MWENDELEZO WA HADITHI YA BINTI MFALME


image


Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, baada ya kijana wa kiume wa binti mfalme kuoa yule ndugu yake baba anafanya sherehe kubwa na wake wenza wamepata habari kwamba kijana wa kiume wa mfalme ameoa ndugu yake wakaamuru kunyamaza ili waje watoe siri siku ya kuapishwa kwa mfalme.


Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme (sehemu ya tatu).

1. Kama tulivyomalizia kwenye sehemu ya pili pale mama wa kijana wa kiume wa mfalme alitaka kumuua binti na bibi ili kupoteza ushahidi ila kijana huyo wa mfalme aliwahi akawaokoa na kumwona kipenzi cha moyo wake na kumchukua nyumbani kama mke wake ila mama hakukubaliana naye ila mfalme kwa kuwa alikuwa anampenda kijana wake akisikiliza kila kitu alichotaka na akaamua kufanya sherehe kubwa na ya kifahari.

 

2 . Na yule bibi kwa kuwa alipenda sana umaarufu na maisha mazuri alijisalimisha kwa wake wenza na akatoa siri zote za yule mke mdogo wa mfalme, wale wake wenza walifurahi sana kusikia habari hiyo na wakapata sehemu ya kumwaibisha adui yao kwa sababu yule mke mdogo wa mfalme alikuwa ni kama kizuizi kwao na mfalme, basi wakapanga njama na kutunza siri ili siku ya kumwapisha mfalme siri itobolewe na kujana wa kiume wa mfalme hasiweze kupata ufalme.

 

3. Katika wakati ule palikuwepo na sheria moja kwamba ili mtu aje kuwa mfalme ni lazima awe ameoa kwenye ukoo ambao hawana undugu hata kidogo ili kuepuka hali ya ufalme kugawanyika kwa hiyo walitaka ufalme ubaki ndani, au kama  kwenye familia ya kifalme hakuna mtoto wa kiume wa kurithi ufalme au yupo ila hana sifa za kuwa mfalme mtoto wa kike anaweza kuwa malkia ila mme wake atoke sehemu tofauti na ile sehemu na hasiweze na undugu wowote na familia ya kifalme iwe kati ya ndugu wa wake wenza yaani pasiwepo na undugu hata chembe.

 

4. Katika maandalizi yote hayo mama wa kijana wa kiume wa mfalme aliona kwamba mwanae hawezi kupata ufalme kwa sababu aliona bibi yupo pale akiwa na ushahidi wote na yuko kati ya maadui zake akapata shida sana akawaza mpaka akakonda , kwa kuwa bibi alikuwa mnafiki na mpenda sifa aliamua kumwita yule mke wa mfalme kwa siri akamwambia kuwa kwamba kwa sasa mwanao hawezi kupata ufalme sasa cha kufanya ni kuhakikisha kuwa tunafanya mbinu ili kijana aweze kuachana na yule binti .

 

5. Kwa kuwa yule Mke wa mfalme alikuwa kwenye hali ngumu akamuuliza bibi tufanye je? Bibi akasema nitakwambia cha kufanya baada ya siku chache, kisha bibi akaenda kwa yule mke wa kwanza wa mfalme akasema andaa binti yako ili yule kijana wa kiume wa mfalme hasipopata ufalme huyu atakuwa malkia. Baadae siku mbili zinafika bibi akaenda kuonana na mke mdogo wa mfalme kwa ajili ya maongezi.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    3 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya html kwa kiswahili    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Hadithi iliyosimuliwa na tabibu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi. Soma Zaidi...

image UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA
Posti hii inakwenda kukisimulia kuhusu hadithi za alifu lela ulela KITABU CHA KWANZA Soma Zaidi...

image Hadithi ya Kaka wa tatu wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Siku ya sita ya wageni
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Hadithi ya kinyozi yeye mwenyew
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image The fastest (anakwenda mbio zaidi)
Posti hii inakwenda kukuletea sifa za mnyama anayekwenda mbio zaidi Soma Zaidi...

image Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image WAKATI WA KUFUMBUKA
Post hii ni mwendelezo wa hadithi inayohusu Kufumbuka ambapo , John anaonekana kama sio mtoto wa Mzee maganga kwa sababu na miungu imekili kwa sababu chakula chote kimeliwa na kuisha. Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mtihani unafika ila Jackie hakujiandaa alishutuliwa na marafiki zake baada ya kuona mwenendo wake haueleweki. Soma Zaidi...