Misingi na Maadili Katika Uislamu

5.

Misingi na Maadili Katika Uislamu

MFUMO WA JAMII YA KIISLAMU

5.1. Misingi na Maadili Katika Uislamu

Maana ya Maadili

Ni mwenendo na tabia inayomfikisha mwanaadamu katika hadhi yake yak ukhalifa na kufikia lengo la kuumbwa kwake.


Mtazamo wa Makafiri juu ya Maadili

Wanafalsafa wa kikafiri wamejaribu kutoa majibu ya maswali ya msingi yafuatayo;

1) Ni lipi lengo kuu la maisha?

2) Ni zipi chem.-chem tunazozitegemea kutambua yapi mema na yapi maovu?

3) Nani msimamizi wa maadili katika jamii?

4) Ni kipi kichocheo kinachowafanya watu katika jamii wawe na maadili?



Udhaifu wa majibu ya maswali haya

1) Lengo kuu la maisha hapa duniani ni;

1. Kuishi maisha yenye furaha ' Je, ni furaha ya nini, ya aina gani, ya nani?

2. Kufikia utimilifu ' Je, ni upi utimilifu?, wa nini? wa nani?, na kivipi?

3. Kutimiza wajibu kwa lengo la kutimiza wajibu ' Je, ni lipi hilo lengo?, nani kaliweka?, lina maana gani?




2) Utambuzi wa mema na maovu ni;

1. Kwa kutumia uzoefu (human experience) ' Je, ni uzoefu wa nani? wa nini?

Na kwa muda gani?

2. Kwa kutumia silka zetu (intuition) ' Je, tutegemee akili ya nani? kizazi kipi?

3. Kwa kufikiri na kuhoji (rationalism) ' Je, ni fikira zipi na za nani?



3) Msimamizi wa maadili ni;

1. Kuwa yatasimamiwa na lengo husika ' Je, lengo lipi ndio sahihi? n.k.

2. Kanuni zinazooana na hoja, akili (law of practical reason) ' Je, ni akili ya nani itumike? Na kivipi?
3. Serikali kwa kutumia vyombo vyake.

4. Maoni ya watu katika jamii ' social pressure



4) Motisha wa Kufuata maadili ni;

1. Kutaka malipo na kuepuka adhabu (reward and punishment) ' Je, ni nani anayetoa malipo au adhabu?
2. Maumbile ya binaadamu kutii na kuheshimu sheria.



Hivyo, ni wazi kuwa majibu na hoja zote zinaudhaifu mkubwa sana na kamwe haziwezi kumwongozo mwanadamu kimaadili.


Mtazamo wa Uislamu juu ya Maadili

Udhaifu wa majibu ya makafiri juu ya maadili ni kutojua chanzo, hadhi na lengo halisi la mwanaadamu hapa ulimwenguni.
Hivyo, Uislamu unajenga maadili kwa kujibu maswali yafuatayo kwa usahihi;

1) Nini chanzo cha binaadamu? ' Ni Allah (s.w)

Rejea Qur'an (15:28-29)



2) Ni ipi hadhi ya mwanaadamu hapa ulimwenguni? ' Ni Khalifa, kiongozi wa

Allah (s.w). Qur'an (2:30-34).



3) Ni lipi lengo kuu la maisha ya mwanaadamu na vyote vinavyomzunguka?

- Mwanaadamu ameumbwa ili kumuabudu Allah (s.w). Qur'an (51:56).

- Viumbe vinavyomzunguka ni kumwezesha binaadamu kufikia lengo lake.

Rejea Qur'an (2:29), (17:70)

4) Ni ipi chem chem ya ujuzi wa mema na maovu?

- Ni Allah (s.w) kupitia Vitabu vyake na Mitume wake. Qur'an (57:25)

- Qur'an na Sunnah (Hadith za Mtume (s.a.w))



5) Ni nani msimamizi wa maadili katika?

- Ni imani thabiti juu ya Allah (s.w), siku ya mwisho na nguzo za imani.

Rejea Qur'an (33:36)

- Mamlaka na Dola ya Kiislamu.

Rejea Qur'an (22:41)

6) Ni kipi kichocheo cha watu Kufuata maadili katika jamii?

- Ni kuhofu adhabu ya Allah (s.w) duniani na akhera

Rejea Qur'an (89:25-26)

- Kutarajia msamaha na malipo ya pepo maisha ya akhera.

Qur'an (9:111), (61:10-13)

- Kuhofu mamlaka ya Dola ya Kiislamu.





                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 300

Post zifazofanana:-

Darsa za sira (maisha ya mtume jaribio la 01
Soma Zaidi...

Kitabu Cha Quran na sayansi
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA MADD YAANI KUVUTA HERUFI KWENYE USOMAJI WA QURAN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA
Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg. Soma Zaidi...

Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga. Soma Zaidi...

Hatua na Mambo (Taasisi za Kisiasa) za msingi alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah
Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah. Soma Zaidi...

UKITAKA KUOMBA BASI MUOMBE ALLAH, UKIMKUMBUKA WAKATI WA RAHA ATAKUKUMBUKA WAKATI WA DHIKI, SHIDA NA TAABU
' ' ' ' ' ' ' ' ': "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': '... Soma Zaidi...

Welcome to Online School
Soma Zaidi...

UTARATIBU WA KULEA MIMBA
Soma Zaidi...

game
Karibu kwenye uwanja wa Game. Soma Zaidi...

Kuangamia kwa Mtoto na Mke wa Nuhu(a.s)
Tukirejea Qur'an (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a. Soma Zaidi...

Maana ya Mirathi na kurithi katika uislamu
Maana ya MirathiMirathi katika Uislamu ni kanuni na taratibu alizoziweka Allah (Sw) katika kuwagawawia na kuwarithisha familia na jamaa, mali aliyoiacha marehemu. Soma Zaidi...