Ndani ya jumba la aladini

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

NDANI YA JUMBA LA ALADINI

Hatimaye Aladini anaingia ndani, Loo! Alitamani kupiga kelele, huku ameziba mdomo wake kwa mshangao. Uzuri wa ndani ulikuwa mara dufu ya nje. Ukumbi kubwa ilio katika umbo la duara. Mlango mkuu wa kuingilia kwenye ukumbi ulukuwa na pazia la rangi ya kijivu. Maashindi ya kiarabu yaliyopangiliwa na kutengeneza umbo la uwa zuri lililoonekana kuchanua. Maandishi yalikuwa ya rangi za kuchanganyika huku rangi ya zambarau ikitawala vyema. “Marhaban bikum” yaani karibuni sana, yalikuwa ndio maneno yaliyoandikwa yalivyosomeka.

 

Zuria la rangi nyekundu lilitandikwa na kuenea ukumi mzima. Zuria lilikuwa na michirizi ya zambarau na kutengeneza madoa makubwa ya rangi ya buluu. Zuria lilichanganya rangi nyingine na kutengeneza mauwa majubwa yaliyo mazuri. Rangi za mauwa hayo zilifanana sana na rangi za magoya ya kanga. Yaani madoa meupe na meuzi. Madirisha makubwa yaliyongaa vyema na kuonyesha kwa ufasaha kilicho nje. Michirizi ya madirisha ilikuwa inavutia kama vile ni mikufu ya dhahabu iliyoning’inizwa kweye vipete vya madirisha.

 

Mapazia yaliyokunywa mafundo yalining’inia kwenye madirisha. Aladini aliliendea dirisha moja na kufungua pazia. Loo! Lilikuwa ni pazia zuri sana, lenye rangi ya kijivu kama lile pazia kubwa. Pazia lilikuwa na picha ya ndege yule aliyeunganisha roho mbili hizi. Alikuwa ni ndege mzuri sana kwa kumuangalia. Vipete kwa kuning’inizia pazia vilikuwa vya rangi ya ugoro iliyo wiva sana iliyochanganyika na michirizi ya rangi ya samawati na kutengeneza mabadilishano ya rangi kama pundamilia aliyenona. Pazia lilifunika diisha na kushuka kwa chini na kutengeneza sura ya kuvutia.

 

Meza kubwa iliyozungukwa na viti iliwekwa katikati ya chumba. Ibila shaka ni meza ya kulia chakula, kwani vitu vilivyoonekana kwenye meza vinasadivu yaliyomo. Masinia 6 yaliyofunikwa na makawa ya rangi ya samawati, yenye micirizi ya kahawiya kwa chini. Masinia yalingaa kama ni almazi iliyowekwa. Kabaesni kadogo kalikojaa vijiko, visahani na vitu vingine. Maji safi yalionekana kwenye jagi. Ni masafi sana kiasi cha kuonyesha kana kwamba jagi ni tupu. Aani anaonekana aliye upande wa pili kama ni kioo. Harufunzuri ilikuwa ikitokea kwnye meza kubwa.

 

Viti vikubw avyenye magodoro ya harir vilizunguka meza na kutengeneza duara lama kiota cha mayai ya kuku anayelalia. Viti vizuri vilivyokuwa vya rangi za kupendeza na kuwekwa vikuku nya lulu pembeni ya kila kimoja. Basi uzuri ulioje wa ndani ya jumba hili. Juu karabai mishumaa mikubwa ya rangi nyekundu na njano ilining’inizwa ikiwa kwenye matovu makubwa ya rangi ya zamabarau. Matovu yalionekana kuwa na vijiwe vya ranirangi vikining’inia hakuna aliyejuwa ni madini ya aina gani. Ila vijiwe hivi ifikapo usiku kuakisi mwanga kutoka kwenye mishumaa na kugeuka kama taa zinazowaka.

 

Mjakazi mkubwa aliyeandaliwa na mama Aladini akaanza kupanga kundi la wajakazi na wafanyakazi kila mmoja kwenda kwenye eneo lake la kazi. Mjakazi mwingine aliye mrefu zaidi na mzuri sana akamchukuwa Aladini na mke wake kuwapeleka kwenye chumba chao. Walikutana na mfululizo wa mapazia yasiyopungua 5 ynye rangi mbalimbali za kupendeza. Hatimaye wakakaribishwa na harufu nzuuri iliyotoka nyuma ya pazia lenye rangirangi kama uwa la waridi. Mjakazi akawakaribisha na kurudi nyuma, huku akimuashiria binti sultani sasa ni kazi kwake kuongoza njia.

 

Mjakazi akabakia pale pale, binti sultani akafungua pazia, Loo! Kitasa cha dhahabu kikawakaribisha. Aladini kwa mkono wake akafungua kitasa, mlango ukafunguka. Hatimaye wawili hawa wapo ndani, kinanukia sana chumba chao. Uzuri wa chumba na mapambo hakukuwa na tofauti sana ya kile chumba cha binti Sultani. Tofauti ni kuwa vitu vyake vilikuwa ni vya thamani sana. Hatimaye kwa uchovu wa safari wawili hawa wakaamuwa kupumzika na mlango ukafungwa.

 

Atimaye siku ikaenda hivyo na muda wa chakula ukafika, wakapata chakula kizuri. Mama Aladni aliendeela kuwa pale, ijapokuwa hakupendelea kuishi pale. Alitarajia baada ya ujio wa Sultani arudi nyumbani kwake. Mama Aladini ijapokuwa mambo yote alikuwa akiyashuhudia kwa macho yake lakini hakuwa akiamini hasa uhalisia na nini itakuwa hatima ya mambo yale. Hivyo hakutaka kulekeza maisha yake ya mwanzo kirahisi. Masi ambo yakawa hivyo na usiku ukaingia na hatimaye kukakucha.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela2 Main: Burudani File: Download PDF Views 1562

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Aladini na binti wa mfalme

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu

Soma Zaidi...
Hadithi iliyosimuliwa na mshona nguo

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu

Soma Zaidi...
Kwa nini mkono umekatwa

KUKATWA MKONO NA KURITHI UTAJIRI Basi niliweza kulala kwa mke wangu siku ile na asubuhi nilimuashia kipande 1000 vya dhahabu na kuondoka kuelekea dukani.

Soma Zaidi...
Alif lela ulela

Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Familia mpya baada ya harusi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

Soma Zaidi...
Kukatwa mkono na kuurithi utajiri

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Hatima ya kijana mchonganishi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...