NAMNA YA KUTUNZA CHUMBA CHA UPASUAJI


image


Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza chumba cha upasuaji, chumba cha upasuaji ni tofauti na vyumba vingine kwenye hospitali kwa hiyo vinahitaji uangalizi wa hali ya juu sana ili kuepuka aina yoyote ya uchafu kuwepo kwenye chumba hicho, zifuatazo ni namna ya kutunza chumba cha upasuaji.


Namna ya kutunza chumba cha upasuaji.

1.Chumba cha upasuaji kinapaswa kuwa na mjengo wa aina yake , kinapaswa kiwe na hewa maalum inayohitajika, madirisha hayapaswi kuwa wazi yanapaswa walau kubwa na wavu ili kuzuia wadudu au uchafu wowote kuingia hasa wakati wa upasuaji na wavu huo ufanyiwe usafi mara kwa mara, pia panakuwepo na sehemu mbalimbali kwenye chumba hicho ili kuweza kuwaruhusu wahudumu kufanya kila kitu kwenye sehemu yake.

 

2.Chumba cha upasuaji kinapaswa kuwa kwenye hali ya usafi kwa wakati wote.

 Usafi kwenye chumba hiki unapaswa kufanyika kila siku walau mara mbili na zaidi kutegemeana na hali ya wagonjwa wanaohudumiwa kwenye sehemu hiyo na kila kitu kinapaswa kusafishwa iwe meza, sakafu na kufuta mavumbi kwenye sehemu mbalimbali na ikitokea labda kuna damu yoyote imetoka kwa mgonjwa inapaswa kutolewa mda huo huo na sehemu hiyo inapaswa kusafishwa na kemikali ambayo inaweza kuua wadudu wote kwa hiyo kemikali inapaswa iwe na nguvu sana.

 

3. Kutunza vizuri vifaa vilivyomo kwenye chumba cha upasuaji.

Tukumbuke kwamba vifaa vinavyotumika kwenye  chumba hiki uweza kutumika mara nyingi kwa hiyo usafishwa kwa utaalamu wote mpaka wadudu wanaungua wote na kuweza kutumika tena kwa mgonjwa mwingine kwa hiyo vinapaswa kubaki kwenye hali ya usafi wa hali ya juu sana ili kuweza kuepuka Maambukizi. Kwa hiyo mtunza vifaa na msafishaji wa vifaa wanapaswa kuwa na elimu ya kutosha kwa kazi hiyo ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

 

4.Chumba cha upasuaji kinapaswa kwa na kila aina ya nguo zinazotumika wakati wa upasuaji.

Nguo zenyewe ni pamoja na kofia inayozuia nywele zisianguke kwenye mwili wa mgonjwa wakati wa upasuaji, maski inayozuia uchafu wowote kutoka puani wakati wa kupiga chafya na uchafu kutoka mdomoni, gauni linazuia uchafu wowote kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa wahudumu inawezekana kuwa ni damu au majimaji yoyote, gloves ambazo zinazuia kugusa damu au majimaji ya wagonjwa ambayo yanaweza kuwa na virusi vinavyoweza kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu au kwa mhudumu kwenda kwa mgonjwa.

 

5.Kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa katika chumba cha upasuaji mgonjwa anayeingia pengine uweza kupasuliwa sehemu kubwa sana na ni rahisi wadudu wanaweza kuingia kwa namna moja au nyingine kwa hiyo wakiingia wanaweza kusababisha madhara makubwa zaidi kuliko ya kwanza kwa hiyo chumba hiki uwekwa kwenye hali ya juu kwa usafi na wahudumu wa hapo wanapaswa kuwa na maarifa makubwa kwa hiyo ni vizuri na haki kukiweka chumba hiki kwenye hali ya juu ya usafi.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Viwango vitatu vya kuungua.
Posti hii inahusu zaidi viwango vitatu vya kuungua. Ili tuweze kujua mtu ameunguaje Kuna viwango vitatu vya kujua kiasi na namna mtu alivyoungua Soma Zaidi...

image Huduma ya Kwanza kwa aliyeungua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa aliyeungua Soma Zaidi...

image Kwanini mdomo unakuwa mchungu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za mdomo kuwa mchungu Soma Zaidi...

image Makundi yaliyo katika hatari ya kupata Ugonjwa wa ngiri.
Posti hii inahusu zaidi makundi ambayo yapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa ngiri, ni hatari kwa sababu tunajua kuwa ngiri utokea kwa sababu ya kuta au tishu zinazoshikilia viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwepo kwa uwazi na kufanya viungo hivyo kutoshikilia vizuri katika sehemu inayostahili, kwa hiyo kwa sababu mbalimbali makundi yafuatayo yako kwenye hatari ya kupata tatizo hilo kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwapa huduma na uangalizi wa karibu kadri iwezekanavyo ili kuepuka Tatizo la kupata ngiri. Soma Zaidi...

image Dalili za ujauzito: Nini kinatokea kwanza
Je, unafahamu dalili za mwanzo za ujauzito? Kutoka kwa kichefuchefu hadi uchovu, ujue nini cha kutarajia. Soma Zaidi...

image Dalili za ukimwi, unavyoenezwa na njia za kujikinga
Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.unasababishwa na virusi ambavyo hutokea kwa mtu mwingine kwa njia mbalimbali Soma Zaidi...

image Ugonjwa wa UTI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa UTI Soma Zaidi...

image Imani potofu juu ya ugonjwa wa Ukimwi.
Posti hii inahusu zaidi imani potofu juu ya ugonjwa wa Ukimwi,ni Imani walizonazo watu wengi kuhusiana na ugonjwa wa Ukimwi. Soma Zaidi...

image Upungufu wa protin
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa protini Soma Zaidi...

image Maumivu wakati wa hedhi.
Posti hii inahusu zaidi maumivu wakati wa hedhi, haya ni maumivu ambayo utokea wakati wa hedhi kwa wanawake walio wengi, wengine huwa hawayapati kabisa na wengine hutapata na kwa kiwango kikubwa kutegemea na matatizo mbalimbali kama tutakavyoona. Soma Zaidi...