Tunajua wazi kuwa mionzi ya jua huwa ni hatari kwa kusababisha saratani kwa hiyo ngozi ya watoto wadogo ,inakuwa bado ni raini na zinaweza kupitisha mwanga kwa urahisi kwa hiyo ni vizuri kutowaweka watoto wadogo kwenye  mwanga wa jua kwa sababu ni hatari unaweza kusababisha saratani kwa watoto wadogo.kwa hiyo wazazi wanapaswa kuwaambia wanafamilia wote ili wasiweze kuwapeleka watoto wadogo kwenye mwanga wa jua.

 

9. Mpeleke mtoto mwenye Dalili za saratani hospitali kwa matibabu zaidi.

Kuzama ukweli watu wameshajiwekea imani kubwa saratani hauponi hiyo si kweli kwa sababu saratani ukiwahi pake inapokuwa kwenye hatua za mwanzoni kupona ni rahisi, lakini ukisubiri kwenda hospitalini kwenye dakika za mwisho na za Maambukizi yameshakuwa mengi sana kupona ni vigumu kwa hiyo tunapaswa kuwahi hospitali ili tuweze kupata matibabu mapema.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    2 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Madhara ya kaswende kwa wajawazito na watoto wadogo.
Posti inahusu zaidi madhara ya kaswende kwa mama mjamzito na mtoto, Ni ugonjwa unaopatikana hasa kwa njia ya kujamiiana na utoka kwa mwenye Ugonjwa kwenda kwa mtu ambaye hana ugonjwa, kwa hiyo tunapaswa kujua madhara ya ugonjwa huu kwa mama mjamzito na mtoto. Soma Zaidi...

image Namna ya kufanya usafi wa sikio
Post hii inahusu zaidi namna ya kufanya usafi wa sikio, sikio ni mojawapo ya ogani ambayo usaidia kusikia,kwa hiyo sikio linapaswa kusafishwa kwa uangalifu kama tutakavyoona hapo chini. Soma Zaidi...

image Dalili za upotevu wa kusikia
posti hii inazungumzia kuhusiana na Upotevu wa kusikia unaotokea hatua kwa hatua kadri umri unavyozeeka (presbycusis) ni jambo la kawaida. T Kwa wale walio na umri wa zaidi ya miaka 75, idadi ya watu walio na  upotezaji wa kusikia inakaribia 1 kati ya 2. Soma Zaidi...

image Post hii inahusu zaidi umuhimu wa kondo la nyuma
Kondo la nyuma ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamziti,kondo la nyuma husaidia katika kazi mbalimbali katika ukuaji wa mtoto. Soma Zaidi...

image Upungufu wa vyakula vya madini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula vya madini Soma Zaidi...

image Nyanja sita za afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu nyanja sita za afya Soma Zaidi...

image Ijuwe saratani ya kibofu cha nyongo
Makala hii inakwenda kukufahamishavkuhusu saratani yavkibifu cha mkojo. Soma Zaidi...

image Mambo muhimu kwa wanawake kabla ya kubeba mimba
Posti hii inahusu zaidi mambo muhimu kwa wanawake kabla ya kubeba mimba,Ni mambo ya kuzingatia ili mama akija kubeba mimba awe mzima kimwili, ki afya na kisaikolojia na hivyo hivyo Mtoto atakayezaliwa atakuwa salama. Soma Zaidi...

image Ugonjwa wa kuharisha na sababu zake.
Kuharisha ni Hali ya kupitisha kinyesi Cha maji chenye damu au kisicho na damu Soma Zaidi...

image Kuharisha choo cha marenda renda ni dalili gani?
Hivi huwa unachunguza choo chako? ivi huwa kinazama kwenye maji ama kinaelea? Kila damu ama malendalenda, je ni cheusi sana na kina harufu kali sana. Soma Zaidi...