NI NINI CHAKULA CHA MINYOO?
NI NINI CHAKULA CHA MINYOO?
Kama tulivyokwisha kuona aina za minyoo, bila shaka umetambua kidogo kuhusu nini wanakifanya wakiwa mwilini. Hivyo basi katika sehemu hii nitakwenda kukueleza chakula cha minyoo ndani ya mwili:-
1.Wanakula chakula tunachokula, katika aina hizi za minyoo wapo minyoo wanaishi kwenye utumbo mdogo. Hii ndiyo sehemu ambayo chakula kinameng’enywa na kuupa mwili nishati na afya yaani kuupatia mwili virutubisho. Lakini minyoo hawa wakati mwingine wanakula chakula alichokula mtu hata kabla ya kumeng’enywa. Hali hii inaweza kusababishia mtu kukosa virutubisho na hatimaye kukonda ama kupoteza usito.
2.Wanakunywa damu, wapo minyoo wengine wanaishi kwenye mfumo wa damu ama ameneo mengine na kuanza kunyonya damu. Minyoo hawa ni hatari sana kwani wanaweza kusababisha ugonjwa wa anaemia. Ugonjwa huu husababishwa na upungufu wa damu.
3.Wanakula viungo vya mwili, katika minyoo hawa kwa mfano liverfluke hawa wanaishi kwenye ini ama maeneo ya nyongo. Minyoo hawa wanakula ini, na kulisababishia vidonda. Pia ini linaweza kuvimba hatimaye kuleta madhara makubwa.
4.Wanakula tishu nyingine, tofauti na hayo tuliyotaja minyoo hawa wanaweza kula tishu nyingine ndani ya mwili. Kama tulivyoona kuna baadhi ya minyoo wanakaa kwenye ngozi, viungio, ini na sehemu nyingine.
Umeionaje Makala hii.. ?
Maumivu ya kifua huja kwa aina nyingi, kuanzia kuchomwa na kisu hadi kuuma kidogo. Baadhi ya Maumivu ya kifua yanafafanuliwa kama kuponda kuungua. Katika baadhi ya matukio, maumivu husafiri juu ya shingo, hadi kwenye taya.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa kula kupindukia ni ugonjwa mbaya wa ulaji ambapo mara kwa mara unatumia kiasi kikubwa cha chakula na kuhisi huwezi kuacha kula.
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha Ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano.
Soma Zaidi...NENO LA AWALI Hapa utaweza kujifunza mambo mengi kuhusu vidonda vyatumbo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata homa ya ini,kwa sababu ya hali zao mbalimbali wanaweza kupata ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Malengelenge sehemu za siri ni maambukizi ya kawaida ya zinaa ambayo huathiri wanaume na wanawake. Makala ya malengelenge sehemu za siri ni pamoja na maumivu, kuwasha na vidonda katika sehemu yako ya uzazi. Lakini huenda usiwe na dalili au ishara za mal
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vipimo mbalimbali vinavyotumika kupima VVU
Soma Zaidi...Coma ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali Jeraha la kichwa , Kiharusi, Tumor ya ubongo, ulevi wa dawa za kulevya au pombe, au hata ugonjwa wa msingi, kama vile Kisukari au maambukizi.
Soma Zaidi...