image

Mikataba ya aqabah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

   -  Hii ilikuwa ni baina ya Mtume (s.a.w) na watu wanaotoka nje ya mji wa   

      Makkah hasa waliokuja kuhiji msimu wa Hija.

 

   -  Mtume (s.a.w) alikutana na kikosi cha kwanza kabisa cha watu sita (6) 

      kutoka Madinah (Yathrib) wa kabila la Khazraj, baada ya kuwafikishia 

      ujumbe wa Uislamu, walisilimu na wakaahidi kuufikisha kwao Madina.

 

  -  Mwaka uliofuata, 621 A.D, kikundi kingine cha waislamu 12 (2 Aus na 

     10 Khazraj) walikutana na Mtume (s.a.w) kwa siri eneo la ‘Jaratul 

     ‘Aqabah’ na kuweka mkataba wa kwanza wa ‘Aqaba na kukubaliana 

      yafuatatayo;

  1. Hawataabudu chochote isipokuwa Allah (s.w) pekee.
  2. Hawataiba wala hawatapokonya misafara ya biashara njiani.
  3. Hawatazini.
  4. Hawatawaua watoto wao tena.
  5. Hawatasema uongo wala hawatawasingizia wengine uovu.
  6. Hawatamuasi Mtume kwa kila atakalowaamrisha na watakuwa waaminifu kwake kwa hali yeyote iwayo.

 

                -  Mtume (s.a.w) aliwapa mwalimu wa kuwafundisha Uislamu, ‘Mus’ab bin 

                             Umair.

                -  Mwaka uliofuata, 622 A.D.walimjia Mtume (s.a.w) waislamu 75   

    (wanawake 2) wakiongozwa na mwalimu wao, ‘Mus’ab na kufunga   

    Mkataba wa pili wa ‘Aqabah sehemu ile ile kwa kukubaliana kuwa;

 

               

                -  Mtume (s.a.w) aliwachagulia viongozi 12 (9 Khazraj na 3 Aus) na watu 

                             watakaokuwa chini ya kila kiongozi, na wanaume wote walimpa Mtume 

                            (s.a.w) mkono wa bai’at kwa maana ya utii wao kwake.

 

                -  Baada ya kikundi hicho kurejea na kufika Madinah salama, ndipo Mtume 

                            (s.a.w) aliwatangazia waislamu wote wa Makkah kuhamia Madinah.

 

                -   Na takriban baada ya miezi miwili hivi, Waislamu wote wenye uwezo wa   

                            kuhama walishahamia Yathrib (Madinah) kwenda kujiimarisha zaidi.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1561


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil. Soma Zaidi...

Kuzaliwa kwa Mtume S.A.W
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.sa. w, sehemu ya 5. Hapa utajifunza kuhusu kuzaliwa kwa Mtume. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Sulaiman(a.s)
Kutokana na histoira ya Nabii Sulaiman (a. Soma Zaidi...

Historia ya Vijana wa Pangoni
Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s. Soma Zaidi...

CHANZO CHA VITA VYA VITA VYA AL-FIJAR NA ATHARI ZAKE
MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU). Soma Zaidi...

Je, Nabii Isa(a.s) ni Mtoto wa Mungu?
Mwenyezi Mungu si kiumbe. Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa dola ya kiislamu madinah
Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kuangamizwa kwa jeshi la tembo mwaka alizaliwa Mtume Muhammad s.a. w
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.sa. w sehemu ya 4. Hapa utajifunza kuhusu historia ya kuangamiza kwa jeshi la tembo. Soma Zaidi...

Maandalizi ya Hijra ya Mtume na Mafunzo tunayoyapata kutoka katika hijra hii
Maandalizi ya Hijra ya Mtume (s. Soma Zaidi...

Maswali kuhusu hali ya bara arabu zama za jahiliyyah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mkataba wa 'Aqabah na vipiengele vyake na mafunzo tunayoyapata katika mkataba wa aqaba
Mtume (s. Soma Zaidi...

Hadhi na haki za Mwanamke katika jamii za Mashariki ya Kati bara la arabu hapo zamani
Soma Zaidi...