Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, tunajua kuwa mama yake na binti alimtorisha yule binti mbali kabisa ila kijana naye aliamua kutoroka na kumfuata binti mfalme na hatimaye akampata alipo.

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme.

1. Kama tulivyoishia kwenye sehemu ya kutoroshwa kwa bibi na binti, hali hii ilimuumiza sana mtoto wa kiume wa mfalme, lakini alipoulizwa hakuweza kusema chochote , ila siku Moja mama yake aliandaa chakula kizuri alichokuwa anakipenda yule mtoto wa kiume wa mfalme akawaita na marafiki zake akampatia zawadi nzuri,akawakusanya mabinti wazuri wakawa kwenye Ile tafrija lengo la Mama ni kutaka kumfanya yule kijana asahau yule Binti Ila hayo yote yalikuwa bure, katika sherehe hiyo watu vijana wote waliamka kucheza na wale mabinti wazuri ila mtoto wa kiume wa mfalme hakucheza na Binti yoyote yule.

 

2.ilifika wakati mpaka mabinti wanamsogelea yule kijana aliwaangalia kwa dharau tu, ndipo ilipofika jioni mtoto wa kiume wa mfalme akaandaliwa chumba kizuri kama heshima ya watoto wa mfalme ndani ya chumba aliwekwa msichana mlembo yule kijana alipoingia na kumkuta alitoka chumbani akamfungia yule msichana ndani yeye akatoka nje na kwenda kulala kwa walinzi wa mfalme, mama yake alipoamka asubuhi na mapema kuangalia kwenye chumba kilichoandaliwa alishangaa kuona msichana Yuko mwenyewe kitandani amelala fofofo, mama aliumia sana na akamfungulia msichana akamruhusa aende kwa wenzake..

 

3. Baada ya mtoto wa mfalme kuwa kwenye mawazo mazito aliamuru kumshirikisha rafiki Yake maangaiko aliyo nayo moyoni ila hakumwambia kwamba yule Binti anayemtesa ni ndugu yake Bali alimwambia kuwa amehama na ajui kaenda wapi, basi yule kijana akamwambia wewe ni mtoto pekee wa kiume wa mfalme kwa nini usimwambie mfalme tatizo lako akakupatia watu wakakusaidia kumtafuta huyo Binti? Yule kijana akakubali shingo upanda alipenda Siri hii isijulikane kwa mfalme na aliogopa sana kumwumiza mama yake kwa hiyo hali ikaendelea kuwa mbaya zaidi na maisha yakaendelea kuwa magumu kwa yule kijana kwa sababu hakutaka kumwaibisha mama yake na hakupenda kuoa msichana mwingine tofauti na yule Binti.

 

4. Kadri siku zilivyoenda ndipo na Mama akaingia katika wasi wasi mkubwa na akaamuru kumwita kijana wake na kuongea naye kuhusu Sheria za ufalme ni kwamba mtoto wa kiume wa mfalme anapaswa kuoa Binti ambaye Hana undugu naye na wewe ukipenda kuoa huyu ndugu yako hautaweza kupata ufalme kwa sababu ya kufanya kitendo cha namna hiyo kwa sababu mimi nilikutambulisha kwa mfalme bila kumtambulisha dada Yako lengo ni kwamba wewe urithi ufalme wa baba Yako ila wewe bado unagangania kuoa ndugu yako, yule kijana wa kiume wa mfalme akasema Mama kama yule angekuwa ni ndugu yangu angekuwa anatambulika a kwenye familia na ukoo pia ila kwa kuwa hawamtambui mimi siwezi kukusikiliza kwa hilo kwa hiyo mama tangia mda huu mimi naenda kumtafuta yule binti popote alipo na nitamuoa na sitasikiliza chochote kutoka kwako.

 

5. Baada ya mama kuona msimamo wa kijana ni mkali mno aliwaandaa watu ili kwenda kumuua yule binti na bibi, lakini kijana akapata taarifa ndipo akaenda kwa baba yake akamuomba jeshi akiwa na lengo la kwenda kumwokoa yule binti, alimwambia baba naomba niende kusherehekea na marafiki zangu ila naomba kwenda na jeshi kusudi wanilinde, kwa kuwa baba alikuwa anampenda sana kijana wake akamuandalia chakula, nyama na vitu vyote vinavyofaa kwa sherehe akampatia na jeshi pia akiamuru jeshi limlinde na kumsikiliza kwa kila kitu atakachowaambia baada ya kufika mbele kidogo akawaambia juwa wafuatane na hao wauaji waliotumwa na Mama yake kwa sababu wanajua binti alipo.

