Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme (sehemu ya nne)
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya nne ni pale bibi anawachanganya kwa maneno yake yaani mke wa kwanza anaambiwa aandae malkia na mke mdogo atafute njia za kufanya kijana wake kuwa mfalme.
Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya nne.
1. Basi siku ya maongezi ikafika kati ya bibi na mke wa mdogo wa mfalme,bibi akamsalimia vizuri akampa sifa zote ila akamwambia kwamba wafanye utaratibu wa kumshauri kijana wa kiume wa mfalme awe na mke wa pili ili aweze kupata ufalme wa nane kwanza na mke huyu ambaye ni ndugu yake na kadri ya sheria hataweza kupata ufalme.
2. Basi bibi na yule mke mdogo wa mfalme wakamwita yule kijana na kumpasha habari ya kila kitu kinachoendelea ila kijana akasema siwezi kumwacha mke wangu ili niwe mfalme bora nikakosa ufalme ila nikaishi na mpenzi wangu, mama yake baada ya kusikia hivyo akahisi kuchanganyikiwa na siku zinaenda kijana hana mda mpaka mama yake akajuta na kusema bora ningewazaa watoto wangu wakiwa wawili.
3. Basi bibi akamwambia Mama usihofu kila kitu kitakuwa sawa nihaidi utanipa nini ,Mama akamwambia nitakutunza mpaka utakapofariki, akasema iwapo yeye atafariki ataacha ujumbe wa bibi kutunzwa maisha yake yote, bibi akasema tuandikiane wakaandikiana bibi akaanza mbinu za kuhakikisha kuwa ufalme unabaki mikononi mwa uzao wa mke mdogo.
4. Baada ya bibi kutoka kwa yule mke mdogo akaenda kwa yule mke mkubwa ambaye alimwambia aandae binti mkubwa kwa ajili ya kupata umalkia, basi bibi akaenda kwa ndugu wa mfalme akamshawishi kijana wa ndugu wa mfalme akamwambia , mfalme ana mpango wa kugawa mali kwa watoto wake ila mali kubwa zitaenda kwa binti wa kwanza na kwa mme wake akamwambia kijana kwa nini usimtongoze yule binti na ukampa mapenzi ya kweli ili upate zawadi nyingi na kuishi na binti wa mfalme.
5. Kijana akafanya hivyo na akafanikiwa kumpa binti yule mimba na binti akaogopa kuishi kwa mfalme akiwa na mimba kwa sababu siku zile wasichana waliobobea mimba kwa waliuawa na yule kijana akamwoa mtoto wa mfalme . Kwa hiyo sifa za kuwa malkia zikaishia hapo . Bibi baada ya kufanikiwa mbinu hiyo akaenda kwa mke mdogo na kutoa taarifa mke mdogo alifurahi sana ila akaendelea kumwacha bibi akae kwa wake wenza ili kuleta habari zaidi, basi bibi akapanga kukutana na mke mdogo kwa maongezi zaidi,
itaendelea baadae
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Simulizi za Hadithi Audio π2 Dua za Mitume na Manabii π3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π4 web hosting π5 Kitau cha Fiqh π6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
NIMLAUM NANI? (Sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi iliyopita ambapo Frank aliwakuta Amina ambaye ni mpenzi wake ameumbatiana na James ambaye ni rafiki yake ,kwa hiyo tuendelee kusikia yaliyotokea baada ya Amina na James kukutwa na Franki.
Soma Zaidi...Hadithi katika kijiji cha burugo
Β Posti hii inahusu zaidi jinsi ya watu walivyoishi katika kijiji cha burugo .tunajuwa hadithi ni sehemu mojawapo ya kubirudisha na kujifunza kitu flani kutoka kwenye jamii .
Soma Zaidi...NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku
Soma Zaidi...Hasara za wivu na kutokuwa wazi ( sehemu ya 2)
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu na kutokuwa wazi sehemu ya pili, sehemu hii inahusu mama Lisa anaenda kwa mama lina ili kuuliza kinachoendelea kwa mtoto wake , kwa hiyo tuona atapata jibu gani.
Soma Zaidi...Ni nani kama mama
Nani kama mama? Hadithi hii itakufunza umuhimu wa kuwa muwazi kuhusu familia yako.
Soma Zaidi...Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi watoto Hawa wawili wakiwa kwenye kituo cha mapumziko ambapo mtoto wa tajiri anabugia soda aliyopewa na yule mwalimu pia tumbo linaanza tena na anaanza kuendesha
Soma Zaidi...