NAMNA YA KUTAWADHA YAANI KUCHUKUWA UDHU


image


Kuchukuwavudhu ni ibada, lakini pia ni matendo ya kuufanya mwilivuwe safi. Katika post nitakwenda kukifundisha namna ya kutia udhu katika uislamu.


Ili uweze kutawadha kwanza unatakiwa uandae maji yaliyo safi.  Maji safi ni yale ambayo hayajachanganyika na najisi na yakawa yamenajisika. 

 

Baada ya kuandaa maji yako sasa ni wakati wa kutekeleza ibada ya udhu.  Vyemakuanza kupigamswaki.  Kwani kupiga mswaki ni sunnah ambazo zimesisiyizwa sana katika Uislamu. 

 

Hatuwa za kuchukuwa udhu:

1. Kutia nia:

Nia ni kukusudia kitendo. Hii ni hatuwa ya kwanza na muhimu kwani Mtume s.a.w amesema "kila jambo hulipwa kwa kuzinhatia nia" hadithi ni sahihi. 

 

2. Anza na kupiga bismillah kisha osha kiganja vya mikono.  Osha kwanza kabla hujatumbukiza mikono kwenye chombo. 

 

3. Kisha osha uso: 

Uso unatakiwa uoshwe kwa marefu hake na mapana.  Hakikisha unaziosha sehemu zote za uso kama kwenye kidevu na kufika hadi kwenye maoteo ha masikio.  Uoshaji wa uso unaambatana na kusukutuwa na kuingiza maji puani. 

 

Hivyo basi kwa mpanhilio utaanzakusukutuwa kisha utaingiza maji puani.  Utafanya hivi mara tatu kisha ndipo utaosha uso pia utaosha mafa tatu.  Pia utaosha na kwenye ndevu kuhakikisha kuwa ngozi ya kidefu imepata maji. 

 

4. Kuosha mikono. 

Baada ya kumalizakuosha uso utaosha mikonokwa utaratibu utaanza mkono wa kulia mara tatu kisha mkono wa kushoto mara tatu. Hakikisha kuwa mkono unauosha mpakakwenye kiwiko.  Vyema ukafika juu zaidi. 

 

Endapo mkonoutakuwa huna amaumekatwa utaosha kipande kilichopo.  Baa ya kumaliza mkono wa kulia utaosha wa kushoto. 

 

5. Kupaka maji kichwani: 

Hapa utafanya hivi mara moja kama alivyokuwa akifanya Mtume S.A.W. Hata hivyo hakuna ubaya ukizidisha.  Lengo hapa ni kuoaka maji kichwani na si kuosha nywele. 

 

Upakaji wa maji utaendana na kupaka maji kwenye masikio. Nje ya masikio nandani yake. Kidole cha cha shahada kiingie ndani yavsikio na gumba kipake juu ya sikio. 

 

Ni katika sunnah kutumia maji yaleyale yaliotumika kupakakichwa.  Yaani baada ya kupaka maji kichwani utaingiza kidole cha shahada ndani ya sikio,  kisha gumba wwka juu ya pindo za sikio kwa juu na kupaka maji. 

 

Unapopaka kichwa utaanzia mbele kuja nyuma kisha utatoa nyumana kuleta mbele,  kisha ndipp utamalizia masikioni .

 

6. Kuosha miguu

Kisha utaosha miguu miwili mara tatutatu.  Utaanza wa kulia na kumalizia wa kushoto.  Hakikisha maji yanaingia mpaka kwenye mipasuko ya miguu yaani magaga.  Hakikisha unaosha mpaka kwenye fundo zamiguu yaani kungu za miguu. Vyema ukizidisha mpaka kwenye ugoko. 

 

Baada ya hapo utakuwa umeshatia udhu. Usikose post inayofuata itazungumzia dua ya kumaliza kutia udhu. 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    6 Maktaba ya vitabu    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Maandalizi kwa ajili ya kifo
Mwanadamu anatakiwa aishi huku akikumbuka kuwa ipo siki atakufa. Hivyo basi inatupata lujiandaa mapema kwa ajili ya kifo. Soma Zaidi...

image Nguzo za swaumu (kufinga)
Hapa utajifunza nguzo kuu za swaumu. Kama hazitatimia nguzo hizi basi swaumu itakuwa ni batili. Soma Zaidi...

image Je ni nani mwenye haki ya kutaliki
Hapabutajifunza endapp mwanamke anahitaji kuachwa ni nini anatakiwa afanye. Soma Zaidi...

image Ni upibutaratibu wa kuingia eda na kutoka eda
Katika uislamu hakuna sheria ya mwanamke kuingizwa eda na kutolewa eda kama ilivyozoeleka. Endelea na post hii ujifunze zaidi Soma Zaidi...

image Zijuwe nguzo 17 za swala.
Ili swala itimie utahitajika kutimiza nguzo zake na masharti yake. Hapa utajifunza nguzo 17 za swala. Soma Zaidi...

image Fadhila za usiku waalylat al qadir
Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kiswali swala ya tahajud na swala za usiku yaani qiyamu layl
Post hii itakujuza jinsi ya kiswali swala ya tahajudi. Pia utajifunza jinsi ya kuswali swala za usikubyaanibqiyamublayl Soma Zaidi...

image Ni zipi najisi katika uislamu
Post hii inakwenda kukupa orodha ya vitu vilivyo najisi. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kiswali swala ya haja
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya haja na jisi ya kuiswali. Soma Zaidi...

image Jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali kulingana na ugonjwa wake. Soma Zaidi...