 

6. Yule kijana akamwambia mkuu wa jeshi kwamba kabla hatujaenda kwenye sherehe tunapaswa kumwokoa mchumba wangu kutokana na wauaji na tupambane nao mpaka tumwokoe , basi mkuu wa majeshi anawapanga watu wake na wakaanza mashambulizi mpaka wakamwokoa yule binti na bibi, baada ya hapo bibi alipopata taarifa za kutaka kuuawa kwa sababu ya yule binti alisikitika sana na akaamuru kuvujisha siri hiyo kwa wake wengine wa mfalme, basi mtoto wa kiume wa mfalme akamchukua yule binti akaenda kusherehekea naye na baadae akaja naye kwa mfalme akamtambulisha kama mke wake mfalme akafurahi kwa kuona kijana wake kapata mke ila mama alikoswa amani.

 

7. Basi ikafika siku ya maandalizi ya kumsimika kijana kurithi ufalme wa baba yake kwa sababu alikuwa ni mzee, kufuatia na sheria ya kwamba mtu anayerithi ufalme ni lazima mke wake wasiwe na undugu hata kidogo na kumbuka habari imo mikononi mwa wake wenza, je unafikili watanyamaza? 

 

itaendelea

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/11/Monday - 10:41:44 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 816

Post zifazofanana:-

Dalili za ngozi kuwasha.
Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa kuhusiana na dalili za ngozi kuwashwa. Soma Zaidi...

Je unaijuwa ugonjwa wa bawasiri
Katika post hii nitakwenda kukujuza kuhusu ugonjwa wa bawasiri Soma Zaidi...

Sababu za mimba kutoka
Post hii inahusu zaidi sababu za mimba kutoka, hili ni tatizo ambalo linawakumba wanawake wengi ambapo mimba utoka kabla ya kumfikisha mda wake, kwa kawaida Ili kawaida mimba nyingi utoka zikiwa na miezi chini ya Saba au wengine wanaweza kusema kwamba mim Soma Zaidi...

Virusi vinavyopelekea Kuharisha Sana na Kutapika Sana(norovirus)
Maambukizi ya Norovirus yanaweza kusababisha kutapika sana na'Kuhara. Virusi huambukiza sana na kwa kawaida huenea kupitia chakula au maji ambayo yamechafuliwa na kinyesi wakati wa kutayarisha. Unaweza pia kuambukizwa kwa kuwasiliana kwa karibu na mtu Soma Zaidi...

Sababu za kuvimba na maumivu kwenye korodani moja au zote mbili
Post yetu ya Leo inaenda kutufundisha kuhusiana na uvimbe wa korodani moja au ambayo kitaalamu huitwa EPIDIDYMITIS. EPIDIDYMITIS ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa kiume wa uzazi. Epididymis ni mrija (tube) uliyoko nyuma ya korodani ambayo mbegu za kiume Soma Zaidi...

je ute wa uzazi uanza kuonekana siku ya 14 tu au kabla ? Na je mimba ya siku tatu inaweza kucheza?
Miongoni mwa dalili zamwanzo za ujauzito ni maumivu ya tumbo ama kupatwa na damu kidogo. Mabadiliko ya ute ute sehemu za siri ni katika baadhi ya dalili. Endelea na makala hii utajifunza zaidi. Soma Zaidi...

Huduma kwa watu waliodhani wamepatwa na maambukizi.
Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo utolewa kwa watu wanaodhani wamepatwa na maambukizi ya virus vya ukimwi. Soma Zaidi...

Kichwa kinaniuma mbele sielewi nini
Zijuwe sababu za kuumwa nankichwa upande mmoja wa kichwa. Soma Zaidi...

Nini sababu ya kuchubuka midomo na kuwa myeupe
Kama una tatizo la midomo kuchubuka na kuwa myeupe ama kuwa na vidonda. Post hii inakwenda kuangalia swala hili. Soma Zaidi...

Faida za minyoo
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za minyoo Soma Zaidi...

Faida za kula parachichi
Somo Hili linakwenda kukuletea faida za kula parachichi Soma Zaidi...

Dalili za mimba changa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba changa Soma Zaidi...