image

Namna ya kuongeza na mjamzito ili kupata taarifa zake na kutoa msaada

Posti hii inahusu zaidi namna ya kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kugundua tatizo lake na kutoa msaada pale penye uhitaji.

Namna ya kuongea na mjamzito.

1.Kwana kabisa hakikisha kama kuna mazingira ambayo yatafamfanya ajisikie vizuri na mazingira yawe na vitu vinavyohitajika na uhakikishe kubwa anaweza kukaa vizuri na kuweza kujisikia huru pale unapoongea naye.

 

2.Muulize kuhusu familia yake na watoto alionao kwa sasa na unapaswa kujua anataka kuwa na watoto wangapi, uliza kama anajua tarehe yake ya kujifungua kama hajui hakikisha anatoka kwako anajua tarehe maalum ya kujifungua.

 

3.Pia muuulize kama as mewahi kutumia uzazi wa mpango, na amepata faida gani au hasara zilizopata kutokana na uzazi wa mpango, kama hana taarifa yoyote kuhusu uzazi wa mpango mafundishe ba uhakikishe anajua jinsi ya kutumia uzazi wa mpango.

 

4.Ongea naye kuhusu dawa anazozitumia kwa sababu kuna wengine wanatumia dawa mbalimbali kama vile za kisukari, presha, degedege,na wengine dawa za kuongeza maisha, ongea naye na umpe ushauri kadri unavyoweza kuhusiana na matumizi ya dawa na matokeo yake.

 

5. Muuulize kuhusu matumizi ya vyakula mbalimbali kwa mfano ni vyakula gani anapendelea na kumshauri kuhusu mlo kamili kwa wajawazito hasa vyakula vya kuongeza damu na madini ya chuma anapaswa kuvitumia kwa wingi na pia anapaswa kuachana na vyakula ambavyo havina faida yoyote mwilini kama vile pemba na utumiaji wa mawe wakati wa ujauzito.

 

6.Pia ongea naye kuhusu matumizi ya vileo kama vile matumizi ya madawa ya kulevya, vileo vikali, uvutaji wa sigara, na vitu kama hivyo ambayo usababisha madhara makubwa kwa mtoto wakati akiwa tumboni, kama kuna matumizi yoyote ya vitu kama hivyo elimu inapaswa kutolewa ili kuzuia matumizi ya vileo 

 

7.Pia tunapaswa kujua kama Mama amepata chanjo zinazohitajika wakati wa ujauzito kama vile chanjo ya pepopunda ambayo umkinga mama na mtoto dhidi ya magonjwa ya kupooza na Magonjwa mbalimbali mbalimbali, kama hajapata hakikisha mama anapata chanjo hiyo 

 

8.Pia ongea na Mama kuhusu Maambukizi ya virusi vya ukimwi na matumizi ya madawa na pia kuhusu Magonjwa ya ngono na matumizi ya dawa, mama kama hana taarifa zozote kuhusu hayo anapaswa kupima na kupewa dawa kama kuna Maambukizi.

 

9.Pia Mama anapaswa kuwa na uhusiano mzuri na watu kwa sababu mimba inaweza kumfanya akabalika katika hali isiyo ya kawaida au pengine anaweza kuwa na hasira na watu basi Mama anapaswa kuambiwa wazi kuwa anapaswa kuwa chukuliwa watu Kawaida na kumhakikishia kuwa akijifungua kila kitu kitakuwa sawa.

 

10.Pia tunapaswa kujua hali ya uchumi wa Mama mjamzito kama anaweza kupata mahitaji ya kila siku ya kawaida na kama akifanikiwa wakati wa kujifungua kama ataweza kupata hela ya kununua mahitaji wakati wa kujifungua, kama hawezi tafuta jinsi ya kumsaidia na kumshauri akate bima ya shilingi elfu thelathini kwa watu sita na itaweza kumsaidia wakati wa kujifungua.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/08/Tuesday - 09:10:41 am Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 548


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Mabadiliko ya uzito kwa mjamzito
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya uzito kwa mjamzito, hii ni hali ya kubadilika kwa uzito kwa Mama akiwa na Mimba Soma Zaidi...

Sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake Soma Zaidi...

Chanzo cha tezidume, dalili zake na tiba zake.
Post hii inakwenda kukufunza mambo mengi kuhusu tezi dume kama chanzo, dalili, matibabu, njia za kujikinga na mambo hatari yanayoweza kukusababishia kupata tezi dume. Soma Zaidi...

Je tumbo huanza kukua baada ya mda gan?
Ni Swali kila mjamzito anataka kujiuliza hasa akiwa katika mimba ya kwanza. Wengine wanataka kujuwa ni muda gani anujuwe mavazi makubwa. Kama na wewe unataka kujuwa muda ambao tumbo huwa kubwa, endelea kusoma. Soma Zaidi...

Ni ipi hasa siku ambayo nitafute ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kutafuta ujauzito Soma Zaidi...

SABABU ZA KUTOKA KWA MIMBA (sababu za kuharibika kwa ujauzito)
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka. Soma Zaidi...

Sabau za maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...

Mishipa ya machozi kufunga kwa mtoto.
Posti inahusu nzaidi kufunga kwa mishipa ya machozi ya mtoto kwa kawaida mishipa ya mtoto inapaswa kufunguka baada ya mwaka mmoja lakini kwa wengine ubaki imefungwa hata baada ya mwaka mmoja na kusababisha madhara mbalimbali kwa mtoto. Soma Zaidi...

Siku za kupata mimba
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba Soma Zaidi...

Mwanamke mwenye HIV akiwa mjamzito ama ananyonyesha
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mwanamke mwenye HIV akiwa mjamzito ama anaenyonyesha Soma Zaidi...

Nini husababisha mtoto kukosa maji kabla ya kuzaliwa?
inaweza kutokea kuwa mtoto aliye tumboni akaishiwa maji hata kabla ya kuzaliwa. yes hali hii huweza kuwapata baadhiya watoto. Soma Zaidi...

Jifunze kuhusu Protini, Fati, Wanga na kazi zao mwilini na vyakula vinavyopatikaniwa kwa wingi
Soma Zaidi...