MWENDELEZO WA HADITHI YA BINTI MFALME SEHEMU YA SITA


image


Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya.


Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sita.

1. Baada ya bibi kutoka kumpasha habari mke mdogo wa mfalme kwa kila kitu kinachoendelea alirudi kwa mke mkubwa  wa mfalme na kumwambia kwamba binti yako ameharibu kwa kuolewa na yule kijana ila ni lazima tufanye mbinu ila upate mfalme kwenye ukoo wako  kwa sababu nitaongea na mke mdogo wa mfalme aende kumtembelea kijana wake ilai siku akienda nenda ulale na mfalme utapata mimba ya mtoto wa kiume,kwa sababu bibi ashafanya mazindiko yake ili mama apate mtoto wa kiume.

 

2. Basi ilifika wakati yule mtoto wa  Mzee na kijana wa kiume wakapata watoto wa kiume wawili mapacha, kwa hiyo yule mke mdogo akaenda kuwasalimia wajukuu wa kiume ili aje ampashe mfalme habari, yule Mke mdogo wa mfalme alipoondoka yule mke mkubwa akaenda kwa mfalme akalala na mfalme akabeba mimba ya mtoto wa kiume, baada ya mke mdogo wa mfalme kurudi bibi akamwambia kwamba mke mkubwa wa mfalme amebeba mimba na dalili ni mtoto wa kiume.

 

3. Basi yule mke mdogo akapanic sana akamuuliza bibi mjanja tufanyeje? Bibi akamwambia tumpeleke yule mke wa kwanza wa kijana wa mfalme mbali na mme wake amsindikize na pia tumwambie mfalme kuwa anapaswa kusimika mrithi wa ufalme, kwa hiyo wakapanga na mtoto wa kiume wa mfalme wakamwahidia mali nyingi kwa sababu ya kupenda mali akakubali kurudi nyumbani kutoka machimboni ila mke yule alimwacha, akamwambia mfalme kwamba niko tayari kurithi ufalme wako, mfalme akafurahi sana ila akampa mashariti kwamba hapendi sherehe anaomba akabidhiwe kadri ya sheria na watu wachache sherehe itakuwa baadae mfalme akakubali.

 

4. Basi kesho yake yule mtoto wa kiume wa mfalme akamwambia mke wake yule pacha wake waende kutembea kwenye ufalme mwingine yule binti akafurahi sana wakaenda walipofika akamwacha huko akampitia mke mwingine yule mwenye mapacha akamleta kwa baba yake mfalme, baba yake akafurahi sana akaandaa sherehe akampatia mtoto wake ufalme na bibi akaitwa kukaa ikulu na baada ya siku chache yule mama mkubwa akajifungua mtoto wa kiume . hadithi yangu imeishia hapo.

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    2 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    5 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    6 Madrasa kiganjani    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Kisa Cha mfugaji na mkewe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Safari ya nne ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Safari ya majibu juu ya maswali mawili
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image The fastest (anakwenda mbio zaidi)
Posti hii inakwenda kukuletea sifa za mnyama anayekwenda mbio zaidi Soma Zaidi...

image Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Nani muuaji?
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu muuaji wa mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

image Mafundisho kutokana na hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mafundisho ambayo tunayapata kutoka kwa binti mfalme, tunapotoa hadithi sio kusoma na kufurahia tu ila kuna mafundisho muhimu katika maisha yetu. Soma Zaidi...

image Familia mpya baada ya harusi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Hadithi ya jini na mfanya biashara
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...