image

Mbinu za kuzuia na kuepukana na maradhi ya uti wa mgongo

Posti hii inahusu zaidi njia au mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepukana na tatizo la ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.

Mbinu za kuweza kupambana au kuepukana na Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kutoa elimu kwa watu ili kuweza kuwajulisha watu kuwepo kwa ugonjwa huu, namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine jinsi unavyoweza kutibiwa na mbinu au njia za kuzuia Ugonjwa huu ili usiendelee kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

 

2. Pia kama kuna Dalili za kuwepo kwa Ugonjwa huu kwenye jamii, jamii inapaswa kuepukana na mikusanyiko isiyo ya lazima ili kuepuka madhara makubwa ambayo yanaweza kutokea kama mtu mmoja ana Ugonjwa huu kwenye mkusanyiko anaweza kusambaza kwa wengine na kusababisha kuendelea kuwepo kwa Maambukizi.

 

3. Kuwaelimisha watu kuacha tabia za kugusana moja kwa moja ambazo zinaweza kusababisha kuenea kwa Ugonjwa huu kwa mfano kubusiana, na pia kwa wale wenye tatizo hili hawapaswi kutema tena mate ovyo wawe na sehemu maalum kwa ajili ya kuweka mate siyo kuyasambaza hali ambayo Usababisha kuendelea kuenea kwa ugonjwa na kuweza kuongeza namba ya waathirika wa Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.

 

4. Pia madawa ya kutibu Ugonjwa huu yanapaswa kuwepo na pia kila aina ya kipimo inapaswa kuwepo ili kuweza kutambua visababishi mbalimbali,na pia kwa upande wa watoto wadogo wanapaswa kutolewa chanjo mapema ili kuweza kuwa na kinga ya kupambana na ugonjwa huu endapo utatokea .

 

5. Kwa wale wenye imani tofauti au potofu kuhusu Ugonjwa huu ni lazima waache ili kuweza kuwapeleka wagonjwa hospitalini na kupata matibabu mapema ili kuokoa maisha kwa sababu Ugonjwa huu bila matibabu yoyote hali inaweza kuwa mbaya na hatimaye kuwapoteza wapendwa wetu.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1155


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

nahis miguu pamoja na mikono kuishiwa nguvu ni mgongo kuuma ni dalili za ugonjwa gan ?
mm nahis miguu pamoja na mikono kuishiwa nguvu ni mgongo kuuma ni dalili za ugonjwa gan ? Soma Zaidi...

Hatua za Maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
Posti hii inahusu zaidi hatua mbalimbali za Ugonjwa wa Ukimwi, kawaida Ugonjwa huu huwa na hatua kuu nne ila kila hatua huwa na sifa zake kwa hiyo tunapaswa kujua hatua za Ugonjwa huu na kujaribu kuzuia maambukizi yasisambae kabisa. Soma Zaidi...

Dalili za ugonjwa wa fungusi uken
Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa fungusi uken, ni ugonjwa unaoshambulia sana sehemu za Siri ambao huwa na dalili kama zifuatazo. Soma Zaidi...

Kuhusu HIV na UKIMWI
Somk hili linakwenda kukueleza kuhusu Mambo mbalimbali yahusuyo HIV na UKIMWI Soma Zaidi...

Maambukizi kwenye uume
Post hii inahusu zaidi maambukizi kwenye uume, maambukizi hata utokea kwenye kichwa Cha uume kwa kitaalamu huitwa Balanitis, zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa ugonjwa huu. Soma Zaidi...

Namna ya kutoa huduma kwa mgonjwa wa Dengue.
Posti hii inahusu zaidi huduma anayopaswa kupata mgonjwa wa ndengue, kwa sababu tunafahamu wazi Ugonjwa huu hauna dawa ila kuna huduma muhimu ambayo anaweza kupata na akaendelea vizuri. Soma Zaidi...

Dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanaume
Posti hii inakwenda kukuletea dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanaume Soma Zaidi...

Dalili za Ugonjwa wa Ebola.
Virusi vya Ebola ni virusi vinavyohusiana vinavyosababisha Homa za hemorrhagic magonjwa yanayoambatana na kutokwa na damu nyingi (kuvuja damu), viungo kushindwa kufanya kazi na, mara nyingi, kifo. Virusi vya Ebola na virusi huishi kwa wanyama, na wanad Soma Zaidi...

VIPI VIDONDA VYA TUMBO VINATOKEA
VIPI VIDONDA VYA TUMBO VINATOKEA 1. Soma Zaidi...

Maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...

MARADHI MAKUU HATARI MATANO (5) YANAYOENEZWA KWA KUNG'ATWA NA MBU (malaria ndio inachukua nafasi ya kwanza)
1. Soma Zaidi...

KISUKARI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...