Nguzo za swala.
Kipengele hiki kinaelezea nguzo mbalimbali za kuswali.
- Ni vile vipengele vinavyokamilisha swala kama ifuatavyo;
- Nia (dhamira moyoni).
- takbiira ya kuhirimia
- kusoma suratul-Fatihah
- kurukuu
- kujituliza katika rukuu
- kuitidali
- kujituliza katika itidali
- kusujudu
- kujituliza katika Sijda
- kukaa kati ya Sijda mbili
- kujituliza katika kikao kati ya sijda mbili
- kusujudu mara ya pili
- kujituliza katika sijda ya pili
- kukaa Tahiyyatu
- kusoma Tahiyyatu
- kumswalia au kumtakia rehema na amani Mtume (s.a.w) na waislamu
- kutoa salaam
- kufuata utaratibu huu (1-17) kwa mfuatano
- Makundi manne ya nguzo za swala
- Nia.
- Nguzo za matamshi (visomo)
- Takbiira ya kuhirimia swala
- Kusoma Suratul-Fatihah
- Kusoma Tahiyyatu
- Kumswalia Mtume (s.a.w)
- Kutoa Salaam
- Nguzo za vitendo
- Ukiondoa nguzo ya ‘Nia’ na ‘kufuata utaratibu’ zilizobaki ni nguzo za vitendo.
.Kufuata utaratibu
- Ni yale mambo akiyafanya mwenye kuswali, hupandisha daraja ya swala yake
- Kuinua viganja vya mikono usawa wa mabega
- Kusoma dua baada ya Takbiira ya kuhirimia
- Kuanza kwa “Audhubillah” kabla ya kusoma Suratul-fatihah
- Kuitikia “Aamin” baada ya kumaliza kusoma Suratul-Fatihah
- Kusoma aya za Qur’an baada ya kusoma suratul-Fatihah rakaa mbili za mwanzo
- Kusoma Tasbih, Tahmid na dua katika rukuu, itidali, sijda, n.k.
- Kukaa na kusoma Tahiyyatu kila baada ya rakaa mbili.
- Kusoma dua baada ya kumswalia Mtume (s.a.w).
- Namna ya kutekeleza Nguzo na Sunnah za Swala hatua kwa hatua
Rejea EDK Kitabu cha 1, Sekondari, Uk. 100-110
- Sijda ya kawaida katika swala
- Sijdatut-Tilaawat (Sijda ya kisomo) – ni Sijda ya sunnah ailetayo msoji au msikilizaji wa Qur’an pale atakaposoma aya inayotaja sijda.
Aya za sijda ndani ya Qur’an ziko 15.
(7:206), (13:15), (16:50), (17:109), (19:58), (22:18), (22:77), (25:60), (27:26), (32:15), (38:24), (41:38), (53:62), (84:21) na (96:19).
- Sijdatus-Sah-wi (Sijda ya kusahau) – ni sijda anayoileta mtu kabla ya kutoa salaam ili kufidia kitendo cha sunnah alichokisahau katika swala.
- Mambo yanayobatilisha (yanayoharibu) Swala
- Kutoelekea Qibla bila dharura (udhuru) wowote kisheria.
- Kupatikana na hadathi kubwa (hedhi/nifasi), ndogo (kutengukwa udhu) au ya kati na kati (janaba).
- Kufikwa na najisi mwilini, nguoni au mahali pa kuswalia.
- Kuvukwa na nguo ukawa uchi – mgongoni, kiunoni, kitovuni, n.k. (tahadhari kuvaa mashati mafupi, madogo kwa wanaume).
- Kusema au kutamka makusudi walau herufi moja isiyo na mahusiano na ibada ya swala.
- Kula au kunywa chochote hata kwa kusahau.
- Kufanya kitendo/jambo lisilohusiana na swala mfululizo mara tatu.
- Kuacha nguzo yeyote ya swala.
- Kuzidisha nguzo yeyote ya swala makusudi.
- Kumtangulia imamu au kumchelewa (ukiwa maamuma) kwa nguzo mbili za kimatendo mfululizo na makusudi.
- Kutia nia ya kuikata swala au kujishauri moyoni uikate swala au usiikate.
- Kuwa na shaka kuwa umetimiza au haujatimiza sharti au nguzo yeyote ya swala.
- Kupotewa na akili au kulala ndani ya swala.
- Kutoa salaam makusudi kabla ya kuisha swala.
- Kuswalishwa kwa asiyekuwa muislamu.
- Kukhalifu (kutofuata) utaratibu wa Nguzo za swala katika mpangilio wake.
- Kuleta dua ya kuomba kitu cha haramu au muhali.
- Kumshirikisha Allah (s.w) kwa kuleta dua au maombi.
- Khushui (Unyenyekevu) katika Swala
Ni jambo la tatu katika kusimamisha swala
Maana ya Khushui – Ni kujituliza kimwili na kifikra na kuzingatia yale mja anayotenda na kusema katika swala.
- Namna ya kupata Khushui katika Swala1.Kuutuliza mwili
- Utulivu wa mwili hupatikana kwa kutojipapasa papasa, kutochezesha viungo na kuangalia pale tu unaposujudia.
2.Kuzituliza fikra (moyo)
- Fikra hutulia kwa kurejesha na kubakisha mawazo yote ndani ya swala kuanzia mwanzo hadi mwisho wa swala.
3.Kuwa na mazingatio
- Mazingatio hupatikana kwa kujua maana pamoja na kuwa makini na kile unachokisema au unachokitenda ndani ya swala.
- Namna ya kufikia Lengo la Swala
- Ni kutekeleza sharti zote za Swala kikamilifu kabla ya kuanza kuswali.
- Ni kutekeleza kikamilifu nguzo zote za swala kuanzia mwanzo hadi mwisho wa swala.
Rejea Qur’an (29:45), (20:14), (7:205), (107:4-6).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali
Nyuma
Endelea
Umeionaje Makala hii.. ?
Nzuri Mbaya Save
Author:
Rajabu 
Tarehe:
2022/01/14/Friday - 08:01:34 am
Topic:
Fiqh
Main:
Dini
File:
Download PDF
Views
3598
Share On:
Share follows: 0 |
Unique share links followed: 0
Post zinazofanana:
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kufanya suluhu katika ndoa.
Soma Zaidi...
Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi
Soma Zaidi...