Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)

Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya.

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wanapanda gari kwenda shuleni kuanza kidato cha kwanza.

1. Kama tulivyoona kwenye sehemu ya kwanza kwamba watoto Hawa wawili walipanga gari kuelekea shuleni kuanza kidato cha kwanza, wote walipandishwa kwenye basi na kukarishwa kwenye kiti kimoja kwa sababu Ile gari walikuwa wanakaa watu wawili wawili  kwa hiyo kila mtu alipandishwa na ka kifurushi kake, kwa upande wa mtoto wa tajiri gari lile ulikuwa ni usumbufu kwake kwa sababu alizoea kupanda magari ya binafsi na kwa upande wa mtoto wa maskini ilikuwa ni mara ya kwanza kupanda basi kwa hiyo kila mtu alikuwa na maono tofauti kuhusu safari Ile.

 

2. Kwa hiyo safari ilikuwa ndefu kama siku Moja na nusu, walipofikisha masaa mawili ya safari mtoto wa tajiri akaanza kula vyakula vyake ovyo ovyo bila mpangilio lakina yule waskini alikuwa hali chochote alipoulizwa wewe kwa nini ufungui kula chakula chako akamjibu akaseme baba na mama wameniambia kwamba Nile taratibu kwa sababu magari makubwa huwa hayasimami ovyo kusudi tukojoe au kwenda haha kubwa , Bali mtoto wa tajiri alijibu kwamba huo ni ushamba nikitaka kwenda kukojoa watanifungulia kwa sababu mimi ni mtoto wa tajiri, Bali mtoto wa maskini akajibu hapa tuko safarini hakuna cha mtoto wa tajiri au wa maskini wote tuko sawa.

 

3. Bali watu walishangaa majibu ya yule mtoto wa tajiri kwa kiburi chake kwa hiyo akaendelea kubugia chakula mara chips, bagga, maziwa na vitu vingine kama hivyo, ila yule mtoto wa maskini alikuwa hajafungua muhogho wake na maji, basi wakafika sehemu ambayo Kuna pori kubwa wanyama kama wote,Simba,fisi ,chui, twigs, tembo walikuwa ni wa kigusa kwenye mazingira hayo na watu wote walipofika mazingira yale walikaa kimya ila mtoto wa tajiri akaanza kuumwa tumbo, akaanza kupiga kelele nataka kujisaidia kwa sababu alikuwa na hali ngumu anaharisha kwenye suruali, anajitapikia akaanza kutukana dereva kwamba wewe unazidiwa na dereva wangu angekuwa yeye angenishusha tu, watu wote wakashangaa yule mtoto wa tajiri, akapiga kelele kama zote na hakuna aliyesimamisha gari na akaendelea kujitapikia na kuharisha na akapewa tu huduma ya kwanza kwenye gari ila alikuwa anatoa matusi kila mara.

 

4. Basi walipofika sehemu nzuri na salama ikabidi kumshusha yule mtoto kwa sababu gari lote lilikuwa Lina harufu mbaya, wahudumu wa gari wakasafisha gari, wakamwambia ajisafishe akakataa akasema nataka dada aje anisafishe kwa sababu yule dogo alizoea hata kusafishwa na kufuliwa kila kitu, basi abiria walishuka na kuchimba dawa pale na wakaanza kula vyakula vyao ila yule dogo wa kitajiri alikuwa amesimama akisubilia kusafishwa,mda wa kuondoka ulifika yule mtoto wa maskini akamwambia mwenzake chukua maji unawe huyu akaanza kulia kwamba hawezi na makondakta wasivyopenda shida wakachukua maji wakamumwagia wakachukua nguo zingine wakampa akavaa na zile nguo chafua akavua akaacha pale akavaaa mpya na safari ikaendelea.

