Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza nywele za mgonjwa hasa kwa wagonjwa mahututi na wale wasiojiweza tunafanya hivyo ili tuweze kuwatoa kwenye hali ya usafi.
Namna ya kutunza nywele za mgonjwa ambaye hajiwezi.
1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa mara nyingi tunakuwa na wagonjwa majumbani kwetu na tunashindwa kuwahudumia kwa sababu ya kutojua au pengine tunashindwa tuwahudumie namna gani kwa hiyo na nywele za mgonjwa zinapaswa kusafishwa kwa njia zifuatazo.
2.Kwanza kabisa unapaswa kumwambia mgonjwa nia na lengo la kumfanyia usafi kama mgonjwa anaweza kusikia na pia hakikisha kuwa hakuna Watu ambao hawahusiki ili mgonjwa aweze kujisikia huru unaweza kuwa na msaidizi wako.
3.Ondoa nguo kwenye sehemu ya kichwa na weka nguo za kumwoshea Mgonjwa inaweza kuwa kanga au kitambaa chochote ambacho ukitoa unaweza kukiosha tena na weka mpira ili maji yasidondoke kwenye godoro na Mashuka mengine.
4.Msaidie mgonjwa aweze kusogeza kichwa chake juu ya kitanda ili kuweza kuwa karibu na beseni na hakikisha kichwa kipo kwenye beseni na wakati wa kumwosha nywele tumia maji ya moto .
5 Chukua maji kutoka kwenye beseni na mwekee mgonjwa na mwekee kwenye kichwa cha Mgonjwa na weka sabuni safisha nywele za mgonjwa na hakikisha kuwa zimetakata na pia chukua taulo safi upanguse nywele za mgonjwa na safisha sehemu ambapo mgonjwa alikuwepo na hakikisha mgonjwa nywele zake zimekuwa safi.
6.Mpake mafuta mgonjwa kwenye nywele zake na kama kuna mba unaweza kuweka dawa ili kuepuka hali ya kujikuna kama inawezekana unaweza kumsuka kama ni mwanamke.
7.Kwa hiyo baada ya kujua haya tuwafanyie usafi wa nywele wagonjwa na mtaweza kuona mabadiliko kwa sababu pengine hali ya mgonjwa uendelea kubwa mbaya kwa sababu ya kuwepo kwa uchafu kwa kumfanyia mgonjwa usafi anaweza kupata nafuu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi mkojo wa kawaida kwa kila mwanadamu na unavyopaswakuwa, mkojo wa kawaida kwa binadamu huwa na sifa zifuatazo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuchoma chanjo, ni njia ambazo utumika kutoa chanjo kwa watoto na watu wazima kwa utaratibu uliowekwa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi huduma Kwa mgonjwa mwenye maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo,ni huduma maalumu ya kumsaidia mgonjwa aliyepata maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo.
Soma Zaidi...Unapokuwa na kizunguzungu unashindwa kuudhibiti mwili wako, unaweza kuanguka kabisa.
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunza sababu zinazowezabkuorlekea kibofu kuuma upande mmoja
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu mwenye kizunguzungu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja, ni njia ambazo utumika ikiwa kuna damu inavuja kwenye sehemu yoyote ya mwili,kwa hiyo tunaweza kutumia njia hizi ili kuepuka kuendelea kuvuja kwa damu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea mambo ambayo hayawezi kuambukiza UKIMWI
Soma Zaidi...