Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya nne)

Post hii inahusu zaidi watoto Hawa wawili wakiwa kwenye kituo cha mapumziko ambapo mtoto wa tajiri anabugia soda aliyopewa na yule mwalimu pia tumbo linaanza tena na anaanza kuendesha

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini .

1. Basi baada ya wale watoto wawili kukutana na mwalimu wa Ile shule, Hawa watoto hawakujua kwamba ni mwalimu Bali ni msamaria mwema tu, basi watoto Hawa walinunuliwa soda , mtoto wa maskini kwa sababu alikuwa na kiasi na wazazi wake walimwambia kwamba asitumie vitu vya kula njiani  kwa mara nyingi alitunza Ile soda ila mtoto wa tajiri kwa sababu ya kula kula kila mara alibugia Ile soda na kwa sababu tumbo lilikuwa halijakaa vizuri alianza kuendesha tena.

 

2. Basi yule mtoto badala ya kukimbilia chooni alijichafua kwenye nguo zake na akasubilia kusafishwa kama kawaida yake , Bali yule mwalimu alimwambia mwanangu hauko nyumbani na pia wazazi wako hawapo hapa jikaze ujisafishe kwa sababu yule mtoto wa maskini aliona jinsi wale makonda walivyomsafisha na yeye akachukua maji akammwagia maji na mwalimu akamwambia ajisafishe na yeye akajisafisha na kwa sababu ilikuwa usiku kidogo baridi lilikuwa ni kama lote  mwalimu akamwonea huruma akaamua kumuomba number ya wazazi wake na kuwapigia.

 

3. Basi baada ya kusikia sauti ya wazazi wake alilia kwa sauti kubwa na kuanza kusema kwa nini mmenitesa kwa nini hamkunifundisha maisha na mbona watoto wenzangu hawana shida hapa mimi mtaniua kama maisha ni hivi hamjanitendea haki mwenzangu aliambiwa kila kitu hata hajaaibika hata kidogo na wazazi wakalaumiana wao kwa wao, basi mtoto akasema sitapanda tena gari la jumla nataka gari la binafsi , kwa sababu baba Ela zilikuwepo aliongea na yule mwalimu Ili wakodi gari la binafsi na yule mtoto wa maskini pamoja na yule mwalimu walikodiwa gari na wakasafiri mpaka shuleni, yule mtoto wa tajiri alifurahi sana na yule mtoto wa maskini alikuwa akishangaa kila kitu.

 

4. Basi baada ya kufika pale shuleni mwalimu akajitambulisha wazi kwamba yeye ni mkuu wa shule pale yule mtoto wa tajiri aliumia sana kwa sababu alikuwa hataki kuhaibika na akikumbuka alichokifanya shuleni, kwa hiyo wanafunzi wakapelekwa bwenini, wakaweka vitu vyao mwalimu alishangaa kuona mtoto wa maskini akiwa na ki mzima kidogo na mtoto wa tajiri ana kila kitu na begi kubwa na ka thamani kubwa kwa hito mwalimu akaona tofauti kati ya wake watoto kati ya vitu walivyonavyo na kati ya tabia zao. 

 

5. Basi wakapelekwa mezani kupata chakula wakakuta ni ugali wa Dona maharage na pia maji ya kunywa , yule mtoto wa maskini akamshukuru Mungu kwa kuona chakula cha aina Ile na mtoto wa tajiri aliangua kilio kuona chakula kile kwa sababu alikuwa hajawahi kuona na watu wote wakaamka na wafanyakazi wakashangaa yule mtoto.

ItaendeleaJe! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/16/Friday - 07:13:36 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 771


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu Soma Zaidi...

Kisiwa cha uokozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Muendelezo wa hadithi ya mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Safari ya majibu juu ya maswali mawili
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya kijana Frank na Amisa pia na wapenzi wawili ambao ni James na Amina. Soma Zaidi...

Chemsha bongo na bongoclass
Jipime uwezo wako wa kufikiri pamoja nasi. Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Kwanini vidole gumba vilikatwa
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa y Soma Zaidi...

Hadithi ya Khalid mwenye kuneemeshwa na Jalid
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Deni la mapenzi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...