picha

Namna ya kutayamamu hatuwa kwa hatuwa

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu.

Kutayammamu

Kutayammamu ni kujitwaharisha kwa kutumia udongo safi. Waislamu huruhusiwa kujitwaharisha kwa kutayammamu katika hali ya dharura ya:
(i)Ugonjwa usioruhusu kutumia maji.
(ii)Kuwa safarini na kukosa maji ya kutumia au kuwa katika mazingira ya safari yasiyoruhusu kutumia maji.
(iii)Kukosa maji.
Tunajifunza haya katika aya ifuatayo:

 

“Na mkiwa wagonjwa au mumo safarini au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi, kusudieni udongo ulio safi (tayammamuni) kwa kuzipaka nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mw enyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru”. (5:6)

 


Katika aya hii tunajifunza kuwa kutayammamu kumeruhusiwa kwa wakati wa dharura tu. Funzo hili tunalipata katika maneno ya Allah kuwa, “Hapendi Allah kukutieni katika taabu”

 


Masharti ya Kutayammamu

Tayammamu haitaswihi mpaka yatakapozingatiwa masharti yafuatayo:
1. Ipatikane dharura inayompelekea mtu kuruhusiwa kutayammarnu.
2. Pawe na hitajio la tayammamu kama vile kuswali, kutufu n.k.
3. Kama kusudio la kutayammarnu ni kutekeleza swala ya faradh, tayammamu hiyo ifanyilce baada ya kuingia wakati wa swala hiyo.
4. Pawe na udongo safe (ulio twahara na ulio katika asili yake) ulio mkavu na wenye vumbi vumbi.

 

Nguzo za Tayammam
Nguzo za tayammam zinabainishwa na aya ifuatayo:
`... Basi kusudieni udongo ulio safi na kupaka nyuso zenu nn mikono yenu..." (4:43)
Aya hii inabainisha kuwa nguzo za tayammam ni:

 


(i)Nia (kukusudia udongo).
(ii)Kupaka uso.
(iii)Kupaka mikono.
(iv)Kufuata utaratibu huu.
Nampa ya Kutayammamu
(i)Kutia nia. Nia huwekwa pale Muislamu anapokusudia udongo na kuutayarisha kwa ajili ya tayammamu.
(ii)Kupaka uso. Piga udongo uliokusudia kwa viganja vyote viwili vya mikono, kisha puliza viganja iii takataka na vijiwe jiwe vilivyo juu yake vitoke. Kisha paka uso wako kwa kutumia viganja viwili kwa pamoja.

 


(iii) Kupaka mikono. Anza kupaka mkono wa kulia kwa kiganja cha kushoto. Weka kiganja cha kushoto nyuma ya kiganja cha kulia. Paka mkono wa kulia kuanzia hapo kwa kurudisha kiganja cha kushoto kinyume nyume mpaka kwenye fundo kisha kupaka sehemu ya juu ya mkono wa kulia na kuishia kwenye kidole gumba bila ya kuugusa kiganja mkono wa kulia. Utarudia zoezi hilo kupaka mkono wa kushoto.

 


Kutumia Ukuta kwa Ajili ya Tayammamu

 


Mtume (s.a.w) aliwahi kutayammamu kwa kutumia ukuta wa nyumba kama inavyobainika katika hadith ifuatayo:
“Abu Juhaim Al-A nsary (r.a) amehadithia kuw a Mtume w a Allah (Rehema na amani ziwe juu yake) alikuja kutoka upande wa Bir-al-Jamal. Mtu mmoja alimuona akamsalimia. Lakini Mtume hakumjibu, bali alienda kwenye ukuta wa nyumba akapakaza viganja vyake vumbi la ukuta kisha akapaka uso wake wote, kisha mkono wa kulia na wa kushoto, ndipo akamrudishia salamu ”. (Bukhari na Muslim).

 


Kutokana na hadithi hii tunajifunza kuwa vumbi kwa ajili ya tayammamu si lazima liwe la ardhini tu bali ukuta au jiwe au sehemu yoyote yenye vumbi vumbi iliyotwahara inafaa kutumika kwa ajili ya tayammamu. Kwa mfano wakati wa mvua ambapo udongo umelowana ukuta wa nyumba au ukuta wa chombo cha usafiri au sehemu yoyote yenye vumbi vumbi au iliyokavu na twahara, itakuwa aula kuitumia kwa tayammamu.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2022/08/13/Saturday - 11:35:54 am Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1943

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Fadhila za usiku waalylat al qadir

Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000.

Soma Zaidi...
Kwanini lengo la zakat na sadaqat halifikiwi katika jamii yetu

Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Nguzo za swala ya maiti

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
maana ya Eda na aina zake

Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine.

Soma Zaidi...
Taasisi za Kifedha Katika Mfumo wa Uchumi wa Kiislamu

- Ni taasisi za kifedha zinazohusika na kuhifadhi akiba na mali za watu zenye thamani kubwa kama dhahabu, n.

Soma Zaidi...
Kutoa kati kwa kati

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...