Mifumo ya benki ya kiislamu.

Hapa utajifunza njia ambazo nenk ya kiislamu hutumia ili kujiendesha

Benki za Kiislamu
Benki za Kiislamu ambazo hutoa huduma kama benki nyingine zinaendeshwa katika msingi wa biashara na sio ule wa riba. Benki za Kiislamu badala ya kukopesha kwa riba, hutumia rasilimali zake kwa zenyewe kujihusisha katika uzalishaji kwa kufuata misingi inayokubalika katika Uislamu. Miongoni mwa misingi inayokubalika kwa Muislamu au Benki ya Kiislamu kuingiza fedha zake katika miradi ya biashara au uzalishaji ni hii ifuatayo:

 

(i)Mudharabah
Mudharabah ni makubaliano kati ya watu wawili au zaidi ambapo mmoja au zaidi kati ya hao anatoa mtaji na mwingine hushiriki kwa ukamilifu katika kuendesha na kuongoza mradi wa uchumi. Faida itakayopatikana katika mradi huo itagawanywa kulingana na makubaliano yao. Hasara itakayotokana na mradi huo itakuwa ni ya mwenye kutoa mtaji. Wengine hawatoi chochote kusaidia hasara kwa sababu wameshatoa mchango wao wa hasara hiyo kwa jasho walilolitoa katika shughuli ambayo haikuzaa matunda bali hasara.

 


Benki za Kiislamu zinaingiza fedha zake katika miradi ya uchumi kwa njia hii ya Mudharabah ambapo benki hutoa mtaji kwa ajili ya miradi mbali mbali ya uchumi kwa mapatano ya kupata kiasi (asilimia) fulani cha faida itakayopatikana na kuwa tayari kulipa hasara itakayopatikan a.

 

(ii)Musharikah
Musharikah ni ushiriki kati ya watu wawili ambapo, tofauti na Mudharabah wote wawili wanachangia mtaji na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli ya kiuchumi, lakini si lazima watoe hisa sawa sawa, kwa makubaliano ya kugawana faida na hasara kulingana na kiasi cha hisa alichotoa kila mmoja wao. Kwa mtindo huu wa “Musharikah” Benki ya Kiislamu inaingia katika kuchangia mtaji, kuendesha na kusimamia mradi wa uchumi na watagawana (faida au hasara) kulingana na kiasi cha mtaji kila mmoja alichotoa.

 


(iii)Ijara-Uara wa Iktina
Huu ni utaratibu mwingine unaokubalika kisheria ambapo mtu au benki inatumia fedha zake katika kukodi vitu kama vile magari, majumba, ardhi, na kadhalika, ambavyo vikifanyiwa kazi huzalisha mali na kutoa faida. Benki za Kiislamu hujipatia faida kubwa kutokana na mtindo huu.

 


(iv)Murabah
Huu ni utaratibu unaotumiwa katika kununua bidhaa kwa wingi kwa ajili ya kuwauzia wafanya biashara ambao waliofikiana kuwa bidhaa hizo zinunuliwe kwa ajili yao. Benki kutokana na uwezo wake inapanga na wafanya biashara kuwa inunue bidhaa nyingi kutoka ndani na nje ya nchi kwa jina lake kisha iwauzie wafanyabiashara hao kwa bei itakayoipatia benki faida. Pia benki kwa mtindo huu inaweza kununua mazao ya wakulima na kuyauza kwa walaji kwa faida.

 


(v)Muqaradha
Mtindo huu wa Muqaradha humruhusu mtu au benki kununua “share” au “bonds” katika kampuni ya uzalishaji kwa mapatano ya kugawana faida au hasara kulingana na kiasi cha “share”.

 

Kwa kufuata mitindo hii katika kuingiza fedha zake katika miradi ya uchumi, Benki za Kiislamu hupata faida kubwa hata zaidi ya kipato cha riba kinachopatikana katika benki za riba. Benki za Kiislamu nazo hugawa faida inayopatikana kwa wateja wake walioweka fedha zao kwenye benki.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/26/Friday - 10:32:52 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 845


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Nafasi ya serikali katika ugawaji
Serikali ina nafasi katika kufanya mgawanyiko katika uchumi. Soma Zaidi...

Ufumbuzi wa tatizo la riba.
Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba. Soma Zaidi...

Nadharia ya uchumi wa kiislamu
Dhana ya uchumi wa kiislamu imejegwa jui ya ukati na kati. Dhana hii imetofautiana sana na dhana nyinginezo kama ubepari na ujamaa. Soma Zaidi...

Ni nini maana ya uchumi katika uislamu
Katikabuislamu dhana ya uchumi imetofautiana na dhana ya kidunia hivi leo ambapo kamari na riba ni moja ya vitu muhimu katika uchumi. Soma Zaidi...

Ni kwa nini riba imeharamishwa kwenye Uislamu
Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake. Soma Zaidi...

Tofauti ya uchumi wa kiislamu na uchumi wa kikafiri
Uchumi wa kiislamu unatofautiana sana na uchumi wa kikafiri. Hapa utajifunza tofauti hizo. Soma Zaidi...

Jukumu la serikali katika kuzuia dhuluma
Serikali ina nafasi kubwa katika kuzuia dhulma na kufanya uchumibuwe huru kuyokana na dhulma. Soma Zaidi...

Sera ya uchumi katika uislamu
Hapa utajifunza sera za kiuchumi katika uchumi wa kiislamu. Hapa utajifunza sera kuu tatu za uchumi wa kiislamu. Soma Zaidi...

Usawa na uhuru wa kuchuma mali katika uislamu
Uchumi wa uislamu umeweka taratibu mbalimbali katika kuchuma mali. Soma Zaidi...

Taratibu za kufanya kazi na kuajiri katika uislamu
Post hii itakufundisha taratibu za kuajiri, kufanya kazi na malipo. Soma Zaidi...

Taratibu za kumiliki hisa na mali ya shirika
Katika Uislamu kuwa na hisa kwenye mali inaruhusiwa. Hapa utajifunza taratibu za kumiliki hisa. Soma Zaidi...

Mifumo ya benki na kazi zake
Hapa utajifunza kazi za benki. Soma Zaidi...