Mtume Muhammad s.a. w amelewa na Baba yake mdogo

Historia na sura ya Mtume Muhammad, sehemu ya 10.

KULELEWA NA BABA YAKE MDOGO
Baada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake. Kiongozi ambaye alikabidhiwa mamlaka ya kukichimba upya kisima cha zamzam baada ya kufukiwa na watu kutoka kabila la Jurhum pindi walipoondoka Makkah.

 

Alisimama Abu Talib kumlea mtoto wa ndugu yake. Kwani huyu ndiye aliyekuwa mtoto mkybwa wa Abdul al-Muttalib.



Abu Talib alimpenda sana kijana wake zaidi ya anavyowapenda watoto wake. Mtume (s.a.w) alikuwa ni mwenyekuridhika kwa kile ambacho alikuwa akikipata.

 

Allah alimuongezea rizk mzee Abu Talib. Mzee huyu alimlea kijana wake Mpaka alipofika umri wa miaka arobaini. Watu walimpenda kijana Muhammad jinsi alivyokuwa na tabia njema na uaminifu.



Watu wa Makkah walikuwa wakiomba mvua kupitia utukufu wake. Imesimuliwa kutoka kwa Ibn ‘Asakir kuwa Jalhamah bin Arfuta kuwa amesema nilifika Makkah wakati ambao kulikuwa hakuna mvua, Maquraish wakatoka kumueleza mzee Abu Talib kuwa awaombee mvua.

 

Basi akatoka akiwa na kijana chake na akamsimamisha pembeni ya ukuta wa al-kabah kisha akaomba dua. Kwa hakika kulikuwa hakuna mawingu lakini ghafla mawingu yakajikusanya kutoka huku na kule na hatimaye mvua ikanyesha



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/11/29/Monday - 01:40:28 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1558


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Sababu za kushuka surat al humazah
Sura hii inaonya vikali tabia ya kusengenya na kusambaza habari za uongo. Wameonywa vikali wenye tabia ya kujisifu kwa mali, kukusanya mali bila ya kuitolea zaka. Soma Zaidi...

JINSI YA KUOMBA DUA ILI IKUBALIWE NA ALLAH
Kukubaliwa kwa dua kunategemea mahusiano yako na Allah. hata hivyo kuna baadhi ya mabo ukiyafanya dua yako inaweza kukubaliwa kwa haraka zaidi. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kuomba dua ikubaliwe. Soma Zaidi...

Makundi ya dini za wanaadamu
Kwenye kipengele hichi tutajifunza makundi ya dini za watu. Na makundi hayo ni matatu. Soma Zaidi...

Kumuamini mwenyezi Mungu..
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Swala ya Istikhara na jinsi ya kuiswali
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya Istikhara Soma Zaidi...

Faida za funga
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kusimamisha swala.
Kwenye kipengele hiki tutajifunza maana ya swala ni nin?. Na masharti ya swala. Soma Zaidi...

Kujiepusha na ria na masimbulizi
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Waislamu wanaolazimika kufunga
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maana ya shahada
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mtume (s.a.w) alivyoandaa ummah wa kiislamu makkah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji, ni mbinu mbalimbali ambazo utumika ili kujaribu kuepuka Dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji. Soma Zaidi...