image

Msimamo wa uislamu juu ya utumwa

Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)

     5.2. Msimamo wa Uislamu juu ya Utumwa.
Hali ya Utumwa kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w).
-  Biashara ya utumwa ilidumu na kuenea sana enzi za ujahili takribani nchi na 
mabara mbali mbali hasa nchi za Magharibi, Uarabuni, Bara la Asia na      kwingineko Duniani. 

-  Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na  
    ubinaadamu wao.

-  Watumwa walimilikiwa kwa kuuzwa na kununuliwa kama bidhaa za biashara
    au kwa matumizi mengineyo pia.

-  Watumwa walikuwa wakitumika kama sehemu ya starehe na kiburudisho kwa
   wakubwa zao.

-  Mateso, unyama na ukatili ilikuwa desturi ya kufanyiwa watumwa na mabwana
    zao katika kutimiza matashi yao.

-  Watumwa walikuwa hawana uhuru wa kufanya na kufuata mila, desturi au dini 
    waitakayo na waipendayo wao wenyewe bila ruhusa ya wakubwa wao.

- Watumwa walikuwa wakitumikishwa kama wanyama au hata zaidi ya wanyama 
    kwa kufanyishwa kazi ngumu zilizozidi uwezo wao.

-  Kila jaribio la ubaya lilifanywa kupitia watumwa, mfano makali ya kisu, mkuki, 
    mshale, n.k yalijaribiwa kwa watumwa.

-  Watumwa ndio ilikuwa nyenzo pekee ya kufanyia kazi, kubebea na kusafirishia
    mizigo mikubwa kwa masafa ya mbali.

-  Hadhi na nafasi kati ya mabwa na watumwa ilikuwa na utofauti mkubwa mno, 
   kiasi kwamba bwana anaweza kumdhalilisha mtumwa kwa namna apendavyo. 

-  Huduma na misaada ya kiutu kwa watumwa ilikuwa hafifu mno, kiasi kwamba
   mtumwa akiugua au kukosa uwezo wa kuzalisha mali alikuwa hana faida tena
   kwa bwana.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1456


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Masharti ya swala
Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali. Soma Zaidi...

Maana ya shahada
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maandalizi ya maiti: kumuosha, kumkafini ama kumvalisha sanda na kumzika
Soma Zaidi...

Umuhimu na nafasi za hijjah katika uislamu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mifumo ya benki na kazi zake
Hapa utajifunza kazi za benki. Soma Zaidi...

Zifahamu njia za kutwaharisha, aina za maji, udongo na Namna ya kujitwaharisha
Soma Zaidi...

IBADA YA HIJA NA NAMNA YA KUITEKELEZA
Soma Zaidi...

Funga za kafara, aina zake na sababu za funga hizi za kafara na hukumu zake
Soma Zaidi...

mambo yanayofungua swaumu
post hii ijakwenda kukufundisha mambo yanayoharibu funga Soma Zaidi...

Kumuandaa maiti punde baada ya kufariki dunia
Soma Zaidi...

Ni zipi funga za suna, na faida na fadhila zake pamoja na wakati wake wa kufunga
Soma Zaidi...

SWALA
1. Soma Zaidi...