Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mwanamke mwenye HIV akiwa mjamzito ama anaenyonyesha
MWANAMKE MWENYE VIRUSI VYA UKIMWI AKIWA MJAMZITO AMA ANAVYOVYESHA.
Watu wengi wamekuwa kijiuliza sana kuhusu hatma ya ujauzito kwa mwenye virusi vya ukimwi. Je ni kiasi gani mtoto aliye tumboni atakuwa salama?. ni tahadhari gani mjamzito mwenye virisi vya ukimwi achukuwe. Na atakapojifunguwa ni muda gani ataendelea kunyonyesha? Katika kipengele hiki tutaangalia kwa ufupi habari hii kama ifuatavyo:-
1.Je inawezekana kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kupata HIV/UKIMWI?Yes inawezekana, na hili ni swali watu wengi wamekuwa wakijiuliza. Itambulike kuwa kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika si lazima kuwa nawe utaathirika, ila kauli hii isieleweke vibaya. Kwani njia ambayo inaongoza leo katika kueneza maambukizi ya HIV ni kushiriki tendo la ndio. Mtu anaweza kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kuathirika endapo:-
A.Endapo hakutatokea michubuko wakati wa tendoB.Endapo muathirika ametumia dawa za ART kwa muda mrefu kwa kufuata masharti hata viral load yake ikawa haionekani (undetected) na akadumu kwa hali hii walau miezi 6C.Endapo walitumia kinga wakati wa kushiriki tendo.
2.Je HIV ma UKIMWI hupelekea mimba kutoka?Inategemea, ila kwa ufupi HIV na UKIMWI huhatarisha ujauzito endapo muathirika hatakuwa mwangalifu ama hatafata maelekezo vyema. Wajawazito walioathirika inashauriwa wafike kituo cha afya mapema sananili kupatiwa maelekezo jinsi ya kulea mimba yake kwa usalama bila ya kuathiri afya ya ujauzito wake. Hata hivyo wanatakiwa wafuate maelekezo vyema.
3.Je maisha ya mtoto yapo hatarini endapo mama mjamzito ana HIV na UKIMWI?Ni kweli kama mama mjamzito hatakuwa makini, anaweza kuweka maisha ya mtoto wake hatarini. Na si maisha ya mtoto tu bali hata maisha yake pia.
4.Je mtoto anapataje HIV na UKIMWI kutoka kwa mama?A.Wakati wa kujifunguwa kama kuna kosa litafanyika.B.Wakati wa kumnyonyosha kuanzia miezi sita toka kuzaliwa mtotoC.Wakati wa kumlea kama mama hatakuwa makni
5.Kwa nyakati za sasa wajawazito wote wanatakiwa kuzalia kwenye kituo cha afya maalumu. Hii ni kwa ajili ya kupunguza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Hatahivyo wakunga wa jadi pia wamepatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya dharura. Ila inalazimika kwa mwenye HIV afanye juu chini azalie hospitali kwa usalama zaidi wa mtoto wake.
6.Je kunyonyesha mtoto kunawza kumuambukiza HIV?Yes inawezekana, hata hivyo mama akiwa makini na maelezo aliyopewa, katu hatoweza kumuambukiza mwanaye. Inashauiwa mtoto kunyonya kwa muda wa miezi 6 tu ama chini ya hapo. Ni kuwa endapo mtoto atakuwa na michubukomdomoni ama tumboni.
7.Mama asimchanganyie mtoto ziwa lake, maziwa ya kopo na chakula. Kama ataamuwakumnyonyesha ndani iwe ni ndani ya miezi 6 tu na asimpe chakula chochote. Na kama ameamuwa kumpa chakula asimnyonyeshe tena. Na kama ameamuwa kumpa maziwa ya makopo ampe hayo tu na asimnyonyeshe. Anaweza kuchanganya chakula na maziwa ya kopo ama ya ng’ombe na si yake na kitu chingine chochote. Mama awe makini sana na jambo hili, asimchanganyie mtoto maziwa yeke na kitu kingine chochote. Hali hii inaweza kusababisha michubuko mdomoni ama tumboni na kusababisha kupata maambukizi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mimba iliyotunga nje na madhara yake kiafya
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia ugumba, ni njia ambazo utumiwa na wapenzi ambao wameshindwa kupata watoto hasa kwa wale ambao wamezaliwa wakiwa na uwezo wa kupata watoto lakini kwa sababu tofauti tofauti wanashindwa kupata watoto kwa hiyo njia zifu
Soma Zaidi...Mapacha walioungana ni watoto wawili wanaozaliwa wakiwa wameunganishwa kimwili. Mapacha walioungana hukua wakati kiinitete cha mapema kinapojitenga na kuunda watu wawili. Ingawa fetusi mbili zitakua kutoka kwa kiinitete hiki, zitabaki zimeunganishwa mar
Soma Zaidi...Ukiwa mjamzito unaweza kushuhudia kutokwa na damu. Je damu hii ni ya hedhi?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi upungufu wa homoni hii ya cortisol,hii ni homoni ambayo utokana na tezi glang(adrenal gland) kufanya kazi kupitiliza hali ambayo mara nyingi husababishwa na msongo wa mawazo wa mda mrefu, yaani wale watu ambao mda mwingi huwa wenye
Soma Zaidi...Kutoka na majimaji ka uchache kwa mwanamke sio jambo lakishangaa sana. Damu hii inawezapiabkikbatana damu na maumivu makali.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi uchafu unaotoka ukeni na rangi zake, kwa kawaida ukeni utolewa uchafu, uchafu huo unaweza kuwa kawaida na unaweza kuwa na rangi mbalimbali kutokana na kuwepo kwa Maambukizi.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukuletea mambo kadhaa yanayohusiana na malezi bora ya mama mjamzito na mtoto mchanga
Soma Zaidi...