image

Mda wa kufanya tendo la ndoa baada ya kujifungua

Posti hii inahusu zaidi mda ambao mama anapaswa kukaa bila kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua.

Mda wa kufanya tendo la ndoa baada ya kujifungua.

1. Hili ni tatizo ambalo linawapata wanawake wengi ambapo hawajui ni mda gani na wakati gani waanze kufanya tendo la ndoa baada ya kujifungua, wengine wanakaa mda mrefu wengine mfupi ila kadri ya wataalamu wanashuri kuwa Mama anaweza kuanza kufanya tendo la ndoa baada ya wiki sita au siku arobaini na mbili tangia siku aliyojifungua, tendo la ndoa linakatazwa lisifanyike kwa Mama ndani ya siku arobaini na mbili baada ya kujifungua kwa sababu zifuatazo.

 

 

2.wakati wa kujifungua mwili wa Mama unakuwa uko tofauti kwa hiyo viungo vya Mama vinapaswa kujirudisha katika hali ya kawaida kwa sababu wakati wa kubeba mimba na kukua Kuna mabadiliko mengi kwenye mwili wa Mama kwa hiyo Mama anapojifungua anapaswa kurudi kwenye hali ya kawaida kadri ya wataalamu hali ya kawaida walau ni siku arobaini na mbili, kwa sababu ya utofauti wetu wakati wa kujifungua ni vizuri kuwasikiliza wataalamu wa afya Ili kama pametokea tatizo wakati wa kujifungua siku zinaweza kuongezewa .

 

 

3. Pia Mama anapojifungua Kuna bado uchafu unakuwa unatokea taratibu, kwa hiyo ikitokea mwanamke akafanya tendo la ndoa kabla ya siku zilizopangwa kwa sababu ya uchafu unaotoka anaweza kupata maambukizi, wote wawili ambao ni baba na Mama kwa hiyo kusubiri ni muhimu.

 

 

4. Na pengine kwa sababu ya kuwepo kwa ujauzito Kuna kipindi homoni zina badirisha mwili wa Mama ambapo Mama anakuwa mkavu kabisa kwenye via vya uzazi hali inayosababisha kuchubuka wakati wa kujamiiana, kwa hiyo ni vizuri kusubiri mpaka Mama apone kabisa.

 

5. Kwa hiyo akina Mama wanapaswa kujua hilo kwa sababu wakikosea kuwakumbusha waume zao wanaweza kupata matatizo mbalimbali na wanaume wanapaswa kuwa Linda na kuwasaidia wake zao Ili siku za kujamiiana zifike.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 8746


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Uzazi wa mpango
Uzazi wa Mpango hutoa chaguo kwa familia kuwa na idadi ya watoto wanaotaka katika muda maalum, wanahisi na mbinu iliyoamuliwa. Uzazi wa mpango una faida kadhaa kwa mama wa mtoto, wanandoa na jamii Ujuzi wa mzunguko wa hedhi humwezesha mtoa huduma kumshaur Soma Zaidi...

Nataka nijue siku ya kubeba mimba mwanamke
Soma Zaidi...

Njia za uzazi wa mpango kwa watu wenye Ukimwi
Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango kwa watu waliopata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Soma Zaidi...

Madhara ya fangasi ukeni
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za Siri za mwanamke husababishwa na fangasi wanaoitwa CANDIDA ALBICANS pia maambukizi haya hujulikana kama YEAST INFECTION. Pia hupatikana katika midomo, mpira wa kupitisha chakula,kibofu Cha mkojo ,uume na uke. Soma Zaidi...

Faida za Uzazi wa mpango
Posti hii inazungumzia Faida za Uzazi wa mpango kwa watoto, mama, wanandoa, na jamii au JUMUIYA. Soma Zaidi...

Hatua za Kuzuia Maambukizi ya Uvimbe kwenye ovari na mirija ya uzazi
Posti hii inazungumzia kuhusiana na hatua za kujikinga na Maambukizi ya Uvimbe kwenye ovari na kwenye mirija ya uzazi Soma Zaidi...

Sabau za maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...

Nia za kupima ujauzito ukiwa nyumbani, Njia kuu 10 za kiasili za kupima mimba changa
Kuna njia nyingi zinatajwa zinapima mimba kama chumvi, sukari, mafuta na sabuni. Hata hivyo zipo njia zaidi ya 10 za kiasili za kupima ujauzito. Utajifunza hapa zote Soma Zaidi...

Samahani nauliza mjamzito akiwa na presha140/90 Kuna madhara?
Presha ya kupanda hypertension huweza kuzumbuwa watu kwa jinsia zote, na umri wote. Wajawazito pia wamekuwa wakisumbuliwa na presha hii mara kwa mara. Soma Zaidi...

Namna ya kumtunza mtoto aliyezaliwa
Post hii inahusu zaidi namna ya kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa, ni njia zitoleeazo na wakunga Ili kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa. Soma Zaidi...

Wanaopasawa kutumia PEP
PEP Ni dawa ambazo utumiwa na watu wanaojamiiana na watu wenye virus vya ukimwi ila wenyewe hawawezi kupata kwa sababu ya kutumia dawa hizo. Soma Zaidi...

Mabadiliko ya ngozi wakati wa ujauzito.
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye ngozi wakati wa ujauzito, ni mabadiliko yanayotokea kwenye ngozi ya Mama wakati wa ujauzito. Soma Zaidi...