Mimba iliyotunga nje

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mimba iliyotunga nje na madhara yake kiafya

MIMBA ILIYOTUNGIA NJE:

Mimba ya namna hii kitaalamu hufahamika kama ectopic pregnancy. Je hii ni mimba gani? Hii ni mimba ambayo yai lililorutubishwa linaendelea kukuwa nje ya mji wa mimba (uterus). mimba inaweza kukuwa sehemu yeyote kwenye tumbo ila nje ya mji wa mimba. Kwa asilimia kama 90% mimba hukuwa kwenye mirija ya falopia. Hii ni mimba hatari sana na inahitaji uangalizi wa haraka sana, kwani inaweza kuhatarisha maisha ya mama. Inakadiriwa kuwa mimba za namna hii huchukuwa kati ya asilimia 1 mpaka 2 ya miba zote.

 

Kwa nini mimba hii ni hatari?1.Mimba inatkuwa nje ya mji wa mimba hivyo haiwezekani mtoto kupona2.Inaweza kusababisha kupasuka kwa mirija ama sehemu ilipokuwa.3.Inaweza kusababisha ulemavu kwa mama endapo itachelewa kuonekana4.Kwa asilimia 30 mimba hii haina dalili hii ni hatari zaidi.5.Inaweza kusababisha uvujaji wa damu kwa kiasi ikubwa6.Inaweza kusababisha mwanamke kuhitajiwa kufanyiwa upasuaji kamma tiba.

 

Sababu za kutokea mimba hiiKama nilivyotangulia kukueleza kuwa asilimia 30 ya mimba hizi hazina dalili. Lakini kwa kiasi kikubwa mimba hizi huwa na dalili. Tafiti zinaonyesha kuwa dalili zake hutokea kabla ya wiki ya 10. Sasa hapa nitakutajia baadhi tu ya dalili za mimba hii:-1.Maumivu ya tumbo upande mmoja wa nyonga.2.Maumivu ya mabega3.Kutokwa na damu kwenye uke.4.Maumivu ya nyonga.5.Mvurugiko wa tumbo na kutapika6.Maumivu ya upande mmoja wa mwili.7.Kizunguzungu na uchovu8.Maumivu ya mabega, shingo na mkundu.

 

Sababu za kutokea kwa mimba hii.1.Kuwa na maambukizi kwenye via vya uzazi yaani PID2.Uvutaji wa sigara3.Kama una umri wa miaka 35 na kuendelea4.Kama unatumia madawa ya kuivisha mayai5.Kama ulishapata ujauzito huu hapo mwanzo upo uwezekano kuja kupata tena6.Kama ulifanyiwa upasuaji kwenye mirija ya falopia7.Kama una tatizo la endometriosis8.Baadhi ya njia za kuthibiti uzazi mfano, IUD

 

Nini tena yapasa kujuwa?1.Ujauzito uliotungia njea haurithiwi yaani kama mama aliwahikupata ujauzito huu hali hii hairithiwi.2.Kutoka kwa ujauzito sio sababu ya kupata mimba hii3.Kutoa ujauzito pia hakuna mahusianao na ujauzito huu4.Mazoezi na michezo pia hihusiani na kutokea kwa ujauzito huu.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-10-29     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1557

Post zifazofanana:-

Kama simu a computer yako inastack
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kufanya endapo simu yako au computer itastack Soma Zaidi...

Kipi kingine utafanya ukiwa Facebook
Somo hili linakwenda kukueleza Mambo mengne unayoweza kuyafanya ukiwa Facebook Soma Zaidi...

Safari ya sita ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Dengue
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dengue, ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ila unasambazwa na mbu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine mbu anayasambaza Ugonjwa huu kwa kitaalamu huitwa Aedes mosquito . Soma Zaidi...

Njia za kuongeza nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuongeza nguvu za kiume Soma Zaidi...

Fida za kula uyoga
Uyoga pia ni katika vyakula vya asili, ijapokuwa upatikanaji wake umekuwa mchache siku hizi. Shukrani ziwaendee wataalamu wa kilimo, kwa sasa tunaweza kuzipata mbegu za uyoga kutoka maabara na kulima uyoga popote pale. Wataalamu wa mimea wanaamini kuwa uy Soma Zaidi...

Kukusanywa na kuhifadhiwa kwa quran
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mambo yanayopelekea ugumba.
Post huu inahusu zaidi mambo yanayopelekea ugumba kwa wanaume, ni mambo ambayo uchangia au upelekea mwanaume kukosa uzazi. Soma Zaidi...

Kujaa gesi tumboni
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kujaa tmgesi tumbon Soma Zaidi...

Saratul-humaza
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Dalili za saratani ya ini
Posti hii inahusu zaidi dalili za saratani ya ini, ni baadhi ya Dalili ambazo zinaweza kujitokeza na kuona kwamba mtu fulani ana saratani ya ini. Soma Zaidi...

Madhara ya kutoka kwa mimba
Post hii inahusu zaidi madhara ya kutoka kwa mimba, kwa kawaida tunafahamu kwamba mimba ikitungwa na mwili mzima huwa na wajibu wa kutunza kilichotungwa kwa hiyo ikitokea mimba ikatoka usababisha madhara yafuatayo. Soma Zaidi...