picha

NINI MAANA YA MINYOO: vimelea wa minyoo (parasites)

MINYOO NI NINI?

NINI MAANA YA MINYOO: vimelea wa minyoo (parasites)

NINI MAANA YA MINYOO?

MINYOO NI NINI?
Minyoo ni katika vimelea ama wadudu wanaoishi ndani ya kiumbe aliye hai. Wanaweza kuishi kwenye wanyama kama ngo’ombe, ngurue na mbuzi, pia wanaweza kuishi ndani ya binadamu. Wanajipatia mahitaji humo kama chakula, hewa na kila wanachohitaji. Wakiwa wanaishi ndani ya mwili wa kiumbe hai wanaweza kusababisha madhara makubwa sana katika afya ya mtu. Wadudu hawa kitaalamu wanatambulika kama parasitic worm.

Katika makala hii tutakwenda kujifunza, dalili, sababu, matibabu na njia za kupambana na minyoo katika mazingira yetu. Pia tutaona madhara ya kiafya yanayoletwa na kuishi na minyoo mwilini. Endelea kuwa nasi upate faida hii

Hatari ya kupata minyoo ni kubwa sana maeneo ya vijijini ama katika maeneo ambayo hali ya usafi sionzuri. Nchi zinazoendelea kama nchi za afrika ni katika maeneo ambayo yanakabil;iwa sana na minyoo kuliko nchi zilizo endelea.

Wataalamu wanatueleza kuwa kuna aina zaidi ya 300,000 (laki tatu) za minyoo. Na katika aina hizi kuna aina 300 (mia tatu) za minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu na kumuathiri kwa namna moja ama nyingine.

Minyoo wanazaliana kwa kutaga mayai, na mayai yao yanatofautiana ukubwa, kuna ambayo yanaonekana kwa macho na mengine ni madogo zaidi kwa kuonekana kwa macho. Kuna aina za minyoo hutaga mayai bila ya kuhitaji kuwepo kwa dume, kwani kuna minyoo ambayo ina jinsia zote kwa pamoja (hermaphroditc).

Minyoo huweza kutaga mayai zaidi ya mara sita kwa siku. Na idadi ya mayai yao ni kati ya mayai 3000, mpaka 700000. na mayai yao yanaweza kudumu kwa miezi mingi biala ya kufa, na yanaweza kuvumialia hali mbalimbali za joto.


                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views 2603

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 ai web app     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Dalili za sukari kupungua mwilini (Hypoglycemia)

sukari kupungua mwilini (Hypoglycemia) huhusishwa kwa kawaida na matibabu ya Kisukari. Hata hivyo, hali mbalimbali, nyingi zikiwa nadra, zinaweza kusababisha sukari ya chini ya damu kwa watu wasio na Kisukari. Kama vile Homa, Hy

Soma Zaidi...
NINI CHANZO CHA UGONJWA WA MALARIA? NI YUPI MBU ANAYESAMBAZA MALARIA

Malaria husababishwa na vimelea (parasite) ambavyo husambazwa ama kubebwa na mbu aina ya anopheles.

Soma Zaidi...
Namna ya kujikinga na ugonjwa wa madonda ya koo

Post hii inahusu zaidi namna ya kuzuia ugonjwa wa madonda ya koo,ni njia ambazo usaidia katika kujikinga na ugonjwa wa madonda ya koo.

Soma Zaidi...
Ufahamu Ugonjwa wa hepatitis B

Hepatitis B Ni maambukizi ya ini ambayo yamekuwa sugu kuanzia mwezi na kuendelea.

Soma Zaidi...
Dalilili za mimba Kuharibika

Kuharibika kwa mimba ni upotevu wa hiari wa ujauzito kabla ya wiki ya 20. Takriban asilimia 10 hadi 20 ya mimba zinazojulikana huisha kwa kuharibika kwa mimba. Lakini idadi halisi labda ni kubwa zaidi kwa sababu mimba nyingi hutokea mapema sana katika u

Soma Zaidi...
Madhara ya mwili kujaa sumu

Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kupatikana ikiwa mwili unaweza kujaa sumu, kwa sababu mwili unapaswa kuwa huru Ili kuweza kufanya vizuri kazi yake ila ikiwa utajaa Sumu Kuna hatari mbalimbali zinaweza kutokea kama vile.

Soma Zaidi...