image

Ndani ya pango la makaburi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

NDANI YA PANGO LA MAKABURI

Mmoja wapo akatowa kamba na kulifunga jeneza vizuri na kuanza kulishusha chini ya mapango kwa kamba ile.hatimaye n ikahisi jeneza limefika chini kutokana na kugonga chini. Nikalifungua jeneza lile na kutowa mikate yangu nane na maji yangu. Nikaangalia huku na huku hakuna pa kutokea. Nikaangalia juu ni mbali sana na tundu ni dogo na hata sauti haifiki. Nilizunguka mchana mzima sikupata pa kutokea. Sikuya kwanza, pili, tatu mpaka siku ya nne sikupata pa kutokea. Nilikata tamaa nikajua sasa huu ndio mwisho wa Sinbad.

 

Nikaanza kula mikate yangu kwa kuilinda ili isiishe kwa araka. Sasa imefika siku ya sita nikiwa na mikate miwili mkononi. Ilipofika siku ya saba mida ya mchana nikasikia migongano. Nikasogea karibu kwenye lile tundu loo!! ni jeneza linakuja. Nilikuwa nikihisabu siku kwa kuangalia mwanga kwenye tundu lile dogo la kuingizia majeneza. Jeneza lile lilipofika chini nikaona mwanamke aliye hai amezikwa na mumewe. Mwanamke yule nikamsaidia kutoka pale nikiwa na imani kuwa ana mikate yake saba ambapo huenda akanisaidia pindi ya kwangu ikiisha. Nikamsaidia kutoka pale na kujanae pembeni kabisa ya lile pango ambapo harufu za wafu hazifiki kwa kasi.

 

Siku ile usiku nilipolala ghafla nikasikia sauti ya mnyama anayechimba, nikasogea vizuri ila kwa kuwa ni kiza nisione vyema. Nikamwacha akaenda kule kwenye wafu na kuanza kula mizogo. Aple nilipo nikajisemea kuwa sasa huenda hii ndio nusura. Mnyama yule akala mizoga na muda wake ulipofika akatoka. Mimi nikawa namfatilia kwa nyuma usiku ule, tukapita njia nyembamba sana hatimaye akatokea baharini. Basi nikarudi tena kule pangoni kwenda kumchukuwa yule mwenzangu na kuchukuwa mali ambazo watu wamekuwa wakizikwa nazo kama mikufu ya dhahabu na thamani nyinginezo.

 

Nilibeba mzigo mkubwa sana wa mali za dhahabu na thamani nyingine nzuri. Tukatka mimi na mwenzangu yule na kwa bahati tukakutana na jahazi linaloelekea baghadad. Tulipanda mimi na mwenzangu yule. Tulipofika baghadad niliwahadithia kila kilichotokea na walishangaa sana kuniona nipo hai. Yule mwanamke nilompata kule nilisubiri eda yake ilipoisha kulingana na tamaduni za waislamu nikamwoamimi. Kwa hakika safari hii nimepata faida sana na mafunzo mengi.

 

Sin bad alipomaliza hadithi hii ya safari yake ya nne akamwambia Sinbad mbeba mizigo kuwa awahikesho ajesikia yalompata kwenye safari ya tano. Safari hii ya tano kuna matukio kadhaa yalinikuta hivyo uwahi mapema. Kisha akampatia pesa kwa ajili ya matumizi ya siku ile na ijayo. Watu wote wakatawanyika.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 875


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA MFANYABIASHARA NA JINI
Soma Zaidi...

Kwisha kwa chakula
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad Soma Zaidi...

HADITHI ZA SINBAD
Soma Zaidi...

HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE Basi tambueni enyi rafikizangu kuwa mimi na waziri wangu huyu hatutokani na familia za kifalme wala mimi baba yangu hahusiani hata kidogo na ufalme. Soma Zaidi...

SAFARI YA NNE YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA NNE YA SINBAD Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara. Soma Zaidi...

HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE. Soma Zaidi...

MFUGAJI NA MKEWE
Download kitabu Hiki Bofya hapa KISA CHA MFUGAJI NA MKEWE. Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WATATU NA WANAWAKE WA BAGHADAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa HATITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME NA WANAWAKE WA BAGHDAD Hapo zamani katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na mbeba mizigo maarufu sana. Soma Zaidi...

SAFARI YA SABA YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SABA YA SINBAD Walipokusanyika siku ilofata Sinbad akawaambia kuwa kilichofanya nikavunja ahadi yangu ya kutosafiri tena ni kauli ya Sultani Nilipopunzika kwa muda wa miezi miwili nilipata habari kuwa Sultani Soma Zaidi...

TONGE LA MWISHO
Download kitabu Hiki Bofya hapa KWISHA KWA CHAKULA Watu waliaanza kumaliza vyakula vyao na wakaanza kufa baada ya siku kadhaa. Soma Zaidi...

Usaliti unaanza hapa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya Khalid mwenye kuneemeshwa na Jalid
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...