MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA MAANA YA DINI


image


Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini.


Maana ya Dini kwa mtazamo wa Uislamu

Kwa mtazamo wa Uislamu “Dini” ni utaratibu wa maisha wanaoufuata binaadamu katika kuendesha maisha yao ya kila siku ya kibinafsi na kijamii. Ni katika maana hii ya dini Allah (s.w) huuliza katika aya ifuatayo:

 

“Je, (watu) wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu na hali kila kilichomo mbinguni na ardhini kimejisalimisha kwake kipende kisipende. Na kwake wata rejeshwa wote.” (3:83).


Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa:Kwanza, kuna dini nyingi zinazofuatwa na watu hapa ulimwenguni, lakini dini iliyostahiki watu wenye “akili timamu” waichague, ni ile dini inayofuatwa na maumbile yote.


Pili, dini ya maumbile yote ya mbinguni na ardhini si nyingine, ila ni ile ya kujisalimisha katika kufuata sheria za maumbile alizoziweka Muumba.

 

Tukirejea kwenye sayansi ya maumbile (natural science) tunajifunza kuwa kila kitu kilicho hai na kisicho hai (living and nonliving thing) ili kiwepo ni lazima kifungamane na sheria za maumbile za kibailojia, kifizikia na za kikemia (Biological, Physical and Chemical laws). Kwa mtazamo huu hata miili yetu pia imejisalisha kwa muumba kwa kufuata sheria za maumbile pasina hiari kama inavyosisitizwa katika aya ifuatayo:

 


“Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawa saw a ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu (yaani dini hii ya Kiislamu inawafikiana bara bara na umbile la binaadamu).Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu.

 

Hiyo ndio dini iliyo ya haki lakini w atu wengi hawajui.” (30:30)
Kwa ufupi, aya hii inatukumbusha kuwa miili yetu imejisalimisha kwa Allah (s.w) bila ya hiari kwa kufuata bara bara sheria za maumbile zinazofungamana na ufanyaji kazi wa kila kiungo cha mwili.Chakula kinayeyushwa tumboni, moyo unasukuma damu, mapafu, ini, figo, na viungo vingine mwilini hufanyakazi kwa kufuata sheria za Muumba na wala sio kwa kufuata sheria walizozitunga wanaadamu katika mabunge yao.

 


Tatu, Uislamu ni mfumo wa maisha uliofungamana na kanuni na sheria alizoziweka Muumba ili watu waendeshe maisha yao ya kibinafsi na kijamii sambamba na hali halisi ya maumbile yaliyowazunguka.

 

Wale watakaoamua kwa hiari yao kufuata kanuni na sheria alizoziweka Allah (s.w) katika kukiendea kila kipengele cha maisha yao ya kila siku watakuwa ni Waislamu, waliojisalimisha kwa Muumba wao kama ilivyojisalimisha miili yao na maumbile yote ya mbinguni na ardhini.

 

Hawa wataishi kwa furaha na amani hapa ulimwenguni, kwani wataepukana na maisha yale ya kupingana na maumbile yaliyowazunguka. Ama wale watakaokataa kufuata kanuni na sheria alizoziweka Muumba na badala yake wakaweka mfumo wa maisha unaopingana na kanuni na sheria hizo watakuwa ni makafiri, walioamua kupingana na maumbile yote yaliyowazunguka. Kwa vyovyote vile watakuwa wameamua kuishi maisha ya upinzani na vurugu.

 

Nne, kimantiki, ni lazima iwepo siku ya Hisabu ambapo watu wote watahudhurishwa mbele ya mahakama ya Muumba na Mmiliki wa maumbile yote, ili walipwe kutokana na uamuzi wao katika kuchagua na kufuata “dini”. Wale waliojisalimisha kwa Allah (s.w) na kufuata “dini” yake, pamoja na kuishi maisha ya nuru (ya Amani na Heshima) hapa duniani, watakuwa na maisha ya furaha na amani ya kudumu huko Peponi. Ama wale waliompinga Allah (s.w) kwa kuweka na kufuata mifumo ya maisha kinyume na “dini” yake, pamoja na kuishi maisha ya giza (ya khofu na huzuni) hapa duniani, watakuwa na maisha ya dhiki na adhabu kubwa huko Motoni kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:

 

“Mwenyezi Mungu ni Mlinzi (kiongozi) wa wale walioamini. Huwatoa katika giza na kuwaingiza katika nuru.Lakini w aliokufuru, w alinzi (viongozi) w ao ni Matwaghuut.Huwatoa katika nuru na kuwaingiza katika giza.Hao ndio watu wa Motoni, humo wakakaa milele”. (2:257)



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Umbile la mbingu na ardhi linavyothibitisha uwepo wa Allah
Allah anatutaka kuchunguza umbile na mbingu na ardhi ili kupata mazingatio. Soma Zaidi...

image Mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na maumbile yake
Kuwa ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na umbile la mwanadamu. Soma Zaidi...

image Nafasi ya akili katika kumtambua Allah
Kwa kutumia akili yako unaweza kumtambua Allah bila ya shaka yeyote ile. Postbhii itakufundisha nafasi ya akilonkatika kutambuwa uwepo na Uwezo wa Allah. Soma Zaidi...

image Mtazamo wa kikafiri juu ya maana ya dini.
Maana ya dini kwa mujibu wa makafiri ina utofauti mkubwa na vile ambavyo uislamu unaamini kuhusu dini. Soma Zaidi...

image Nguzo za Imani kwa mujibu wa mafunzo ya kiislami.
Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu nguzo sita za imani katika Uislamu. Soma Zaidi...

image Ni ipi maana ya Imani katika Uislamu, na ni zipi sifa za muumini.
Katika Uislamu imani inanguzo kuu 6.Pia muumini anatakiwa ajipambe na sifa za waumini. Posti hii itakufundisha kuhusu imani katika Uislamu. Soma Zaidi...

image Kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila dini?
Mwanadamu hawezi kuishi bila dini, kwani dini imekusanya mfumo mzima wa maisha yake. Soma Zaidi...

image Ni Ipi Elimu yenye manufaa
Elimu inaweza kugawanyika katika makundibmrngine mawili ambayo ni elimu yenye manufaa na elimubisiyi na manufaa Soma Zaidi...

image Kwa namna gani Allah huwasiliana na wanadamu kwa kupitia ndoto.
Ndoto za kweli ni moja kati ya njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu. Soma Zaidi...

image Jifunze ni kwa namna gani Malaika waliweza kuwasiliana ana manabii Malimbali
Wakatibmeingibe Allah anapotaka kuwasiliana na wanadamu hutuma Malaika wake. Soma Zaidi...