picha

Nguzo za Imani kwa mujibu wa mafunzo ya kiislami.

Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu nguzo sita za imani katika Uislamu.

NGUZO ZA IMANI

Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:

1 Kumuamini Allah (s.w).

2 Kuamini Malaika wake.

3 Kuamini Vitabu vyake.

4 Kuamini Mitume wake.

5 Kuamini Siku ya mwisho.

6 Kuamini Qadar yake.

 

Hawi Muumini wa Kiislam yule ambaye amekanusha angalau moja ya nguzo hizi kama inavyobainika katika Qur-an:

 

“... Na mwenye kumkanusha Allah (s.w) na Ma la ika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho., basi bila shaka amepotea upotofu ulio mbali (kabisa)” (4:136)Mtu hatakuwa Muumini kwa kutamka tu hizi nguzo sita, bali pale atakapozijua kwa undani na kuendesha maisha yake yote kwa misingi ya nguzo hizi.

 

Tunazifahamu nguzo hizi sita kutokana na Hadith ya Mtume (s.a.w) iliyosimuliwa na Umar (r.a) kama ifuatavyo:Siku moja tulipokuwa tumeketi pamoja na Mtume (s.aw.) alitutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe kama theluji na nywele zake nyeusi sana, hakuwa na dalili zozote za msafiri, ingawa alikuwa mgeni kwetu sote.

 

Halafu alikaa mbele ya Mtume (s.a.w) hali magoti yake yakikabiliana na yale ya Mtume na akaweka mikono yake katika mapaja ya Mtume na akasema:”Ewe Muhammad nifahamishe juu ya Uislamu ” na Mtume akasema ; “Ni kushuhudia ya kuwa hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah, Kusimamisha swalaa, kutoa Zakat, Kufunga Mwezi wa Ramadhani, Kuhiji Makkat kwa mwenye kuweza” Halafu yule mgeni akasema “umesema kweli”. Tukastaajabu kwa nini aliuliza halafu akasadikisha.

 

Halafu akasema; “Nifa ham ishe juu ya Iman ”. Mtume akasema : “Ni kumuamini Mwenyezimungu na, Ma la ika wake , Vitabu vyake, Mitume wake, Siku ya Mwisho na Qadar, Kheri na shari yake.

 

Kisha akasema nifahamishe juu ya Ihsaan” Akasema “Ni Kumuabudu Allah kama kwamba unamuona, ikiwa wewe humuoni yeye anakuona ” Halafu akasema nifahamishe juu ya Kiyama ” Akasema: “Hajui mwenye kuulizwa juu ya hilo zaidi ya mwenye kuuliza.

 

Akasema “Nifahamishe dalili zake. Mtume akasema: “Ni wakati ambapo mjakazi atamzaa bibi yake, na utakapowaona wachungaji masikini wanaposhindana kujenga maghorofa. “Yule mgeni alipoondoka, Mtume alikaa kimya kwa muda kisha akasema: “eweUmar, unamfahamu muulizaji?’ Sote tukamjibu kuwa Allah na Mtume wake wanajua zaidi. Mtume akasema “Huyo ni Jibriil amekuja kuwafundisheni dini yenu” (MUSLIM) 

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2022/12/20/Tuesday - 10:09:03 am Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 2658

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 web hosting    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)

"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu

Soma Zaidi...
Taathira ya Imani ya Malaika katika maisha ya kila siku

Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini.

Soma Zaidi...
Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake

Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu.

Soma Zaidi...
(c)Vipawa vya Mwanaadamu

Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine.

Soma Zaidi...
Udhaifu wa mtazamo wa makafiri juu ya dini dhidi ya mtazamo wa uislamu

Somo Hili linaeleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Makundi ya dini za wanaadamu

Kwenye kipengele hichi tutajifunza makundi ya dini za watu. Na makundi hayo ni matatu.

Soma Zaidi...
Mwanadamu hawezi kuishi bila dini kutokana na vipawa alivyooewa na Allah

Je ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya kuwa na dini?. Vipawa alivyopewa na Allahni jibu tosha juu ya swali jilo

Soma Zaidi...