Namna ya kuangalia maendeleo ya mtoto akiwa tumboni mwa Mama

Posti hii inahusu zaidi namna ya kuangalia maendeleo ya mtoto akiwa tumboni mwa mama, zoezi hili ufanyika kila mwezi pale mama anapokuja kwenye mahudhurio kwa kufanya hivyo tunaweza kuja maendeleo ya mtoto kwa kila mwezi.

Namna ya kuangalia maendeleo ya mtoto akiwa tumboni mwa mama.

1.Kwanza kabisa tunapaswa kupima mapigo ya moyo ya mama, kupima urefu wa Mama, kupima joto la mwili Mama, msukumo wa damu wa Mama na upumuaji wa Mama kwa kufanya hivyo tunaweza kujua kabisa maendeleo ya mtoto kama vipimo vyote viko sawa kwa Mama na kwa mtoto patakuwa hakuna shida ila kama vipimo vya mama haviko sawa na kwa mtoto huenda pakawepo na shida kwa hiyo hatua za kutibu ufuata au Mama uenda kwa daktari kwa uchunguzi zaidi.

 

2. Pamoja na hayo Mama anapaswa kuangaliwa kama ana damu ya kutosha kwa kuangalia macho, viganja na kama kuna dalili yoyote ya kutokuwepo kwa damu Mama anapaswa kwenda kupima kiwango cha damu na kama ni kidogo ataweza kupewa dawa na kama ni chini ya tano atapaswa kuongezewa damu.

 

3. Kuangalia matiti ya Mama kama kuna aina yoyote ya uvimbe na kuangalia kama matiti yana Dalili za kuwepo kwa maji maji ambayo ni ishara ya kuwepo kwa maziwa baada ya kujifungua, kama kuna dalili za uvimbe  Mama anapaswa kuangaliwa kw karibu zaidi.

 

4.Na pia tunapaswa kuangalia kama Upumuaji wa kwenye tumbo kama ni sawa na kwenye kifua kama ni sawa hiyo ni Dalili nzuri, na pia kuangalia kama tumbo lina makovu au kama Mama amewahi kufanyiwa upasuaji au kama kuna mstari kutoka kwenye kitovu kwenda chini ambayo ni Dalili nzuri za kuwepo kwa mimba.

 

5.Baada ya kuangalia hayo tunapaswa kushika shika tumbo na kuangalia jinsi mtoto alivyolala kama ametanguliza kichwa au matako, kama amelala ki upande au kama kuna mapacha , Mama anapaswa kuambiwa ulalo wa mtoto ili aweze kujiandaa vizuri wakati wa kujifungua.na kama mtoto amelala vibaya Mama anasisitizwa kuzalia hospitalini ili kuepuka madhara mengine.

 

6.Na pia tunapaswa kujua kama mtoto anapumua kwa kusikiliza mapigo ya mtoto kwa dakika moja na kumuuliza Mama kama mtoto anacheza kama hachezi mama anapaswa kwenda kumwona daktari mara moja ili kuangalia tatizo ni nini Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/08/Tuesday - 09:37:43 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1339


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Ujue Ute kwenye uke
Post hii inahusu zaidi Ute ambao umo kwenye uke, Ute huu utofautiana kulingana na hali ya mama aliyonayo, kama mama ana mimba uke utakuwa tofauti na yule ambaye hana mimba au kama Ute una una magonjwa na hivyo utakuwa tofauti. Soma Zaidi...

Madhara ya sindano za kuzuia mimba kwa vijana.
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya matumizi ya sindano za kuzuia mimba kwa vijana ambao hawajafikilia mpango wa kuanza kujifungua watoto. Soma Zaidi...

Kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.
Post hii inahusu zaidi kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, hali hii utokea kwa watoto wadogo wakati wa kuzaliwa kwa sababu maalum kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

Mishipa ya machozi kufunga kwa mtoto.
Posti inahusu nzaidi kufunga kwa mishipa ya machozi ya mtoto kwa kawaida mishipa ya mtoto inapaswa kufunguka baada ya mwaka mmoja lakini kwa wengine ubaki imefungwa hata baada ya mwaka mmoja na kusababisha madhara mbalimbali kwa mtoto. Soma Zaidi...

Aina za uvimbe kwenye kizazi.
Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali za uvimbe kwenye kizazi, uvimbe unatokea kwenye kizazi ila utofautiana kulingana na sehemu ambazo uvimbe huo umepata. Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kwa mama ili apate huduma endelevu.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na huduma kwa mama wajawazito na waliojifungua. Soma Zaidi...

Sababu za kuongezeka uzito wa wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuongezeka uzito kwa wajawazito, Mara nyingi Mama akibeba mimba uongezeka uzito kutoka wiki ya Kwanza mpaka wiki ya mwisho ya kujifungua. Soma Zaidi...

Mbinu za kuwakinga watoto na saratani.
Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo tunaweza kuzitumia ili kuwakinga watoto dhidi ya saratani, kama tulivyotangulia kusema kwamba saratani ya watoto mara nyingi Usababishwa na akina Mama hasa kwa sababu ya mtindo wa maisha wakati wa ujauzito kwa hiyo tun Soma Zaidi...

Faida na hasara za Kufunga kizazi kwa wanawake.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Kufunga kizazi kwa wanawake. Soma Zaidi...

Ongezeko la homoni ya estrogen
Posti hii inahusu zaidi ongezeko la homoni ya estrogen, kwa kawaida homoni hii ya estrogen inapaswa kulingana ikitokea ikaongezeka uleta madhara mbalimbali kwenye mwili na Kuna dalili ambazo zzz inaweza kujionesha wazi mpaka tukafahamu kuwa ni tatizo la o Soma Zaidi...

Habari Mimi ni mjamzito was miezi Tisa sasa nimeanza kutokwa na maji kidogo kidogo ukeni bila uchungu na no mimba yangu ya kwanza he Kuna shida?
Ujauzito husababisha mabadiliko mengi mwilini, ikiwepo ongezeko la Majimaji ukeni ifikapo tarehe za kukaribia kujifunguwa. Majimaji haya ni muhimu kwa afya ya mtoto aliye tumboni. Soma Zaidi...

Dalili za kasoro ya moyo za kuzaliwa kwa watoto
Ikiwa mtoto wako ana kasoro ya moyo wa kuzaliwa, ina maana kwamba mtoto wako alizaliwa na tatizo katika muundo wa moyo wake. Baadhi ya kasoro za moyo za kuzaliwa kwa watoto ni rahisi na hazihitaji matibabu, kama vile tundu dogo kati ya chemba za moyo amb Soma Zaidi...