Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya minyoo
MINYOO NI NINI?
Minyoo ni katika vimelea ama wadudu wanaoishi ndani ya kiumbe aliye hai. Wanaweza kuishi kwenye wanyama kama ngo’ombe, ngurue na mbuzi, pia wanaweza kuishi ndani ya binadamu. Wanajipatia mahitaji humo kama chakula, hewa na kila wanachohitaji. Wakiwa wanaishi ndani ya mwili wa kiumbe hai wanaweza kusababisha madhara makubwa sana katika afya ya mtu. Wadudu hawa kitaalamu wanatambulika kama parasitic worm.
Katika makala hii tutakwenda kujifunza, dalili, sababu, matibabu na njia za kupambana na minyoo katika mazingira yetu. Pia tutaona madhara ya kiafya yanayoletwa na kuishi na minyoo mwilini. Endelea kuwa nasi upate faida hii
Hatari ya kupata minyoo ni kubwa sana maeneo ya vijijini ama katika maeneo ambayo hali ya usafi sionzuri. Nchi zinazoendelea kama nchi za afrika ni katika maeneo ambayo yanakabil;iwa sana na minyoo kuliko nchi zilizo endelea.
Wataalamu wanatueleza kuwa kuna aina zaidi ya 300,000 (laki tatu) za minyoo. Na katika aina hizi kuna aina 300 (mia tatu) za minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu na kumuathiri kwa namna moja ama nyingine.
Minyoo wanazaliana kwa kutaga mayai, na mayai yao yanatofautiana ukubwa, kuna ambayo yanaonekana kwa macho na mengine ni madogo zaidi kwa kuonekana kwa macho. Kuna aina za minyoo hutaga mayai bila ya kuhitaji kuwepo kwa dume, kwani kuna minyoo ambayo ina jinsia zote kwa pamoja (hermaphroditc).
Minyoo huweza kutaga mayai zaidi ya mara sita kwa siku. Na idadi ya mayai yao ni kati ya mayai 3000, mpaka 700000. na mayai yao yanaweza kudumu kwa miezi mingi biala ya kufa, na yanaweza kuvumialia hali mbalimbali za joto.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi hukua kutoka kwenye tishu laini za misuli ya uterasi. Fibroids nyingi ambazo zimekuwepo wakati wa ujauzito hupungua au kutoweka baada ya ujauzito, kwani uterasi inarudi kwenye ukubwa wa kawaida.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za kifua kikuu kwa watoto,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto pindi wanapopata Maambukizi ya kifua kikuu.
Soma Zaidi...HOMA YA DENGUEHoma ya dengue ni miongoni mwa maradhi hatari ambayo husambazwa na mbu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi makundi ambayo yapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa ngiri, ni hatari kwa sababu tunajua kuwa ngiri utokea kwa sababu ya kuta au tishu zinazoshikilia viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwepo kwa uwazi na kufanya viun
Soma Zaidi...Saratani ya Mapafu ni aina ya Kansa inayoanzia kwenye mapafu. Mapafu yako ni viungo viwili vya sponji kwenye kifua chako ambavyo huchukua oksijeni unapovuta na kutoa kaboni dioksidi unapotoa nje.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa Ugonjwa huu wa ukimwi ukishasmbaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuleta madhara makubwa kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la fizi kuachana, ni tatizo ambalo uwakumba watu wengi kwa wakati mwingine unakuta fizi zimeachana kutoka sehemu moja kwa nyingine kwa hiyo tunaweza kuona sababu kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...