 

5. Basi safari ilipoendelea yule mtoto wa maskini alikuwa akiangalia mazingira kwa sehemu mbalimbali walizopita akiangalia milima na mabonde tambarale na pia akiangalia mbuga za wanyama ila mtoto wa tajiri aliendelea kupiga usingizi kwa sababu ndoo ya maji aliyomwagiwa ilikuwa  ya baridi mno na maji yalikuwa ya kwenye madimbwi, basi mtoto wa tajiri aliamka usingizi na mwenzake akamwambia unaona milima na mabonde ambavyo mwalimu alikuwa anatufundisha darasani huyu akajibu kwamba yeye huwa anaangalia kwenye move kwa hiyo Hana shida ya kusumbua kichwa chake.

 

6. Basi safari ilikuwa kama inaelekea kwenye nusu ya safari yule mtoto aliona kwamba amekelwa kukaa kwa mda mrefu akaanza kulia baba na mama mko wapi mbona mmenitesa na nimekaa humu mda mrefu na mwenzangu naona Hana shida yoyote kwa nini hamkunizoeza maisha magumu kusudi niweze kustahimili mapema walau siku Moja mngenipandisha kwenye magari ya watu wengi ningezoea, na vyakula mmenifungia vibaya na tumbo linauma na ninaharisha kwa nini na mimi mngenifungia chakula kama cha mwenzangu Wala nisinge aibika na mngenifundisha kunawa walau nisingekuwa kituko kwenye gari kwa maana kila mtu ananiangalia mimi na Kuna wanafunzi wanaoenda kusoma shule nitakuwa aibu kwao, mtoto aliongea maneno mengi mpaka watu wakaumia na wakaamua kumbembeleza na akatulia.

 

7. Basi kwenye gari lile palikuwemo na mwalimu wa shule wanapoenda wale Vijana ni mwalimu mzuri kwa malezi ya wanafunzi, alirekodi kila kitu alichosema yule mtoto na akakumbuka kwamba kila mwanafunzi akija shule ni lazima kuandika namba za wazazi akaamua kuweka Ile rekodi vizuri na gari lilipofika kwenye kituo cha mapumziko akaamua kuwafuata wale Vijana wawili kwa sababu yule mtoto wa maskini alikuwa anaendelea kula mhogo uliochomwa na maji na yule mtoto wa tajiri alikuwa yuko hoi anaogopa hata kunywa maj. Basi yule mwalimu akawasalimia na kuongea nao akawanunulia soda , kwa mtoto wa maskini ilikuwa kama ni ndoto kuona soda ikabidi haiweke Ili aje anywe baadae, na yule wa tajiri akaanza kubugia na tumbo kwa kuwa lilitingishwa likaanza tena. Mwalimu akamuuliza mtoto wa maskini kwa nini hujanywa akasema wazazi wangu wameniambia nisinywe ovyo ovyo njiani.

 

8. Basi kwa kuwa mwalimu yule alikuwa anafahamu mazingira yale alijaribu kumsaidia mtoto wa tajiri na kusema hauko nyumbani kwa sasa ndipo unaanza maisha kajisafishe na nikupe simu uongee na wazazi wako, basi mtoto akajisafisha na namba za simu za wazazi wake alizifahamu vizuri, basi akaweka number kwenye Simu ya yule mwalimu na bahati nzuri baba yake alipokea mtoto kusikia sauti ya baba yake aliangua kilio kikubwa,

Itaendelea



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/16/Friday - 05:18:02 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 906


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Safari ya sita ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad Soma Zaidi...

Mtoto wa Tajiri na maskini ( sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu hadithi fupi tu kuhusu mtoto wa tajiri na maskini, palikuwepo na watoto wawili mmoja akiwa mtoto wa tajiri na mwingine wa maskini. Soma Zaidi...

Safari ya nne ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Kifo cha mtoa burudani wa sultani
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu hadithi ya kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

Jaribio la tatu la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Dawa mbadala za vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa mbadala za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Siri ya wageni wale inafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Muendelezo wa hadithi ya mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Ujio wa wageni wa baraka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Jaribio la kwanza la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Dalili za fangasi ukeni
Post hii inakwenda kukujulisha dalili za kuwa huwenda una fangasi sehemu zako za siri. Soma Zaidi...