Nguo zinazovaliwa kwenye chumba cha upasuaji na kazi zake

Posti hii inahusu zaidi nguo za kuvaliwa kwenye chumba cha upasuaji na kazi zake, hizi ni nguo ambazo wahudumu wa afya wanapaswa kuzivaa wakati wa upasuaji kwa ajili ya kuwakinga na Maambukizi kati ya wahudumu wa afya na wagonjwa pia

Nguo zinazovaliwa kwenye chumba cha upasuaji.

1.Kofia

Hii ni mojawapo ya nguo inayokaliwa kwenye chumba cha upasuaji, kofia yenyewe huwa mara nyingi imeshinwa kwa nguo, kazi yake ni kuzuia nywele kutoka kwenye kichwa cha mhudumu kuingia kwa mgonjwa wakati wa upasuaji, kwa hiyo kila mhudumu anapaswa kuivaa hii kofia kwa kufanya hivyo Maambukizi yataweza kupungua na kuepuka kuwepo kwa magonjwa yadiyotegemewa.

 

2.Nguo nyingine ni Maski au kwa lugha nyingine tunaweza kuita Barakoa.

Mask au barakoa uvaliwa na kufunika sehemu za mdomo, pua kwa hiyo kazi yake ni kuzuia mate kudondoka wakati wa upasuaji au hewa kutoka mdomoni inaweza kuwa na wadudu kwa hiyo ikasababisha wadudu kuingia kwenye sehemu ambayo imefunguliwa na kuleta Maambukizi au pengine mhudumu anaweza kupiga chafya na kusababisha wadudu kusambaa, lakini kama kuna Maski hakuna kitu chochote kinachoweza kutokea mdomoni au puani.

 

3.Nguo nyingine ni apron.

Hivi ni nguo ambayo uvaliwa juu ya gauni, nguo hii kazi yake ni kuzuia damu au majimaji kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu, kwa sababu wakati mwingine mgonjwa anaweza kuwa na Maambukizi na yakifika kwa mhudumu moja kwa moja yanaweza kusababisha Maambukizi kwa mgonjwa kwa hiyo ni lazima mhudumu kuvaa hii apron ili kuepukana na Maambukizi.

 

4.Nguo nyingine ni gauni.

Hii nayo ni nguo inapaswa kuvaliwa wakati wa upasuaji kwa sababu ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu au kutoka kwa mhudumu kwenda kwa mgonjwa, kwa hiyo kila mhudumu ni lazima kuvaa hii nguo hili kuepukana na Maambukizi ya magonjwa mbalimbali yanayoweza kusambaa kwa damu au kwa maji maji kama vile Ukimwi, homa ya ini na magonjwa mengine mengi.

 

5.Nguo nyingine ni boot au viatu vilivyofunikwa.

Pia nazo zinapaswa kuvaliwa wakati wa upasuaji kwa sababu uzuia Maambukizi kwa mfano kama kuna sindano imedondoka chini kwa bahati mbaya isiweze kuingia moja kwa moja kwenye mwili bali Uchoma juu ya viatu kwa sababu pengine mgonjwa anaweza kuwa na magonjwa ya kuambukiza kama sindano ikichoma juu ya boot ni vizuri kuliko kuchoma moja kwa moja kwenye ngozi.

 

6.Nguo nyingine ni gloves.

Pia nazo uvaliwa wakati wa upasuaji kwa sababu uzuia maambukizi kutoka kwa mhudumu kwenda kwa mgonjwa na kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu, hizi gloves kama zikichafua inabidi zibadilishwe ili zivaliwe nyingine kwa kuepuka Maambukizi kwa hiyo nazo zinapaswa kuvaliwa kwa mda wake na kwa sheria zake.

 

 

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Afya File: Download PDF Views 1499

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

YANAYOATHIRI AFYA KUTOKANA NA VIZAZI, FAMILIA NA KURITHI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
MAANA YA AFYA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
ITAMBUE SARATANI CHANZO CHAKE, DALILI NA KUKABILIANA NAYO

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
YANAYOATHIRI AFYA KATIKA MAZINGIRZ

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Darsa za Afya

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Kitabu cha Afya 04

Afya inaweza kuathiriwa na vitu vingi sana. Hapa tutaendelea kuona mabo zaidi yanayoathiri afya yako.

Soma Zaidi...
KITABU CHA MATUNDA

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
ZIJUWE FIGO, KAZI ZA FIGO NA NAMNA YA KULINDA FIGO DHIDI YA MARADHI

Je unatambuwa namna fgo inavyofanya kazi, unazijuwa kazikuu za fogo mwilini, na je unajuwa namna ya kujilinda dhidi ya maradhi ya figo?. Basi makala hii itakujuza kuhusu masomo haya1

Soma Zaidi...