Mrembo mtoto wa tajiri

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

MREMBO MTOTO WA TAJIRI

Baba yangu alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa nchini Misri. Hakujaaliwa kuwa na watoto wengi, ni mimi tu ndiye niliyekuwa mtoto wa pekee katika jumba la Tajiri. Baba yangu alifariki na kuniwachia mali zake zote. Nilikuwa naishi na bibi pamoja na watumwa wa baba waliokuwa ni wafanyakazi wangu. Pia nilikuwa naishi na mama yangu. Sikuwa na mke hivyo nilikuwa nikila nyumbani. Sikuwa na hamu na mwanamke, yaani ni kama mtu aliyerogwa. Nilikuwa nikichukia sana mwanamke, niliamini kuwa nikiwa karibu na wanawake nitaweza kufilisika. Wanawake pekee niliokuwa nikiwaheshimu na kufurahia uwepo wao ni ndugu zangu na watu wengine wa karibu na familia yangu.

 

Hali hii ilinifanya niwaze sana kuendeleza biashara kuliko kucheza na wanawake hasa wale wa mitaani. Umri wangu ulizidi kwenda na hatimaye wakati wa kuoa ulifika. Nilitamani sasa kutafuta mchumba lakini moyo ulikuwa ukinisuta maana wale nilokuwa nawachukia sasa natakiwa nitafute nitakaeishi naye milele. Chuki yangu haikuisha hivyo ikawa vigumu kwangu kumpata mchumba kutoka mabinti waliyopo mtaani. Niliamini njia pekee ni kutoka nje ya mji n kwendatafuta mke vijijini ama mji mwingine.

 

Sikumoja katika pirika zangu za utafutaji , wakati wa jioni ulinikuta pembeni ya jumba moja la kitajiri. Niliwa pembeni nimekaa napiga mahesabu yangu ghafla dirisha kubwa likafunguliwa na nikaona ukumbi mkubwa sana kwenye jumba la tajiri. Bostani zuri sana lilionekana kwenye kumbi hilo kubwa. Nilipoangalia vyema kumbi lile halikuwa lenye kufunikwa juu, mwangaza mzuri ulikuwa ukipenya kwa juu. Niliamini itakuwa wemefunika kwa turubai la mpira.

 

Mauwa mazuri yalijibanga vyema, harufu mwanana ilikuwa ukipenya puani mwangu. Mauwa yalichanua vyema na kufanya ji ukimbi lingare na kuvutia mtazamaji. Ilitulia kidogo huku nikithaminisha uzuri ulioje wa bustani lile. Wakati nikiangalia zaidi ghafla sura nzuri ikatokea nyuma ya uwa moja kubwa. Loo! Ni mwanamke mmoja mzuri sana alikuwa nakuja huku akiwa amebeba keni la kumwagilia mauwa.

 

Nikatafuta sehemu nzuri ya kukaa nipate kumuona vyema. Nilianza kuvutiwa na urefu alio nao, kwani hakuwa mfupi mno na si mrefu mmo. Nilipata kuiona vyema sura iliyo na ngozi nyeupe, pua iliyo tokeza vyema, macho makubwa kama mwanamwari wa pakistani. Nikiwa mbali kidogo nilitamani kusogea jirani ili nillihofu kumshitua, nilipata mwanya wa kujibanza sehemu nikaanza kumuona vyema. Nikaanza kutazama kwenye maeneo kadha na kugundua makubwa mabayo wengi katika wanawake wa mtaani hawakuwa nayo.

 

Kirundo cha nywele kilionekana ndani ya hijabu, kirundo kilishuka mpaka mgongoni, nilianza kuhisi mapigo ya moyo kama yanabadilika. Wakati alipokuwa akinyanyua keni na kuanza kumwagilia mauwa nilipata kuona bangili kwenye mgono wake. Zilikuwa zikimeremeta sana. Niliamini kuwa bila shaka ni babguli za dhahabu. Ziliweza kugongana na kutoa mlio mzuri. Nilianza kunogewa na uwepo wa mwanamwari. Nilibahatika kuona nyusi zilizotiwa wanja na kunyooka kama mbalamwezi ya mwezi mwandamo.

