Posti hii utokea huduma ya kwanza kwa mtu aliye na shida ya kushindwa kupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu Cha mkojo,
Huduma ya kwanza kwa mtu Mwenye tatizo la kushindwa kupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu Cha mkojo.
1. Muweke mgonjwa kwenye hali ya kutaka kukojoa.
Kwa kufanya hivyo tunaweza kusababisha mkojo kutoka au msaidie mgonjwa kumwekea kwenye kufaa Cha kukojolea kwa kufanya hivyo mkojo unaweza kupita na mgonjwa anaweza kupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu Cha mkojo na anaweza kuwa kawaida na kuendelea kukojoa.
2. Mpatie mgonjwa vitu vya moto vya kunywa kama vile chai ya moto, kahawa,na kufaa Cha kukojolea kiwe Cha moto.
Kwa kufanya hivyo tunaweza kusababisha mkojo kutoka kwenye kibofu Cha mkojo na mgonjwa anaweza kukojoa na kurudia kwenye hali ya kawaida, kwa sababu maji ya moto au vitu vya moto vinaweza kushutua mishipa ambayo inakuwa imebana na kumfanya mgonjwa akawa kawaida.
3. Mpeleke Mgonjwa kwenye bomba la maji na fungua maji kwa speed kubwa na mkojo unaweza kutoka.
Kwa kufungua maji ya bomba kwa speed kubwa mno usababisha kuamsha sehemu za kibofu Cha mkojo na kusababisha mgonjwa aweze kupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu kitendo hiki ufanyiwa hasa kwa watu wale waliofanyiwa upasuaji na huwa wanaweza kukojoa kwa kawaida.
4. Mpatie mgonjwa dawa ya maumivu.
Mgonjwa anayeshindwa kupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu Cha mkojo anapaswa kupewa dawa za maumivu kama vile parnadol, Asprini, tramadol na dawa nyingine ambazo zote za maumivu kwa sabat labda kitendo Cha kushindwa kupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu Cha mkojo ni kwa sababu ya maumivu kwa pale alipofanyiwa upasuaji kwa kumpatia dawa ya maumivu subiri kwa mda na uangalie kama anaweza kupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu Cha mkojo na kuendelea na maisha yake ya kawaida.
5. Kama mgonjwa amepewa kila njia na mkojo ukashindwa kutoka kwenye kibofu Cha mkojo, mgonjwa anaweza kuwekewa milija wa kupitisha mkojo ambao kwa kitaamu huitwa catheter hiki ni kifaa ambacho upitishwa mkojo Moja kwa Moja kutoka kwenye kibofu Cha mkojo na kuingia kwenye sehemu ambayo imeandaliwa na kisha kumwaga. Kwa hiyo njia hii utumika ikiwa zote zimeshindikana.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi dalili za jeraha kali kwenye ubongo, ni majeraha ambayo utokea kwenye ubongo pale ambapo mtu anapata ajali au amepigwa na kitu chochote kigumu kichwni, zifuatazo ni dalili za jeraha kali kwenye ubongo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza vitu vinavyosababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili na Sababu za Homa ya manjano ya watoto wachanga ni kubadilika rangi kwa manjano katika ngozi na macho ya mtoto mchanga. Homa ya manjano ya mtoto hutokea kwa sababu damu ya mtoto ina ziada ya rangi ya
Soma Zaidi...Hapa tutaangalia baadhi ya sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate na namna ya kutibu tatizo la kujaa kwa mate mdomoni
Soma Zaidi...Kutokuona siku zake mwanamke ni ishara kuwa kuna shida kwenye umfumo wa uzazi. Wakati mwingine kutokuona siku ni ishara ya baraka ya kupata mtoto. Ijapokuwa kuna wengine wanadiriki kutoa mimba kwa sababu zisizo za msingi. Je unadhani UTI inaweza kusababi
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano. Kifua kikuu ni ugonjwa sugu wa kuambukiza na anuwai ya magonjwa ya kliniki yanayosababishwa na Mycobacterium tuberculosis complex.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu kiungulia kwa wanawake wajawazito na tiba yake, ni ugonjwa au hali inayowapata wajawazito walio wengi kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito.
Soma Zaidi...Kwa nini unapata maumivu makali wakati wa kuingia hedhi, je unajuwa sababu za maumivu makali ya tumbo la chago.
Soma Zaidi...