Muda wa kuchaji simu yako

Posti hii itakwenda kukujuza juu ya kuda mzuri wa kuchaji simu yako

MUDA WA KUCHAJI SIMU YAKO

Wwatu wengi wamekuwa wakijiuliza ni muda gani hasa inapasa kuchaji simu, je nisubiri mpaka chaji iishe kabisa, ama nichaji ikiwa na asilimia ngap?. maswali kama haya na yanayofanana nitakwenda kuyajibu katika makala hii.

 

Kikawaida betri inaweza kudumu kuwa hai kati ya miaka 5 mpaka 10. lakini uwezo wa betri hupungua kadri siku sinavyoendelea. Unaweza kudhibiti hali hii kwa kuwa makini na baadhi ya mambo kadhaa. Miongoni mwa mabo hayo ni kuwa makini na muda wa kuchaji.

 

Wataalamu wa teknolojia wanatueleza kuwa muda mzuri wa kuichaji betri ni pale itakapobakiwa na asilimia kati ya asilimia 50% na 90%. na hakikisha kuwa huichaji mpaka ifikapo 100%. ni vyema kama unataka ifike 100 basi angalau ufanye hivyo mara chache.

 

Sio vyema sana kuilaza kwenye chaja japo jambo hili halina madhara kwa simu za kisasa kwani zenyewe zina kifaa cha kuifanya isimame kuchaji pindi ikifapo asilimia 100% ya chaji.

 

Hakikisha betri yako haivi chini ya asilimia 40% na mbaya zaidi isifike asilimia 2% ama 0%. na kama unahitaji kuihifadhi betri yako basi ichaji angalau asilimia 40% kisha uihifadhi.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-09     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1081


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-