image

Mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu

Ni mgawanyo upi wa elimu haukubaliki. Ni ipi elimul akhera na elimu dunia? (Edk form 1 Dhana ya elimu)

Mgawanyo wa Elimu usiokubalika katika Uislamu (usio sahihi).


 -    Katika Uislamu, HAKUNA mgawanyo wa ‘Elimu Dunia’ na ‘Elimu Akhera’.

 -  Mgawanyo huu ni potofu wenye dhana ya kikafiri kuwa kuna maisha ya Dini yanayoongozwa na Mwenyezi Mungu na maisha ya Dunia yanayoongozwa na binaadamu.

Mgawanyo huu sio sahihi kwa sababu zifuatazo:

1. Nabii Adam (a.s) aliandaliwa yeye na kizazi chake kuwa Makhalifa (viongozi) na alifundishwa majina (fani zote) ya vitu vyote.


Rejea Qur’an (2:31) na (2:38-39).

2.Amri ya kusoma aliyopewa Mtume (s.a.w) na umma wake haibagui elimu ya dini na dunia.

 

3.Muasisi wa (chanzo cha) elimu na fani zote ni Mwenyezi Mungu (s.w). Hakuna mwanaadamu aliyeasisi elimu au fani yeyote ila ni mwendelezaji tu. 


Rejea Qur’an (96:3-5).

4. Pia Qur’an inatufahamisha kuwa wanaomcha Allah (s.w) ipasavyo ni waumini wataalamu waliozama katika fani mbali mbali za kumjua Allah (s.w), sio tu fani za kidini za Fiqh, Tawhiid, n.k.


Rejea Qur’an (35:27-28)

6. Katika Qur’an Allah (s.w) anatufahamisha kuwa waumini wenye elimu ya fani mbali mbali ndio wenye daraja kubwa zaidi mbele yake.


Rejea Qur’an (58:11), (49:13).

7. Hakuna mgawanyo wa elimu unaooneshwa katika Hadith za Mtume (s.a.w) zinazoelezea fani za elimu.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1780


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Mtazamo wa Uislamu juu ya maana ya dini
Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini. Soma Zaidi...

KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Lengo la kushushwa vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maana ya muislamu.
Kwenye kipengele hichi tutajifunza ni nani muislamu. Soma Zaidi...

Maadili na malezi ya jamii
Soma Zaidi...

Lengo la kuumbwa Mwanadamu ni lipi?
Kwenye kipengele hichi tutajifunza lengo la kuumbwa mwaanadamuengo la kuumbwa ulimwengu na viumbe vilivyomo. Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida
Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya? Soma Zaidi...

Dhana ya ibada kwa mtazamo wa uislamu..
Mtazamo wa uislamu juu ya ibada (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kujiepusha na maringo na majivuno
Maringo, majivuno, majigambo, dharau ni vipengele vya kibri. Soma Zaidi...

Maana ya kumuamini mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha ya kila siku
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

maana ya dini
Soma Zaidi...

Dalili za kuwepo mwenyezi Mungu
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...