Namna ya kutoa huduma kwa mgonjwa wa Dengue.

Posti hii inahusu zaidi huduma anayopaswa kupata mgonjwa wa ndengue, kwa sababu tunafahamu wazi Ugonjwa huu hauna dawa ila kuna huduma muhimu ambayo anaweza kupata na akaendelea vizuri.

Huduma kwa mgonjwa wa Dengue.

1.Kwa hali ya kawaida Ugonjwa ambao unasababishwa na virusi huwa hauna dawa lakini kuna huduma mbalimbali ambazo utolewa na mgonjwa anaweza kupona na kuendelea na hali yake ya kawaida na pengine huwa tiba inayotolewa kuendana na dalili iliyopo kama Mgonjwa anaumwa kichwa dawa ya maumivu utolewa au kama anaharisha dawa ya kuzuia kuharisha utolewa na mambo kama hayo hatimaye Mgonjwa anapata nafuu na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

 

2. Kwa sababu mgonjwa wa Dengue anakuwa na maumivu makali ya kichwa kwa kawaida anapewa dawa ya maumivu na kwa wakati mwingine anapewa maji ambayo yamependekezwa na wizara ya afya ni lingers na pengine Mgonjwa kama ana uwezo wa kunywa maji ya kawaida anaweza kunywa na pia kuna wakati mwingine hali ikiwa imefikia pabaya mgonjwa huwa anatoa damu kwa hiyo kuna hatari ya kupungukiwa damu kwa hiyo anaongezea damu na anapewa dawa ya kusaidia damu iache kutoka mara kwa mara.

 

3. Vile vile Tunapaswa kuzuia Ugonjwa huu kwa kwa kuwapatia watu elimu kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huu na kuwapatia mbinu za kujikinga na ugonjwa huu kwa kutumia neti wakati wa usiku kukata vichaka na mazalia ya mbu na kwa wakati mwingine kutumia dawa za kujipaka ili kuweza kupunguza kiwango cha kuenea kwa mbu.

 

4. Kwa hiyo baada ya kujua Ugonjwa huu jamii pia inapaswa ielezwe wazi pale Ugonjwa huu unapotokea ili kuweza kuwafahamisha watu wajue namna ya kujikinga na hasa kuwakinga watoto wadogo na wazee ambao wapo kwenye hatari kubwa ya kupata matatizo zaidi, kwa hiyo na mila na desturi potovu zinapaswa kuepukwa wakati wa kipindi hiki cha Ugonjwa huu ili kuepuka madhara na matatizo yatokanayo na Ugonjwa ambao hauna dawaJe! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/04/08/Friday - 07:26:12 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 871


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-