image

Nafasi ya akili katika kumtambua Allah

Kwa kutumia akili yako unaweza kumtambua Allah bila ya shaka yeyote ile. Postbhii itakufundisha nafasi ya akilonkatika kutambuwa uwepo na Uwezo wa Allah.

KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU

Nafasi ya akili katika kumtambua Allah (s.w)
 
Imani ya kweli juu ya Allah (s.w) itathibitika moyoni baada ya kumjua vyema Allah (s.w) na sifa zake zote tukufu. Allah (s.w) hatumuoni kwa macho bali tunamfahamu kwa akili zetu katika kuchunguza dalili mbali mbali zilizotuzunguka.
 
Tunavyojifunza katika Qur-an, matumizi ya kwanza ya akili tulizotunukiwa ni kuyakinisha kuwepo kwa Allah (s.w) na sifa zake. Msisitizo wa matumizi ya akili na fikra zetu katika kazi hii ya kumjua Allah (s.w) na sifa zake tukufu unabainishwa katika aya zifuatazo:“Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana ziko hoja (za kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu - Allah) kwa wenye akili”. (3:190).
 
“Na katika ishara zake, (za kuthibitisha kuwepo kwake na uweza wake) ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kutoka kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofa hamu” (30:21)
 
“Na katika ishara zake (za kuonyesha uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu na (mengine yenu na hali ya kuwa muumbaji ndiye huyo huyo mmoja). Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi”. (30:22).
 
“Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na (kuamka) mchana, na kutafuta kwenu fadhila yake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaosikia.” (30:23)
 
“Na katika ishara zake ni kukuonyesheni umeme kwa (kukutieni) hofu na tamaa (ya kuja mvua), na kuyateremsha (hayo) maji kutoka mawinguni. Kwayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofahamu” (30:24)
Aya hizi chache zatosha kuonesha msisitizo wa Qur-an juu ya kutumia akili na fikara zetu katika kumfahamu vyema Allah (s.w). Kila mtu atakavyozama katika utafiti wa mazingira katika fani yoyote ile ndivyo atakavyoweza kumuona Allah (s.w) na utukufu wake kwa upeo mkubwa zaidi. Allah (s.w) mwenyewe anathibitisha hilo katika aya zifuatazo:
 
“Je! Huoni kwamba Mw enyezi Mungu Ameteremsha maji mawinguni! Na kw ayo Tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana.(35:27)
 
Na katika watu na wanyama wanaotambaa na wanyama (wengine), pia rangi zao ni mbali mbali, kwa hakika wanaomcha Allah miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanazuoni): Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Msamehevu.” (35:28)
Wataalamu (wanazuoni) kwa mnasaba wa aya hizi si wale waliobobea kwenye fani ya fiq-h tu na nyinginezo zinazoitwa za “dini” bali ni pamoja na wale walio zama kwenye fani mbali mbali za elimu ya mazingira. Kwa mujibu wa aya hizi, wataalamu waliopigiwa mfano ni wale waliobobea katika taaluma ya hali ya hewa (meteorologists), katika taaluma ya madini (Geologists), katika taaluma ya matunda (horticulturist), katika taaluma ya wanyama (Zoologist) na katika taaluma ya watu na tabia zao (anthropologists). Wale ambao hawatumii vipawa vyao vya akili katika kumfahamu Mola wao kutokana na mazingira wamefananishwa na wanyama, kama tunavyojifunza katika Qur-an:
 
“Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam wengi katika majini na watu (kwa sababu hii) Nyoyo (akili) wanazo, lakini hawafahamu kwazo, macho wanayo lakini hawaoni kwayo na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika. (7:1 79)
 
“Hakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni hawa wanaojipa uziwi na ububu ambao hawayatii akilini (wanayoambiwa au wanayoyaona)” (8:22).
 
Vilevile Alla(s.w) anawashutumu wale wanaobishana kuhusu Yeye pasina kuwa na elimu.
 
Je! Huoni ya kw amba Mw enyezi Mungu amekutiishieni vilivyomo mbinguni na ardhini, na Akakukamilishieni neema zake zilizo dhahiri na za siri? Na wako watu wanaobishana katika (mambo) ya Mwenyezi Mungu pasipo elimu wala uwongofu wala Kitabu chenye nu ru (31:20)
 
Na katika w atu w ako w anaojadiliana juu ya Mw enyezi Mungu bila ya ilimu wala uwongozi wala kitabu chenye nuru (22:8).
Kutokana na aya hizi tunabainikiwa kwa uwazi kuwa katika Uislamu suala la kumuamini Allah (s.w) si suala la kibubusa (la kufuata mkumbo tu) bali ni suala la kitaaluma linalohitaji utafiti wa kina wa kisayansi. Kuna maeneo matano makubwa ambayo tukiyazamia vizuri kisayansi, yanatupatia dalili mbali mbali za uwazi zinazotuthibitishia kuwepo kwa Allah (s.w) na utukufu wake usio na mfano wake. Maeneo haya ni:
Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake
Nafsi ya mwanaadamu
Historia ya mwanaadamu
Maisha ya Mitume
Mafundisho ya Mitume
 
“Na katika ishara zake (za kuonyesha uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu na (mengine yenu na hali ya kuwa muumbaji ndiye huyo huyo mmoja). Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi”. (30:22).
 
“Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na (kuamka) mchana, na kutafuta kwenu fadhila yake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaosikia.” (30:23)
 
“Na katika ishara zake ni kukuonyesheni umeme kwa (kukutieni) hofu na tamaa (ya kuja mvua), na kuyateremsha (hayo) maji kutoka mawinguni. Kwayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofahamu” (30:24)
 
Aya hizi chache zatosha kuonesha msisitizo wa Qur-an juu ya kutumia akili na fikara zetu katika kumfahamu vyema Allah (s.w). Kila mtu atakavyozama katika utafiti wa mazingira katika fani yoyote ile ndivyo atakavyoweza kumuona Allah (s.w) na utukufu wake kwa upeo mkubwa zaidi. Allah (s.w) mwenyewe anathibitisha hilo katika aya zifuatazo:
 
“Je! Huoni kwamba Mw enyezi Mungu Ameteremsha maji mawinguni! Na kw ayo Tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana.
(35:27)
 
Na katika watu na wanyama wanaotambaa na wanyama (wengine), pia rangi zao ni mbali mbali, kwa hakika wanaomcha Allah miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanazuoni): Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Msamehevu.” (35:28)
 
Wataalamu (wanazuoni) kwa mnasaba wa aya hizi si wale waliobobea kwenye fani ya fiq-h tu na nyinginezo zinazoitwa za “dini” bali ni pamoja na wale walio zama kwenye fani mbali mbali za elimu ya mazingira. Kwa mujibu wa aya hizi, wataalamu waliopigiwa mfano ni wale waliobobea katika taaluma ya hali ya hewa (meteorologists), katika taaluma ya madini (Geologists), katika taaluma ya matunda (horticulturist), katika taaluma ya wanyama (Zoologist) na katika taaluma ya watu na tabia zao (anthropologists). Wale ambao hawatumii vipawa vyao vya akili katika kumfahamu Mola wao kutokana na mazingira wamefananishwa na wanyama, kama tunavyojifunza katika Qur-an:
 
“Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam wengi katika majini na watu (kwa sababu hii) Nyoyo (akili) wanazo, lakini hawafahamu kwazo, macho wanayo lakini hawaoni kwayo na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika. (7:1 79)
 
“Hakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni hawa wanaojipa uziwi na ububu ambao hawayatii akilini (wanayoambiwa au wanayoyaona)” (8:22).
 
Vilevile Alla(s.w) anawashutumu wale wanaobishana kuhusu Yeye pasina kuwa na elimu. Je! Huoni ya kw amba Mw enyezi Mungu amekutiishieni vilivyomo mbinguni na ardhini, na Akakukamilishieni neema zake zilizo dhahiri na za siri? Na wako watu wanaobishana katika (mambo) ya Mwenyezi Mungu pasipo elimu wala uwongofu wala Kitabu chenye nu ru (31:20)
 
Na katika w atu w ako w anaojadiliana juu ya Mw enyezi Mungu bila ya ilimu wala uwongozi wala kitabu chenye nuru (22:8).
 
Kutokana na aya hizi tunabainikiwa kwa uwazi kuwa katika Uislamu suala la kumuamini Allah (s.w) si suala la kibubusa (la kufuata mkumbo tu) bali ni suala la kitaaluma linalohitaji utafiti wa kina wa kisayansi. Kuna maeneo matano makubwa ambayo tukiyazamia vizuri kisayansi, yanatupatia dalili mbali mbali za uwazi zinazotuthibitishia kuwepo kwa Allah (s.w) na utukufu wake usio na mfano wake. Maeneo haya ni: Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake Nafsi ya mwanaadamu Historia ya mwanaadamu Maisha ya Mitume Mafundisho ya Mitume

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1052

Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA
Soma Zaidi...

Adabu ya kuingia katika nyumba za watu
Enyi mlioamini! Soma Zaidi...

Kina Cha uovu wa shirk
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Uchambuzi wa Neema Alizopewa Nabii Sulaiman(a.s)
(i) Kutiishiwa Upepo Qur'an inatufahamisha kuwa Nabii Sulaiman alitiishiwa upepo akaweza kuutumia apendavyo kwa amri yake. Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s. Soma Zaidi...

DUA YA 1 - 10
1. Soma Zaidi...

Imani ya Kiislamu na ni nani muumini?
Soma Zaidi...

Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu
Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu Ni upi? (EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu) Soma Zaidi...

mtazamo wa uislamu juu ya dini
Soma Zaidi...

Maadili kati surat Al-Hujurat (49:1-13)
Enyi mlioamini! Soma Zaidi...

Maswali juu ya mtazamo wa uislamu kuhusu dini
Mtazamo wa uislamu kuhusu dini (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hijabu na kujikinga na zinaa
Soma Zaidi...