Namna ya kumfanyia usafi Mgonjwa kwa mwili mzima.

Namna ya kumfanyia usafi Mgonjwa kwa mwili mzima.

Posti hii inahusu namna ya kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima, ni njia ambazo utumika kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima au kumwosha Mgonjwa hasa wale walio mahututi na hawawezi kuamka kitandani.

Namna ya kumwosha Mgonjwa.

1.Kwanza kabisa tunajua kuwa kama mgonjwa hajiwezi na hawezi kuamka mara nyingi usahaulika kwa upande wa usafi, nimeshuhudia mara nyingi wagonjwa wa hivi ukiwaosha hali zao zinabadilika na anapata nafuu na mgonjwa hasipooga kwa mwezi mzima anaweza hasipone haraka kwa hiyo tunapaswa kuwasafisha wagonjwa kama ifuatavyo.

 

2. Kwanza kabisa unaondoa mashuka ya juu ya mgonjwa na hakikisha hakuna Watu ambao hawahusiki na labda msaidizi tu na siku zote tumia maji ya moto na pia ondoa mito na bakiza kidogo ambayo inaweza kumfanya aweze ku kukaa vizuri.

 

3.Anza kutoa mashuka ya upande mmoja wakati mgonjwa umemlaza upande na mashuka  hayo umeyasogeza kwa upande ambao ameulalia na chukua maji na sabuni weka kwenye Dodoki na anza kusafisha upande mmoja na pia hakikisha chini kuna mpira ili kuepuka kulowanisha kitanda na suhuza sehemu hiyo kwa kitambaa   ambacho kimekamuliwa vizuri na hakikisha upande unatakata.

 

4.Mgeuze vizuri mgonjwa kwa upande wa pili na Isha upande huo vizuri kwa kuweka maji na sabuni kwenye Dodoki na sugua vizuri na baadae suuza kwa kitambaa kisafi kilichokamuliwa na ukimaliza upande wa pili, nenda kwenye sehemu za siri weka maji kwenye kutimbaa pangusa vizuri pia suuza nenda kwenye miguu na fanya hivyo hivyo ila kama mgonjwa anaweza kujifanyia usafi kwenye sehemu za siri mwache afanye mwenyewe.

 

5.Baada ya hapo mpake mafuta na ondoa mashuka machafu yaliyokuwepo wakati unamsafisha mvalishe nguo na pia mtandikie vizuri na mgonjwa akifanyiwa hivyo mara kwa mara kama alikuwa mahututi na hali yake itakuwa nzuri kabisa na wakati mgonjwa unamsafisha maji lazima yabadilishwe kutoka sehemu moja kwenda nyingine

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views: 1998

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 web hosting     👉5 ai web app     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

Visababishi vya magonjwa.

Posti huu inahusu zaidi visababishi mbalimbali vya magonjwa, tunajua wazi kuwa ugonjwa ni hali ya kutokuwa kawaida kwa ogani mbalimbali kwenye mwili na kusababisha mwili kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Soma Zaidi...
Mgawanyo wa matibabu ya kifua kikuu.

Posti hii inahusu zaidi mgawanyo wa matibabu ya kifua kikuu, tunajua kubwa kifua kikuu ni Ugonjwa ambao utumia mda mrefu kidogo katika matibabu kwa hiyo mgawanyiko wake uko kwenye sehemu mbili muhimu kama tutajavyoona

Soma Zaidi...
Kazi za wahudumu wa afya wakati wa kutoa dawa kwa wagojwa

Hii post inahusu zaidi kazi za wahudumu wa afya wakati wa kutoa dawa, ni kanuni zinazopaswa kufuata wakati wa kutoa dawa kwa wagojwa.

Soma Zaidi...
Uvimbe kwenye utandu laini uliopo tumboni (peritonitis)

Posti hii inazungumzia kuhusiana na Uvimbe au mashambulizi ya bacteria kwenye utando laini uliopo tumboni ambao kitaalamu hujulikana Kama peritonitis.

Soma Zaidi...
Faida za minyoo

Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za minyoo

Soma Zaidi...