Namna ya kumsaidia mtoto mwenye degedege

Namna ya kumsaidia mtoto mwenye degedege

Degedege ni ugonjwa unaoshambulia sana watoto chini ya miaka mitano,na uwaletea matatizo mengi pamoja na kuwepo kwa ulemavu na vifo vingi vinavyosababishwa na ugonjwa huu.

Zifuatazo ni njia za kumsaidia mtoto kama amepatwa na degedege,

1. Mlaze mtoto kwenye sehemu ambayo itazuia kungata ulimi, kwa sababu mtoto akiachwa na degedege atasikia maumivu  kwenye ulimi na anaweza kushindwa kunyonya au kula

 

2. Kama Kuna makohozi yoyote yanayombana kifuani au kohoni inabidi yatolewe kwa sababu yanaweza kuingia kwenye mfumo wa hewa na kuleta matatizo mengine

 

3.mpatie mtoto dawa ambazo zinahitajika kwa ajili ya kuzuia degedege, dawa hizi ziwe zimeagizwa na daktari hizo dawa zipo hospitalini na uponyesha ugonjwa huu.

 

4. Hakikisha kwamba kiasi Cha sukari kwenye mwili ni Cha kawaida, kama sukari haiko kwenye kiwango chake jaribu kufanya iwe kwenye kiwango na pia angalia kiasi Cha madini kwenye mwili

 

5. Angalia kama joto la mwili liko kawaida, kama  haliko kawaida mpatie dawa za kushusha joto la mwili, angalia pia msukumo wa damu, pia upumuaji,mapigo ya moyo yanaendaje, hakikisha kila kitu kwenye mwili Kiko kawaida

 

6. Hakikisha mtoto Yuko sehemu nzuri ambayo hawezi kuanguka na hakikisha mtoto anaangaliwa mda wote Ili kuepuka madhara mbalimbali yanayoweza kutokea wakati anahudumiwa

 

7. Endelea kuangalia chanzo Cha degedege kama ni maambukizi kutokana na magonjwa nyemelezi au ni bakteria au ni virusi, kama ni ugonjwa wowote inabidi kutibiwa mara Moja.

Angalisho kama mtoto bado ana degedege usimpe kitu chochote Cha kula kwa kupitia mdomoni maana chakula kinaweza kuingia kwenye mfumo wa hewa.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views: 4854

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game     ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰4 web hosting     ๐Ÿ‘‰5 ai web app     ๐Ÿ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa walioingiliwa na uchafu puani.(foreign body).

Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa alieye ingiwa na uchafu puani (foreign body)

Soma Zaidi...
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENGโ€™ATWA NA NYUKI

Kungโ€™atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki.

Soma Zaidi...
Ratiba ya chanjo ya kifua kikuu

Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kifua kikuu, hiii ni ratiba ambayo chanjo hii utolewa na ushauri mbalimbali utolewa ili kuweza kufanikisha kazi ya chanjo hii

Soma Zaidi...
Madhara ya ulevi

Poshi hii inahusu madhara ya ulevi.Utegemezi wa pombe kwa kawaida humaanisha kuwa mtu anatumia kiasi kikubwa cha pombe na kuna masuala kuhusu kupoteza udhibiti.

Soma Zaidi...
Zijue faida za maji ya uvuguvugu.

Posti hii inahusu zaidi faida za maji ya uvuguvugu, hasa hasa maji haya ni vizuri kabisa kuyatumia hasa wakati wa asubuhi na pia wakati tumbo likiwa halina kitu, kwa hiyo zifuatazo ni faida za maji ya uvuguvugu.

Soma Zaidi...
Ratiba ya chanjo ya kuzuia kuharisha

Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kuharisha hii ni chanjo wanayopewa watoto wadogo chini ya miaka mitano kwa lengo la kuzuia kuharisha chanjo hiyo kwa kitaalamu huitwa Rotarix.

Soma Zaidi...