MJI WA MAKKAH NA KABILA LA KIQUREISH


image


Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)


  • Mji wa Makkah na Kabila la Kiqureish.

-    Mji wa Makkah ni mji mkongwe wa kihistoria ulioanzishwa na Nabii Ibrahiim miaka mingi iliyopita.

 

-    Nabii Ibrahim (a.s) na mwanae Nabii Ismail (a.s) ndio walioinua kuta za nyumba tukufu ya Ka’abah kwa amri ya Allah (s.w).

    Rejea Qur’an (2:127).

 

-    Ka’abah ni nyumba ya mwanzo na pekee ulimwenguni iliyowekwa kwa ya kuhiji wanaadamu wote ulimwenguni.

    Rejea Qur’an (22:27), (3:96) na (22:29).


 

-    Kutokana na jangwa na ukame wa mji huu, Allah (s.w) alijaalia chem.-chem ya maji ya zamzam kutokana dua ya Nabii Ibrahim (a.s).

    Rejea Qur’an (14:37).

 

-    Mji huu ulipata utukufu kutokana na uwepo wa nyumba tukufu ya Ka’aba ambapo kabila la Qureish ndio walikuwa walinzi wa nyumba hiyo.

    Rejea Qur’an (106:1-4).

 

-    Ni mji alikozaliwa Mtume Muhammad (s.a.w) mwaka 570 A.D katika kabila la Kiqureish mwaka wa ndovu.

    Rejea Qur’an (105:1-5).

 

-    Kabila la Kiqureish liliheshimika kuliko makabila mengine kwa huduma walizokuwa wakitoa kwa watu wanaohiji, misafara ya biashara na kule kuitumikia nyumba hiyo.

 

-    Kabila la Qureish ni miongoni mwa makabila ya waarabu yaliyojishughulisha sana na biashara mbali mbali ndani na nje ya Makkah kwa muda mrefu.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    3 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Nguzo za uislamu
Katika kipengele hiki tutajifunza nguzo za uislamu.aina tano za nguzo za uislamu,dhana ya nguzo za uislamu,lengo na umuhimu wa nguzo za uislamu Soma Zaidi...

image Walio katika hatari ya kupata magonjwa ya ngono
Posti hii inahusu zaidi watu walio kwenye liski ya kupata magonjwa ya ngono, ni watu wanaofanya mambo yanayosababisha kupata magonjwa ya ngono. Soma Zaidi...

image Swala ya jamaa.
Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa. Soma Zaidi...

image Lengo la ibada maalumu
Lengo la ibada maalumu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Sanda ya mwanaume na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Uchambuzi wa hadithi za mtume
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kutoa kati kwa kati
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Dhana ya ibada kwa mtazamo wa uislamu..
Mtazamo wa uislamu juu ya ibada (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Sababu ya uislamu kuwa ndiyo dini sahihi pekee
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Zoezi la nne mada ya fiqh.
Maswali mbalimbali kuhusu fiqh. Soma Zaidi...