Menu



Nguzo za swaumu (kufinga)

Hapa utajifunza nguzo kuu za swaumu. Kama hazitatimia nguzo hizi basi swaumu itakuwa ni batili.

Nguzo za Funga

Nguzo za funga ni mbili: Kutia Nia na kujizuilia na kila chenye kufunguza tangu mwanzo wa alfajiri mpaka kuingia magharibi.Nia ni dhamira anayokuwa nayo mtu moyoni mwake kuwa atafunga. Nia ya funga ya faradhi inatakiwa iletwe kabla ya Alfajir, kwa mnasaba wa Hadith ifu atayo:

 


Bibi Hafsah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: ambaye hakunuia kufunga kabla ya alfajir, hana funga. (Tirmidh, Abu Daud, Nis a i).

 


Ama nia ya funga za sunnah, inaweza kuletwa mchana iwapo mtu hajala chochote tangu alfajir kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:

 


Aisha, Mama w a Waumini (r.a) ameeleza: Mtume (s.a.w) alikuja kwangu siku moja akaniuliza: Una chochote (cha kula)? Nilijibu: Hakuna. Kisha akasema: “Basi nitafunga.” Siku nyingine alikuja tena kwetu tukamuambia: Mtume wa Allah, tumeletewa zawadi ya Hais (aina ya chakula cha mchanganyiko wa Tende na Siagi). Kisha akasema: “Nionyeshe, nilifunga tangu asubuhi. Kisha alikula chakula kile.” (Muslim).

 


Katika Hadith hii tunajifunza mambo mawili. Kwanza tunajifunza kuwa mtu anaweza kunuia funga ya sunnah mchana kabla ya adhuhuri, iwapo atakuwa hajala chochote tangu alfajiri.

 


Pili, tunajifunza vile vile kutokana na Hadith hii kuwa mtu anaruhusiwa kuvunja funga ya sunnah pasi na sababu ya kisharia.

 

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 956

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Faida za kuswali swala za sunnah

Posti hii inakwenda kukufundisha kuhush swala za sunnah.

Soma Zaidi...
NI ZIPI NGUZO NA SHARTI KUU ZA SWALA ILI IKUBALIWE

Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.

Soma Zaidi...
msimamo wa uislamu juu ya kupanga uzazi na uzazi wa mpango

Msimamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzaziKama tulivyoona, msukumo wa kampeni ya kudhibiti kizazi, umetokana na mfumo mbaya wa kijamii na kiuchumi ulioundwa na wanadamu kutokana na matashi yao ya ubinafsi.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kuelekea qibla katika swala.

Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla.

Soma Zaidi...