Mtume Muhammad s.a.w analelewa na Babu yako ikiwa na umri wa miaka 6
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 9.
KULELEWA NA BABU YAKE:
Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Mzee huyu alimpenda sana mjukuu wake kuliko ambavyo alivyokuwa anawapenda watoto wake.
Alikuwa katu hamuachi mjukuu wake akiwa peke yake. Mzee Abdul Al-Muttalib alikuwa akiwekewa godoro kwenye kivuli cha Al-kabah na watoto wake wanakaa pembeni ya godoro kwa heshima ya baba yao, basi alikuwa Mtume (s.a.w) anakaa kwenye godoro lile. Baba zake wadogo wanapomtoa mzee Abdul al-Muttalib alikuwa akiwakataza na kuwaambia kuwa kijana huyu atakujakuwa na nafasi nzuri.
Mzee Abdul al-Muttalib alikuwa sikuzote akipendezwa na vitendo vya mjukuu wake. Mzee huyu aliendelea kumlea yatima huyu mpaka alipofikia umri wa miaka nane, na hapa ndipo mzee huyu alipofariki dunia na kuongeza majonzi zaidi kwa kijana huyu.
Mzee Abdul al-Muttalib alifariki wakati Mtume (s.a.w) alipokuwa na umri wa miaka nane na miezi miwili na siku kumi (10).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Bara arabu enzi za jahiliyyah, jiografia ya bara arabu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hatua na Mambo (Taasisi za Kisiasa) za msingi alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah
Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah.
Soma Zaidi...