 

Akiwa anaendelea kumwagilia mauwa ghafla nyuki akamuingia kwenye hijabu yake. Akiwa katika harakati za kumtowa nyuki alimuuma na kutoa miguno ya maumivu. Sauti ile ilikuwa ni kama moto uliomwagiwa petroli kwenye moyo wangu. Binti aliendelea kumtoa nyuki, hatimaye akapunguza baadhi ya mafazi yake kwa haraka. Nilianza kukodoa mimacho nipate kuona vya ndani. Ghafla dirisha likafungwa, na nisijuwe nini kimeendelea zaidi. Kwa unyonge na upole nilirudi nymbani na kujitupa kitandani.

 

Sikuthubutu kula wala kunywa, hamu ya kula, kuzungumza na kunywa ilitoweka yote. Ghafla nilionyesha dalili za kuumwa na nikaanza kuchemshiwa dawa. Bibi yangu akaja ndani na aliponiangalia tu akagunduwa kuwa kuna jambo linaendelea. Bibi akaendelea kunidodosa ili apatekujuwa undani ndipo nikamuhadithia vyete vilivyonikuta. Bibi akanieleza “usipatetabu mjukuu wangu, mimi binti yule ninamjuwa na hata kwao ninakwenda sana, nitaongea naye kisha nitakuja kupa jibu ni lini ukutane naye”. baada ya kusikia maneno yale nilifurahi sana na hapohapo nikapona.

 

Siku mbili zikapita bila ya bibi kunieleza chochote, hatimaye nikaanza kuumwa tena. Siku ya tano bibi akaja chumbani kwangu na kuanza kunipa habari za furaha. Bibi akanieleza kuwa “Nilikwenda kumfata yule binti, na nikamueleza kuhusu ugonjwa wako baada ya kukuona. Alichonijibu kuwa hata yeye alikuona na hakutaka ufahamu, alianza kukupenda tuka alipokuona. Naye toka mlipoonana hakuamka kitandani kwa kukuwaza na asijuwe wewe ni nani na atakupata wapi. Hakuweza kuamini kama wewee ni mjukuu wangu. Hivyo ameniomba mkutane kesho kabla ya kutoka watu msikitini, maana geti lao litafunguliwa kwa ajili yako lakini ukichelewa baba yake atarudi na hutopata nafasi tena”

 

Maneno ya bibi yalikuwa kama mkuki wa furaha uliokita katikati ya moyo wangu. Kwa furaha nilimkumbatia bibi na kumbusu. Ilikuwa ni siku ya Al-hamisi, nilitamani iwe ijumaa. Siku ya ijumaa hatimaye ikifika na asubuhi baada ya kupata kifungua kinywa bibi akaja na kunieleza kuwa nishevu nywele zangu vizuri nipendeze. Nikaagiza kijana aende akaniletee kinyozi anayesifika. Basi ndipo nikaletewa kinyozi huyu mnayemona hapa. Na hapo ndipo mambo yalipoanza kuharibika.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-07     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2106


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Hatima ya kijana mchonganishi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Malipo ya wema ni wema
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa nne wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Mtoto wa Tajiri na maskini ( sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu hadithi fupi tu kuhusu mtoto wa tajiri na maskini, palikuwepo na watoto wawili mmoja akiwa mtoto wa tajiri na mwingine wa maskini. Soma Zaidi...

Hadithi ya aliyekatwa vidole gumba
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Ndoa ya Sinbad na binti mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Matibabu ya vidonda sugu
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu matibabu ya vidonda vya tumbo sugu Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya mvuvi na jini
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi yeye mwenyew
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Ndoto ya mgonjwa, binti mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...